A-L-L-Y Profile picture
Sep 17 23 tweets 11 min read
Mitandao ina fursa nyingi sana, na moja ya fursa kwa vijana leo hii ni #blogging.

Kutengeneza $100 hadi $1,000 kwa mwezi kwenye blogu ni kitu kina wezekana kabisa.

Basi ungana nami katika #ElimikaWikiendi nikufundishe jinsi gani unaeza tengeneza pesa kwenye blogu.
Kwanza kabisa tuanze kwa kufahamu blogu ni kitu gani?

Blogu ni aina ya Mtandao unaokuwezesha kuandika makala, kuweka picha, videos na kadhalika katika mlolongo maalumu.

Blogu ni teknolojia inayowezesha watu kuchapa maoni na fikra zao katika mtandao.

#ElimikaWikiendi
Na blogu zipo za aina nyingi tu na zina endeshwa kwa kutumia majukwaa tofauti tofauti.

Endapo unataka kunza blog leo hii basi hii hapa ni makala inayo elekeza hatua kwa hatua nama ya kuanza blogu yako ndani ya dk 15 tu.

kidigitali.com/2021/09/Blogge…

#ElimikaWikiendi
Muhimu ufahamu kuwa kabla hujaanzisha blogu yako, unatakiwa uchague topic (Niche) ambayo blogu yako itajikita nayo.

Hapa ndipo msingi wa mafanikio ya blogu yako.

Chagua mada ambayo utaandika makala zenye kutatua changamoto au kutoa elimu.

#ElimikaWikiendi
Lakini ukiweza ku focus kwenye kutatua matatizo yaliyo kwenye hizi Niche. Basi huwezi kukosa pesa mtandaoni.

Wellness (Healthy)
Beauty and Cosmetics
Entertainments
Spiritual and Worship
Make Money Online
Investment and Technology
Relationship

#ElimikaWikiendi
Umesha chagua niche yako na umesha tengeneza blogu yako tayari.

Swali ni je! una pataje pesa?

Hapa ndipo wegi huwa wanajiuliza.. na leo katika #ElimikaWikiendi nita kupa mwongozo wa aina mbali mbali za jinsi unavyo weza tengeneza pesa na blogu yako.
Kuna njia mbali mbali za kutengeneza pesa kweye blogu na nitaenda kuzi chambua moja moja.

Njia ya kwanza ni kuweka Matangazo (Ads) kwenye blogu yako.

Tunapo ongelea matangazo, yako ya aina nyingi pia.

1. Matangazo ya Ads Network (Mfano. Google Adsense)

#ElimikaWikiendi
Ad Networks zipo nyingi sana ila kampuni zinazo lipa vizuri blogger ni kama vile Google Adsense, Adsterra, Ezoic, Media Vine hizi ni baadhi tu.

Ukijiunga na hizi kampuni wao wana weka matangazo yao kwenye blogu yako na wana kulipa.

#ElimikaWikiendi
2. Matangazo ya kampuni binafsi

Hii ni njia ambayo wewe binafsi kama una tafuta kampuni kadhaa na kufanya nao kazi ya kuwatangaza kupitia blogu yako.

Hii njia inatakiwa blogu yako iwe na ushawishi mkubwa ili uweze kuwa shawishi. Mfano mzuri ni Millard Ayo.

#ElimikaWikiendi
Njia nyingine ya kuingiza pesa kwenye blogu yako ni #AffiliateMarketing

Hii ina husu kutangaza bidhaa za watu wengine kwenye blogu yako na watu waki nunua bidhaa hizo basi una lipwa kiasi flani cha pesa (Commision)

Na hii ni njia moja nzuri sana.

#ElimikaWikiendi
Kuna kampuni nyingi sana za affiliate marketing ambazo kama blogger unaweza kujisajili nazo na ukaanza kuuza bidhaa zao kwenye blogu yako.

Unaweza kuanza hata na Amazon Associates au affiliate za kampuni binafsi pia.

#ElimikaWikiendi
Mimi binasi natumia zaidi kampuni ya Impact.com ambayo ina affiliates nyingi ndani yake.

Na kupitia blogu yangu na zi tangaza bidhaa zao na watu wanapo nunua basi mimi nalipwa asilimia kadhaa kutokana na mauzo hayo.

#ElimikaWikiendi
Affiliate marketing ni njia rahisi sana.. ebu fikiria kama unapata gawio la $5 tu katika kila mauzo... endapo ukiuza bidhaa 200 tu basi tayari umeingiza $1,000

Unaeza kusoma hii makala hapa ikakupa mwongozo wa affiliates nzuri.

kidigitali.com/2022/01/best-a…

#ElimikaWikiendi
Njia nyingine ya kuingiza pesa kwenye blogu ni Kuuza Digital products zako. Kama vile Course, eBooks au consultation.

Mfano mzuri kwenye blogu yangu mimi nauza ebooks, na fanya training za digital skills na pia natoa mentorship na watu wana lipia huduma hizi.

#ElimikaWikiendi
Muhimu ni uwe na stadi unazo weza kuuza kama huduma kwa watu.

Unaweza kutoa huduma ya kulipia kwenye blogu yako pia. watu wakalipia makala zako ili kuweza kuzisoma.

#ElimikaWikiendi
Tumeangalia njia ambazo unaeza pata pesa kupitia blogu yako.

Ili uwe na blogu yenye mafanikio mazuri kuna mambo muhimu sana yanatakiwa.

1. Blogu yako iwe na makala (Content) nzuri. Huwezi pata watembeleaji/wasomaji kama blogu yako haina maudhui mazuri.

#ElimikaWikiendi
2. Hakikisha una pandisha makala mpya mara kwa mara. Ili blogu yako ifanye vizuri ni vyema kuwa una weka makala mpya kila siku ili upate watembeleaji wengi na kukuta makala mpya.

3. Hakikisha una tumia vizuri mitandao ya kijamii kukuza blogu yako.

#ElimikaWikiendi
4. Muhimu zaidi ni kuwa, blogu yako inatakiwa itambuliwe na tovuti za utafutaji (Search engines) kama Google, bing na zinginezo.

Hii itakufanya upate watembeleaji kwa makla zako wakizi tafuta mitandaoni katika search engines.

Hivyo hakikisha una fanya SEO.

#ElimikaWikiendi
5. Hakikisha una fanya tafiti kujua ni maneno (Keywords) gani kwenye niche yako watu wana yatafuta sana na kuyaulizia ili iwe rahisi wewe kuandika kile watu wana kitafuta.

6. Jitahidi kuitangaza blogu yako watu waifahamu zaidi.

#ElimikaWikiendi
Je! Unataka kuanza blogu leo hii. Basi hizi ni hatua muhimu unazo takiwa kuzi fanya.

1: Chagua mada (Niche) ya blogu yako pamoja na jina la blogu.
2: Chagua jukwaa la blogu yako utakalo tumia (Blogger, WordPress or wix n.k)

#ElimikaWikiendi
3: Chagua domain name na kampuni ya ku host blog yako endapo uta tumia wordpress
4: Unda blogu yako kwa design nzuri
5: Anza kandika makala yako ya kwanza Write your first blog post

#ElimikaWikiendi
6: Share makala yako na watu kwenye social media waweze kuisoma
7: Monetize blogu yako kwa njia nilizo zitaja hapo awali
8: Peleka traffic ya kutosha kwenye blogu yako na ifahamike na wengi

#ElimikaWikiendi
Kwa Leo, Tuishie hapa!

Kama umeipenda thread hii:

1. Follow me @ally_eh kwa makala nyingi kama hizi.
2. RT iwafikie wengi zaidi.

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with A-L-L-Y

A-L-L-Y Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @ally_eh

Sep 16
HOW YOU CAN MAKE A CAREER BY WRITING CONTENT (Specifically Online content or blog articles for a Living)

If you wish to start your freelancing career as a content writer all you have to do is learn and practice writing.

Just write anything... Image
write whatever comes into your mind.

Write every day.

write anything, write on Twitter, in your diary. Just write and as you go on you get better and improve.
Then practice on various topics and start researching more writing styles and as you go you improve your writing, styles, and flow.

START with what you can afford.

1. Open a free blog (Blogspot.com) easy to use and free.
Read 11 tweets
Apr 30
Leo katika #ElimikaWikiendi nakuletea "Mambo Muhimu ya Kuzingatia kwa Vijana wanao Ingia kwenye FURSA za Mtandaoni."

Vijana wengi sana wana tamani au wameingia katika kuzisaka fursa mbali mbali za mtandaoni.

Basi ungana nami tuchambue mambo muhimu ya kuzingatia.
1. Jinsi ya Kuchagua kitu gani ujikite nacho mtandaoni.

Hapa ndipo wengi sana waka anza kukosea. Mtandaoni kuna mambo mengi sana.

Huwezi kujihusisha na kila kitu, hivyo ni muhimu sana kuchagua ni kitu gani ufanye.

#ElimikaWikiendi
Kuna fursa nyingi sana.

Mfano;
- Freelancing
- Blogging
- Affiliate Marketing

Na vingine vingi tu.

Hapa ndipo wengi hushindwa kuchagua nini hasa afanye. Hauzuiliwi kufanya vitu vingi ila jikite na vichache kwanza.

#ElimikaWikiendi
Read 17 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(