Kubalehe ni hatua muhimu sana kupitia ili kuweza kupata mtoto. Wastani wa kubalehe na kuvunja ungo kwa wasichana ni miaka 9-12 kwa sasa, ingawa miaka ya zamani ilikuwa kuanzia miaka 12-14. Wavulana huanza kubalehe wakiwa na miaka 12-14. #ElimikaWikiendi
Mbegu za mwanaume zina kromosomu (nyuzi nyuzi katika kiini seli cha kila kiumbe ambazo hubeba viiniurithi yaani jeni) aina mbili X na Y. Mayai ya mwanamke yana kromosomu aina moja tu ya X. #ElimikaWikiendi
Kromosomu X ya mwanaume ikiungana na kromosomu X ya mwanamke hupatikana mtoto wa kike ila kromosomu Y ya mwanaume ikiungana na kromosomu X ya mwanamke hupatikana mtoto wa kiume. #ElimikaWikiendi
Uovuleshaji ni kipindi ambacho mwanamke hutoa mayai na ndicho kipindi ambacho mwanamke hushika mimba kirahisi. Kipindi hiki hujulikana pia kama siku za hatari ambapo inashauriwa mwanamke akutane kimwili na mwanaume anayetaka kuzaa naye. #ElimikaWikiendi
Vile hisia za tendo la ndoa zinavyokuwa juu na kufika kileleni hufanya mayai na mbegu za kiume kutoka kwa ubora wake. Iwapo yai litarutubushwa na kisha kujikita katika mfuko wa uzazi basi mimba itatungwa. Iwapo yai halitarutubishwa hutoka nje kama damu ya hedhi. #ElimikaWikiendi
Kwanini wenzi wengine hawapati mtoto? Wanandoa wenye matatizo ya uzazi (wasiopata mtoto) ambao vipimo havionyeshi tatizo basi watakuwa wanakosea namna ya kufanya tendo la ndoa. Ili kupata mimba kirahisi tendo la ndoa linapaswa kufanyika kwa furaha na ufundi wote. #ElimikaWikiendi
Epuka mkao wa mwanamke kuwa juu wakati mkijamiana kwani hufanya mbegu zimwagike kwa kufuata mteremko. Pia, jaribu kuweka mto chini ya kiuno ili kukiinua na kufanya mbegu ziingie ndani kwa urahisi. #ElimikaWikiendi
Unapotaka kushika mimba acha au punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya. Uvutaji sigara hupunguza kiwango na uzito wa shahawa kwa wanaume. Uzito wa shahawa hupungua kwa asilimia 22-57 kwa wale wanaovuta sigara. #ElimikaWikiendi
Uwezo wa shahawa kuogelea kwenye mirija ya uzazi ya mwanamke pia nao hupungua kwa asilimia 20 kwa wale wanaovuta sigara ikilinganishwa na wale wanaume wasiovuta sigara. #ElimikaWikiendi
Tafiti zingine zimethibitisha kuwa wanaume wanaovuta sigara wana asilimia kubwa ya kutoa shahawa ambazo hazina maumbile mazuri au ya kawaida na hivyo kuongeza uwezekano wa mimba kutoka (spontaneous abortion) au kuzaa mtoto mwenye maumbile ambayo sio ya kawaida. #ElimikaWikiendi
Tafiti mbalimbali pia zimethibitisha kuwa uvutaji sigara huharibu mirija ya seminiferous tubules ambayo hupatikana kwenye korodani na ni sehemu ambapo shahawa hutengenezwa, hivyo uharibifu wake hupunguza wingi na uzito wa shahawa. #ElimikaWikiendi
Mnawezaje kupata mtoto wa kiume? Ili kuongeza uwezekano wa kupata mtoto wa kiume, wenzi wanapaswa kula vyakula kama mihogo, magimbi, samaki, nyama, pweza, matunda kama tikitikimaji, ndizi, maparachichi n.k. #ElimikaWikiendi
Mwanamke kufika kileleni kabla ya mwanaume huongeza uwezekano wa kupata mtoto wa kiume kwa maana mwanamke kutoa ute rafiki kwa mbegu za kiume kuishi na kufikia yai mapema kwa vile kwenye uke kuna asidi inayoweza kuua mbegu haraka. #ElimikaWikiendi
Ili kupata mtoto wa kiume wenzi wanashauriwa kufanya tendo la ndoa siku ya uovuleshaji wenyewe mnaita danger day ambapo yai linakuwa karibu kwa mbegu ya kiume kukutana nalo. #ElimikaWikiendi
Ili kuongeza uwezekano wa kupata mtoto wa kiume wenzi napaswa kufanya tendo la ndoa kwa mtindo ambao unaruhusu uume kuingia ndani zaidi (deep penetration) kama mguu begani 😁 kitu kitakachorahisisha mbegu kufika haraka kwa yai. #ElimikaWikiendi
Mwanaume anapaswa kuvaa nguo za ndani zisizobana zitakazoruhusu sehemu za siri kupata hewa safi hivyo kufanya mbegu kuwa na ubora mkubwa. #ElimikaWikiendi
Mwanaume anapaswa kutofanya tendo la ndoa kwa angalau wiki moja kabla ya siku ya uovuleshaji (denja dei 😁), hii itafanya idadi ya mbegu za kiume kwenye manii kuwa kubwa. #ElimikaWikiendi
Jinsi gani mnaweza kupata watoto mapacha? Wanawake wote wana nafasi sawa ya kupata mapacha, inakadiliwa mimba 1 kati ya 250 huwa ni ya mapacha. Mwenye uwezo wa kusababisha watoto mapacha ni mwanamke pekee. #ElimikaWikiendi
Mwanamke pacha au ana ndugu wa familia mapacha ana uwezekano wa kupata mapacha sababu ana uhusiano wa moja kwa moja. Kuna aina mbili kuu za mapacha, mapacha wanaofanana na mapacha wasiofanana. #ElimikaWikiendi
Mapacha wasiofanana hutokana na mayai mawili yaliyorutubishwa na mbegu 1, mapacha wanaofanana wanatokana na yai 1 lililogawanyika mara 2. 1/3 ya mapacha wote hufanana. Mwanamke yeyote anaweza kupata mapacha hata kama kwenye familia yake hakuna historia hiyo. #ElimikaWikiendi
Wanawake wa kabila la Yoruba kutoka Naijeria ndio wanaongoza kwa kuzaa mapacha duniani. Watafiti wamehusianisha uwezo huo wa kuzaa mapacha na ulaji mihogo & magimbi vitu vyenye kiwango kikubwa cha phytoestrogen inayoongeza uwezekano wa kutoa mayai zaidi ya moja. #ElimikaWikiendi
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.