Leo ngoja niwape tip kidogo ya uzoefu wa hizi kazi za Freelancing hasa kule Upwork
Fuatilia huu uzi🧵
Asilimia kubwa ya kazi Upwork na platform nyingine zinatangazwa na wateja walioko 'Ulaya na Marekani' wakitaraji kupata wigo mpana wa wauuza ujuzi mtandaoni hasa kutoka Asia/India
Kule kuna wauza ujuzi wako vizuri na wanatoa huduma nafuu sana ndio maana hata huyu mteja amejisahau hakuweka location preference ila kwenye kazi amekuwa biased na Freelancers wa India🤔👇
Sasa hapo inabidi uwe makini sana kufanya client assessment, attention to detail na ujua aina ya Freelancers wenzako unaopambana nao at global stage kupata kazi.
Kwa kifupi jaribu kuwa Smart unapomba kazi na jenga mazingira ya kuthaminisha muda na bei unazocharge na kujitofautisha na wengine kwa kutoa huduma ya uhakika, yenye viwango bila kusahau matumizi ya tools mbali mbali.
Tools muhimu kule Upwork ni pamoja na Calendly, Zoom and Loom maana hizi ziko integrated kwenye platform yao kwa ajili ya kupanga appointment, kufanya audio, video call na kurecord use case/proof of concept kati yako na mteja.
Mfano unaweza kutumia application au tool ya Loom kurecord proof or work au kumpatia maelekezo mteja na kujua kama ameview shared video (hapo utajua pia ameview proposal yako)
Mfano kazi hii mimi nimeomba na kwakuwa najua solution yake nimetumia Loom kurecord an overview of proof of work as proposed solution.
Submitted proposal with a Loom video record as proof of concept👇
Link to the Loom video hii hapa unaweza kuicheki na kupata picha jinsi ya kutumia katika niche yako. loom.com/share/9af20364…
Pia kwenye Loom mbali ma kujua kuwa mteja ameview proposal yako na recorded video (by %) una option ya kuweka Call-to-Action kama kumwambia akutumie ujumbe, kumualika kwenye Zoom call au hata kumuomba feedback👇