Bonge La Afya Profile picture
Elimu, Maarifa, Mijadala, na Taarifa za afya.

Sep 21, 2020, 7 tweets

1/7: Jamii inaweka msukumo mkubwa sana kwa dada zetu "KUOLEWA", Msukumo unaoambatana na kikomo cha miaka kwamba akifika miaka fulani awe ameolewa.

Kama kuolewa ni jambo muhimu kiasi hiki, kwa nini hatuwaandai kuoa/kuolewa tangu mashuleni?

2/7: Mbaya zaidi mategemeo ya wanajamii wengi ni kuwa binti huyu atakua "MKE BORA". Binafsi naona sio sawa, sio sawa kwa maana kama jamii tunajisahau sana. Unawekaje mategemeo makubwa kama haya wakati hufanyi juhudi zozote kuhakikisha mtoto huyu anakua katika njia bora.

3/7: Napongeza taasisi nyingi zilizoweka nguvu katika kumnyanyua mtoto wa kike kutoka katika mkandamizo wa haki zao katika jamii, Swali langu kwenu kama tunavyopambana na hedhi salama lini tutaongelea NDOA? Hatuoni kama ni muhimu kuliwekea nguvu swala hili?

4/7: Mtoto wa kike anapokua anakua, wazazi wengi humkemea na kumfundisha kuwa wanaume ni wabaya na hatakiwi kuwazoea au hata kuwasogelea. Ila akikua unamtaka aolewe na mwanaume huyu huyu eti kisa umri umeenda.

Kwa nini tusiwakuze watoto wetu kwa kuwaelekeza ukweli?

5/7: Naweza kusema jamii ni sababu ya ndoa nyingi kuyumba/kuvunjika. Kwanza ingewezekana hili jambo la kuoa/kuolewa lisiwe jambo la jumuiya bali jambo la familia. Tuwaache mabinti zetu kufanya machaguo yaliyo sahihi kwa wakati sahihi.

6/7: Angalau basi kabla hatujaweka msukumo huu tutengeneze utaratibu wa kuwaelimisha mabinti zetu ili baadae watakapo kuwa na uwezo wa kujifanyia maamuzi, wafanye maamuzi sahihi kwa manufaa ya maisha yao.

7/7: Turudishe mila za mama zetu kuongelea jando, utandawazi umebadirisha mambo mengi sana, zamani tuliona watoto wa kike wakijipikilisha na michezo mingine, Hii ilikua namna ya kujifunza adabu ya mwanamke/mke katika nyumba.

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling