James Munisi Profile picture
Creator & Innovator | Electronics & Telecom Engineer | Business Administrator | 1+1=11 | All about Techs | Founder @Njiwa_Store | We are @TOTTechs |#SimuZaNjiwa

May 14, 2023, 13 tweets

💨"Wandugu! Android 14 inakuja na ni nzuri mpaka naona inawafanya marafiki zangu wanaotumia iPhone waone wivu😅! Lakini msiwe na wasiwasi bado mimi ni rafki yenu nitawa-text kwa sababu tunakuja wawekea RCS kwenye iPhone"
Amesema #bardAI
Mimi nakuletea feature mpya za Android 14 twitter.com/i/web/status/1…

Android 14 ni version mpya ya simu zinazotumia operating system ya google. Ilitangazwa mwanzoni tarehe 20, february 2023 ambapo mpaka sasa hivi inaendelea kuboreshwa.

Android 14, tangu inze kutumika imefanyiwa maboresho kibao!
Zifuatazo ni features zilizo kwenye maboresho hayo!

1. New lock screen:
Mwonekano mpya wa lock screen ya android 14 umeboreshwa kwenye
■ Imekuwa rahisi kubadili na kuweka wigget, shortcuts na themes mpya
■ Unaweza badili mwonekano wa saa,kuongeza widget na kutengezeza shortcuts ya apps zako pendwa.
Angalia kwenye picha👇🏾

2. New Multitasking Mode:
Kwa multi tasking- mode mpya imeboreshwa zaidi ambapo now unaweza kufungua apps mpaka 4 kwa wakati mmoja na kuhama kati ya hizo apps kwa urahisi.

3. New privacy and Security features:
Kwenye privacy na security sasa utakuwa na access ya location yako na ku-contol kwa namna gani apps zingine zitatumia data zako hizo.

Hii itarahisisha usalama wa simu yako kwani hamna app itakua inatumia location bila wewe kujua

4. Support for lossless audio:
Sasa unaweza kusikiliza mziki unaoupenda bila kupoteza quality yoyote ya sauti. Hii inamaanisha utaweza sikiliza mziki na ala zake zote!.

5. Supports for 10-bit HDR:
Hii inamaanisha sasa unaweza kuangalia picha vizuri zaidi kwa wider range na kwa mng'aro zaidi. Hii ni sababu android inasaport 10- bit HDR

6. Android 14 will offer AI generated wallpaper:
Sasa taweza kutengeneza picha yako peke yako dunia nzima kwa kutumia Google's text to image deffusion model.
Hii itakuwezesha kutengeneza picha uitakayo kwa kuiambia AI kipi utahitaji na ifate design gani.

7. Updates to camera2 na CameraX extensions:
Hii itaboresha na kufanya urahisi wakati wa kupiga au kuchuoua videos sehemu zenye mwanga mdogo.
Angalia softawere hiyo inavyowasiliana na camera kwenye structure hapo chini

8. System share sheet with app actions
Kama unatumia android 14 utaona share sheet imeboreshwa.
Ambapo google sasa wanaifanya iwe official. hii hutumiwa na apps kutuma vitu kama links,Qr code, image na kadhalika

9. Maboresho kwenye Navigation button:
Hapa google wamefanya maboresho kwenye Muonekano wa navigation button. Na sasa unaweza force navigation button ya simu yako kuwa transparent (isiyo onekana)

By the way, imebakia miezi michache ili Android 14 ikamilike!.
Kujua kuhusu mambo yatakayo ongezeka kwenye android version 14 beta follow @NjiwaFLow kisha mfollow mwandishi @Rydx_017 then washa notification ili uwe wa kwanza kupata madini haya Muhimu...

Kujua ni simu gani zinapokea Android 14 beta kwa sasa niliandika uzi huu hapa chini 👇🏾

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling