My Authors
Read all threads
Fursa Adhim Msimu wa korona! Thread!

cc. @chapo255
@CarolNdosi
@Eric_Bernard94 Image
Tujikumbushe kidogo tu kwamba Covid_19 ilianza mwishoni mwa mwaka 2019, ambapo visa kadhaa vilianza kuibuka maeneo ya Uchina , Hasa katika jiji la Wuhan. Image
Pamoja na jitihada kadhaa ambazo zilichukuliwa tangu kipindi kile mpaka sasa ninapoandika uzi huu Bado Corona imebaki kua ni janga ambalo linausumbua ulimwengu, kama ni ndoto basi bado ni usiku wa manane.
Takwimu za Dubwana hili bado zinazidi kupaa ambapo mpaka uzi huu unaandikwa Dunia imetangaza takribani vifo 235,000 na visa vya washukiwa Milioni Tatu na Laki Tatu 3.3M vya janga hili.
Pamoja na kua na dubwana hili katika maeneo yetu maisha bado hayajasimama. Zipo fursa na Raslimali ambazo bado zinaendelea kutumika kila kukicha. Si hivyo tu Dunia ijipange kutokea mabadiliko makubwa sana kwenye Teknolojia, Ubunifu ,Malezi ,Utendaji kazi n.k Hatutarudi Tulipokuwa Image
Wewe pia unaweza kua shahidi kwamba pamoja na kupungua kwa baadhi ya huduma kama zile za uzalishaji katika maeneo mengi duniani, bado wapo watu wanaopambana kwa kila namna kujaribu kusogeza huduma zao karibu zaidi na wateja wao. Kwa tahadhari kubwa wamekua wakitumia Teknolojia Image
Ili kufikisha huduma zao karibu zaidi na jamii na wateja wao kiujumla. Mimi na wewe tunaweza tukawa tumeanza kunufaika kidogo na huduma hizi.
Wapo watu ambao walikaa na kufikiria sana kabla ya janga hili ambapo kwao msimu huu umekua wa mafanikio makubwa sana na huenda wakatoboa maisha kwasababu ya dubwana hili, hii inamaanisha kwamba Kampuni za kutoa Digital Services bado nyingi zinanufaika kupitia hali hii.
Tumeshuhudia makampuni kama Zoom,Google Cloud Next ’20, Tencent’s WeChat Work,DingTalk,Microsoft Teams,LogMeIn,Cisco(Webex) n.k yakipaa kwa kuongeza watumiaji wengi kwa siku mpaka wiki kuliko ilivyokua mwanzoni, kutokana na matumizi katika huduma za vikao vya mtandaoni. ImageImage
Si hivyo tu kuna wengine pia kwa namna moja au nyingine wameumia juu ya janga hili ikiwepo kupoteza kazi zao, na huenda wasizipate tena baada ya janga hili kuisha kwasababu mbalimbali ikiwemo kudorora kwa hali ya uzalishaji kutegemeana na huduma iliyokua inatolewa mwanzoni.
Wenye viwanda na biashara nyingi kwa sasa wanatizama ni kwa namna gani wanaweza kubadili mifumo ya uzalishaji kulingana na kasi ya sayansi na teknolojia, na kupunguza nguvu kazi ya watu yaani (Human Labour) mara baada ya janga hili. Image
Nadiriki kusema ya kwamba pamoja na kuwepo kwa sakata hili yapo masomo mengi tunayoweza kujifunza msimu huu ambayo kimsingi yanaweza kuwa na umuhimu sana janga hili linapoendelea hadi litakapokwisha. Ikiwemo Mabadiliko makubwa ya namna ya utendaji kazi kuliko ilivyozoeleka.
Huwezi jua huenda usirudi tena kazini kwa bosi wako, ila huo sio mwisho wa maisha, lazima uangalie ni kwa namna gani unaweza survive na kukabiliana na maisha na hali halisi.
Napenda kukusogezea Fursa kadhaa ambazo unaweza zijaribu msimu huu wa korona Image
1. Kutoa Huduma za Chakula mara baada ya kupita kwa dubwana hili. Sote tunaweza kubaliana kwamba chakula ni huduma ya msingi ambayo kila mmoja anaipata ili maisha yaendelee. Kutokana na mdororo, hofu na kuogofya kwa watu wengi msimu huu kama upo kwenye eneo la wazi
ambalo linaruhusu shughuli za kilimo, zalisha kwa wingi maana vyakula vitahitajika hata baada ya Corona, Watu wapo majumbani wanahitaji vyakula na huduma za vyakula zalisha kwa kuzingatia ubora. Waweza nufaika baadae. Mazao ya muda mfupi, Mboga mboga na matunda yaweza faa sana.
Nje na kilimo unaweza anza kufanya ufugaji japo kwa kuanza kulingana na ukubwa wa eneo lako. Ufugaji wa jamii ya ndege, (mfano kuku, kanga, bata na wengineo) yaweza kua moja ya sehemu kubwa ya fursa muhimu kwa msimu huu na mara baada ya Dubwana hili kuisha.
Serikali haijazuia uzalishaji zalisha huku ukizingatia tahadhari huenda huu ukawa wakati wako wa kutimiza ndoto zako za msingi. ImageImage
2. Jijenge na jiimarishe kujifunza ujuzi mpya na ubunifu. Badala ya kushinda na kukesha sana bila kuwa majukumu maalumu ya kufanya, Tenga muda jifunze maarifa mapya ambayo yanaweza kukujenga hata baada ya janga hili kuisha. Mtandao una mengi ya kukufundisha tumia fursa hii kupata
madini mapya ya kujijenga ki fikra. Soma kozi muhimu mtandaoni na zikufaidishe maishani. Msimu huu ndio wa kuja na njia mbadala za kutoa huduma ziwe za kuwasilisha bidhaa au huduma. Waweza tengeneza wazo zuri la biashara hasa ya kutoa huduma ambayo si lazima wote mkae ofisini.
3. Jifunze juu ya namna mabadiliko ya Teknolojia yanavyoathiri mifumo ya kazi nyingi ambazo zinamuhusu binadamu asilimia 100. Amini nakuambia huenda janga hili likafyekelea mbali ajira nyingi sana. Wapo wataalam, makampuni ya uzalishaji na wamiliki wa biashara watapata mawazo Image
mapya juu ya kutumia teknolojia mpya zitakazo waruhusu wa zalishe kwa muda mrefu na kwa gharama nafuu. Mapinduzi ya Viwanda kwa kupitia Sayani na Teknolojia yatakua makubwa, Amini kwamba kazi nyingi zitafanywa na mashine (ROBOTS) Badala ya binadamu je umejipanga? Image
5.Jifunze namna ya kua mbunifu. Ubunifu huu umejikita katika kujua je ni kipi jamii inachohitaji kwa wakati huo. Kuanzisha biashara ya kusambaza bidhaa ambazo ni adimu kwenye maeneo tofauti tofauti laweza kua jambo jema, tena lenye manufaa. Tambua uhitaji na ufanyie kazi. Image
6. Talanta yako na kipaji chako vyaweza kua vya msingi sana msimu huu. Ukiwa nyumbani endelea kujifunza zaidi vile unavyovipenda, mfano mziki, uandishi, kuimba n.k Vinaweza tumika baada ya Corona pia na kukusaidia kuendeleza maisha. Kipaji na Talanta vyaweza kuwa silaha kubwa. ImageImage
Mwisho, Pata muda wa kuwaza zaidi maisha baada ya Covid_19 , Wengi wanaumia kwa Misongo ya mawazo kipindi hiki wakiwaza na kuangalia idadi ya vifo tu, angalia fursa zinazoweza kutokea baada ya janga, Inaweza kukupa Tulizo la Mawazo kiasi. Usisahau Vitami C supplements Image
Mwanga wa jua na Kufuatilia kwa umakini yale tunayoelekezwa na wataalamu wa Afya.

Huu ni mwanzo Tu.

Rt & Share iwafikie na wengine.

MUNGU Ibariki Dunia, Afrika & Tanzania.
Ahsante. Image
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with WIlly

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!