Discover and read the best of Twitter Threads about #DaktariMwandishi

Most recents (19)

Mjadala uliofanyika leo katika mkutano mkuu wa MEWATA kuhusu afya ya akili baada ya kujifungua, umenikumbusha mbali.
Siku moja napita round wodi ya watoto wachanga nawahimiza kina mama kunyonyesha watoto, mama mmoja aliniita “dokta ukimaliza njoo” #UZI #MEWATA2023
Nilipoenda akamchukua mwanae akanikabidhi mkononi akasema, “shogaangu hebu niangalizie mwanangu, maana mie sijielewi”
Nikamuuliza, “unajiskiaje” nikidhani labda ana shida ya mwili ili tuwaite watu wa wodi ya kina mama waje kumhudumia. Akasema, “yani nikimbeba hivi mtoto kumpa
maziwa, kuna sauti zinaniambia kabisa nimnyonge. Yani nawaza nimzibe pumzi afe. Sasa mi sitaki kumdhuru mwanangu, naomba unilelee tu”

Unajua hivi vitu ukivisoma kwenye vitabu vinaonekanaga kama utani fulani hivi hadi siku unakutana navyo. Nikawasiliana na in charge tukatoa
Read 13 tweets
When I saw a stream of blood down my leg, I knew right there and then; it’s happening! My worst nightmare was coming true and I couldn’t believe it because it was already days after delivery. I have NEVER been that terrified ALL MY LIFE.
This is my story: SURVIVING PPH #Thread 🧵
I tried to be calm, but I could hear my heart pounding in my ears. It felt like someone ripped out my heart and put it in speaker right next to my ears. I felt dizzy, so I sat down. I can’t tell if I was dizzy because of blood loss or the fear of becoming a statistic.
As we prepared to go back to the hospital, I tried so hard to appear calm; a big smile on my face but in my heart I was terrified. I knew it very well, PostPartum Hemorrhage is no joke. In a matter of seconds EVERYTHING COULD GO WRONG.
I asked for ONE thing: my rozary ring.
Read 24 tweets
Kuna safari hata ziwe fupi vipi, hazisahauliki. Hazisahauliki kwa mengi; watu uliosafiri nao, watu uliokutana nao, experience ya safari na mengine mengi.
Mimi safari hii pichani sitaisahau.
Nilipata wasaa wa kushare na @buguzi @NormanJonasMD @DrArabiFrank na @JuliethSebbaMD #UZI Image
Ilianza kama utani hivi, nikafahamishwa nimepata nafasi ya kufanya mafunzo Morogoro ambayo yaliandaliwa na @sikika1 na @tacaidsinfo
Na mimi mpenda safari na mpenda afya, naanzaje kukosa? Nikafungasha kibegi changu uelekeo mji kasoro bahari.
Moro bwana! Moro PAZURI NYIE! Basi tu. ImageImageImageImage
Katika mengi nilojifunza siku hizo mbili, kuna kitu kimoja kilichonivutia zaidi ya mandhari nzuri ya Morogoro, maana mara ya mwisho nilikuwa hapa ilikuwa ni trip ya Udzungwa na Mto Mawe.
Kitu hicho ni Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI Tanzania (ATF). Leo naomba niwashirikishe Image
Read 16 tweets
SEHEMU YA PILI #IjueChanjoNaDaktariMwandishi
Leo, saa 3 asubuhi, Rais SSH atazindua chanjo pale ikulu kwa kupata chanjo hiyo.
Wakati huo, tuendelee kujifunza kuhusu chanjo za COVID19 haswa aina ya Johnson&Johnson ambayo ndio imepokelewa. #UZI FUATILIA
#DaktariMwandishi
3. JE, NIKIPATA CHANJO YA COVID19 KUTANIFANYA NIWE NA SUMAKU (MAGENTIC)?

Hapana. Chanjo za COVID19 hazina uwezo wa kutengeneza "electromagnetic field" (uwezo wa wewe kuwa sumaku) na chanjo zote hazina metals.
Unaweza kuangalia nini kimo kwenye chanjo katika ukurasa wa CDC.
4. KWANINI BAADHI YA TAARIFA ZINASEMA TUMEPOKEA CHANJO YA JOHNSON&JOHNSON NA NYINGINE ZINASEMA "JANSSEN"?
Jina kamili la chanjo iliyopokelewa Tanzania kupitia mpango wa COVAX ni "Johnson&Johnson's Janssen(J&J/Janssen) COVID19 Vaccine" kwahiyo ni kitu kimoja wala si chanjo tofauti
Read 18 tweets
#IjueChanjoNaDaktariMwandishi
Bado naikumbuka siku ile ilipotangazwa chanjo ya kwanza ya COVID19, nilikuwa twitter, sikuwahi kufurahia matunda ya sayansi kama siku hiyo.
Wakati huo, tayari janga la COVID19 na upotoshwaji ulikuwa juu ...#UZI (SEHEMU YA KWANZA)
#DaktariMwandishi
kitu ambacho sikutegemea, ni upotoshwaji mkubwa zaidi uliokuja na chanjo.
Lakini, siwalaumu wenye maswali dhidi ya chanjo. Yapo maswali muhimu mno ambayo, hatuwezi kuyasukumia uvunguni kwa kigezo cha upotoshaji.
Ni lazima yajibiwe hata kidogo.
Nitajitahidi kutoa majibu machache.
Kabla sijajibu, naomba niseme kuwa ni sawa kuwa na maswali juu ya kile unachokipokea, lakini si sawa kusambaza taarifa za uongo na zisizo na ushahidi wowote.
Kufanya hivyo ni ugaidi. Ni uhalifu dhidi ya binadamu.
Kwanza niseme, mimi NAAMINI KATIKA CHANJO.
NAAMINI KATIKA SAYANSI.
Read 24 tweets
BARUA KWA BINTI WA 🇹🇿 #UZI
#PARTONE
Binti,
Salaam zikufikie pale ulipo kama upepo uvumavyo kutoka baharini kwenda nchi kavu. Natumaini hujambo. Mimi sijambo.
Kila siku nakuwaza sana. Nafikiria nifanyeje kugusa maisha yako.
Kabla ya yote nijitambulishe, mimi ni #DaktariMwandishi Image
Dhumuni la barua hii, ni kusema na wewe Binti. Natamani barua hii ningeiremba kwa maua, lakini naamini maneno nitakayoandika ni mbegu tosha.
Jana ilikuwa siku ya wapendanao, haijalishi ulipokea salamu au la, naomba pokea zangu; NAKUPENDA.
Enzi hizo nikiwa sekondari, ilikuwa siku
nzuri sana. Wale ma-admire/dada wa shule/vindende tuliandikiana kadi na kupeana zawadi. Ilipoangukia wikiendi kama hii, mambo yalikuwa moto zaidi, tulipokea kadi na barua kutoka kwa marafiki mbalimbali. Tukisubiria jumatatu tuibie kuingia facebook kuchungulia salam tulizotumiwa.
Read 16 tweets
#UZI : NEW ARRIVALS 🔥
Vile #ViwaloVyaKudu vimerudi tena! 😍🔥
-Ukipenda, screenshot tuma DM ulipie kama ipo.
-Nguo isiyolipiwa, haitotunzwa.
-Bei ni 17000Tshs, haipungui.
-Delivery J'PILI TU, Mikoani tunatuma, Unaweza kuja kuchukua KAIRUKI siku yoyote.
KARIBU💙
#DaktariMwandishi ImageImageImageImage
Karibuni 💙🔥
Wale wa PAJAMA PARTY, SLEEP OVER, SLUMBER PARTY, 😋😋😋 ImageImageImageImage
Karibuni 🔥💙
Wale mabibi harusi watarajiwa kwenye Bridal Photoshoot, Birthday photoshoot n.k 🔥🔥🔥 ImageImageImageImage
Read 10 tweets
Akasimama Mama Victor, kila mtu alikuwa akisubiria maneno yake. Ni mama wa makamo, alipendeza sana. Akasema yeye ana funzo dogo, AINA TANO ZA MANENO.
Nimeona nisiwe mchoyo, niwashirikishe niliyojifunza jana kwenye #SisterhoodTeaParty by DinaMarious #UZI (MFUPI)
#DaktariMwandishi Image
1. Maneno matamu-
Yapo ya aina mbili
a)maneno ya faraja (maneno ya kutia moyo, maneno ya kuinua nafsi ya mtu)
b)maneno ya mapenzi (yamejaa huba, yanakufanya utekenyeke kabla hata hujaguswa, haya ni maneno ya kumpa umpendaye, maneno ya kutia hamasa)
#SisterhoodTeaParty
2. Maneno ya Raia- hautakuwa na maadui wala marafiki, unakuwa ni mtu wa salamu na watu lakini hujengi mahusiano zaidi. Unakuwa na mipaka, unajenga ukuta kukuzunguka hivyo unakuwa huna adui wala rafiki, huna mwandani, huna mtu wa kukuegemea wala wa kumuegemea.
#SisterhoodTeaParty
Read 12 tweets
Nimeketi kitandani, nikatazama picha hii, nikatabasamu.
Hakika ni sanaa iliyofana.
Kwanini picha hii? tena ambayo bado haijakamilika?
Hayumkini ni kwasababu imeakisi utu wangu, ya kwamba mimi si mkamilifu.
Natazama nilipotoka. Nashusha pumzi. Natabasamu. #UZI
#DaktariMwandishi Image
Kwa sababu fulani, machozi yananilenga.
Nafumba macho. Taa zimezimwa. Chumba kipo kimya. Wenzangu wawili wametoka, mmoja amelala, siku yake haikuwa njema.
Sauti ya pekee ni ya feni inayozunguka kutupunguzia joto la jiji hili.
Navuta hisia. Mawazo yanarudi nyuma. Kumbukumbu
za tangu nikiwa mdogo. Nikiwa nisiyejua ya dunia. Nakumbuka kisiwani Mafia, rafiki yangu mzungu Samantha, na mdogo wake, Christopher. Najiuliza, wako wapi? Nawakumbuka Dorothea, Geo, Mselo, Mlekwa na Waziri. Namkumbuka Mama Mchungaji, alikuwa mwalimu mkuu wangu chekechea, alikuwa
Read 24 tweets
MAISHA NI SAFARI, JARIBU. MAISHA NI MAPIGANO, PIGANA.
Ni maisha ya Mtoto Mercy Maeda: mtoto pekee ambaye kwa sasa alitakiwa awe anaendelea na masomo ya Kidato Cha Pili, St. Mary’s Mazinde Juu, ila sasa anapigana na saratani ya DAMU (LEUKEMIA)
#UPENDOUSIOPIMIKA
#DaktariMwandishi Image
Mama yake Natu Rashid Maeda aliugua saratani ya titi kwa miaka 10 akapata matibabu kwa miaka 10 haikuwa rahisi kwa familia kiuchumi.
Familia ikiwa inamshukuru Mungu yakuwa mama amehakikishiwa kupona kabisa ndani ya miezi 4 Mtoto Mercy anagundulika kuwa na saratani ya damu na sasa ImageImage
inahitajika takribani dola za kimarekani 137,000 (milioni 300 TZS) kwa ajili ya huduma ya kupandikiza uboho (bone marrow transplant).
Hii familia imeshauza na kukopa kufikia hata kupoteza ajira ya mzazi mmojawapo kuweza kuendelea na matibabu ya awali walipofikia hawana tena uwezo
Read 5 tweets
Ni wakati mwingine wa kugusa maisha ya mwenzetu. Wakati wa UPENDO USIOPIMIKA.
Getrude Ofunguo aliyepo KCMC akisumbuliwa na Bone Marrow Failure, (Aplastic Anemia).
Bone marrow hutengeneza seli za damu, seli hai nyeupe, nyekundu na chembe sahani. Hivyo Bone marrow
#DaktariMwandishi Image
inapofeli, mtu anapungukiwa na seli nyekundu za damu(zinazosafirisha oksijeni mwilini), seli nyeupe za damu(zinazolinda mwili dhidi ya mashambulizi ya vimelea visababishavyo magonjwa) na chembe-sahani(zinazosaidia damu kuganda pale unapoumia).
Mtu anapokuwa na upungufu wa vyote,
anakuwa katika hatari kubwa ya magonjwa nyemelezi, kutokwa na damu nyingi na kuwa na upungufu wa damu.
Mwenzetu Getrude, amefanikiwa kupata Millioni 16 kati ya Millioni 200 zinazohitajika kwa ajili ya matibabu yake.
Kama watanzania 184,000 (Laki moja na themanini na nne elfu) TU
Read 4 tweets
Mara ya kwanza nilimuona kwenye muvi ambapo kichwa chake kilikuwa dili.
Ni mwanamke mrembo, ingawa filamu nyingi humuonyesha tofauti na historia isemavyo.
Nywele zake ni nyoka na ukikutanisha macho yake na yako unageuka jiwe. Anaitwa MEDUSA! #UZI FUATILIA
#DaktariMwandishi Image
Historia yake inatoka kwenye hadithi za kigiriki, jina lake MEDUSA likimaanisha "mlinzi". Alikuwa binti mrembo, bikra na mtumishi wa mungu wa bikra, Athena. Alimtumikia kwenye helalu lake hadi mungu wa bahari, Poseidon alipombaka Medusa. Akapata mimba ya mapacha lkn hakuzaa. Image
Yule mungu Athena, akamlaani Medusa, akabadili nywle zake nzuri kuwa nyoka na kila kiumbe, binadamu, mnyama au miungu iliyokutanisha naye macho aligeuka jiwe.
Medusa akakimbia kwa hofu baada ya kushindwa kuishi na watu na miungu. Akaenda kuishi mapangoni. Akajificha. Image
Read 18 tweets
#UZI TEKNOLOJIA NA AFYA YA AKILI (kwa hisani ya @simonsinek)

"Tunakua kwenye dunia ya Facebook na Instagram. Kwa maneno mengine, tupo viziri kwenye kuweka FILTERS kwenye vitu. Tupo vizuri kuonyesha watu kuwa maisha yetu ni mazuri, ilhali kiuhalisia tuna sonona"
#DaktariMwandishi
"Mtandaoni kila mtu yupo TOUGH, kila mtu anaonekana ameyapatia maisha. Ila kiukweli, ni wachache sana wapo TOUGH na wengi bado hawajayapatia maisha. Kwahiyo tuna kizazi kinachokosa kujiamini kuliko vizazi vilivyopita.

Tunajua unapotumia simu na mitandao ya kijamii, ubongo wetu"
"hutoa kemikali ya DOPAMINE, ndio maana unapopokea text, unajisikia vizuri.
Au unapojisikia mpweke, unatuma text kwa marafiki kama 10 kuwasalimu, kwasababu unajisikia vizuri unapopata jibu.
Ndio maana tunahesabu LIKES, FOLLOWERS, RTs na unarudi kutazama post yako ina likes ngapi"
Read 26 tweets
Natazama nyuma, mawazo yangu yanagota mwaka 2010, nikiwa mwanafunzi wa kidato cha pili.
Ni mchana baada ya chakula, hakuna mwalimu darasani, natoka naketi pembezoni mwa darasa na daftari langu la Kemia kujisomea.
Hatua kadhaa mbele yangu ni ukuta wa shule. #UZI
#DaktariMwandishi Image
Nje ya ukuta huo kuna mti wa mwembe unaochungulia ndani ya ukuta ma kamlima kidogo, ni barabara wanayopita wanafunzi wa shule za kata za jirani, Kwembe na Luguruni.
Nikiwa nimezama katika notes zangu, naisikia sauti ikiita, "Angel, Angel"
Nainua macho yangu kuona wanafunzi watatu
wa Kwembe wa kiume wamesimama kwenye kale kamlima.
"Mimi sio Angel, nikawaitie?", nawajibu.
"Ndio, katuitie Angel form 2", akajibu mmoja wao.
Nilijua wazi hatukuwa na mwanafunzi aitwaye "Angel", tulikuwa na Angela.
Nikainuka kwenda darasani, nikamchukua Melissa, nikampanga.
Read 23 tweets
"Mzalendo, nani amekupa ruhusa ya kukalia majani ya jeshi?", ilikuwa ni sauti ya amri kutoka mgongoni kwangu.
Nilitazama nyuma na kukutana na kijana mrefu, maji ya kunde, mkakamavu, sura ya kazi kwelikweli.
Nikainuka, nikamtazama nisijue la kusema. FUATILIA #UZI
#DaktariMwandishi Image
Ilikuwa ndio dakika chache baada ya kuwasili Maramba JKT 838KJ, nikiwa nasubiria kukabidhi simu na ufanyiwa usajili.
Nikamsikia Afande akimuita yule aliyenisemesha, "Mbise, yatupie taulo baba."
Na huyo ndiye Afande wa kwanza kumfahamu, Afande Mbise.
Yeye ndiye aliyepewa jukumu la
kutusimamia sisi wazalendo.
Ilikuwa jioni, baada ya kukabidhiwa sehemu ya kulala na kula chakula cha usiku, Matron alitupeleka moja kwa moja hadi "uwanja wa damu", mbele alisimama yule kijana, Afande Mbise akiimbisha 'chenja'(nyimbo) mbalimbali za jeshi.
Moyoni nilikuwa na hofu
Read 13 tweets
UPENDO USIOPIMIKA #UZI
Ni mwaka 2014 mwishoni, tulikuwa kidato cha 6 Mazinde Juu, binti aliyekuwa analala kitanda cha juu yangu, Happy alipokea taarifa za msiba wa baba yake mzazi. Zilikuwa taarifa za kusikitisha zilizobadili maisha yake daima. FUATILIA.
#DaktariMwandishi 👣
Happy, binti mwenye akili, aliyetoka katika familia isiyojiweza lakini alifanya vyema katika matokeo yake ya kidato cha 4 katika shule jirani ya serikali, hivyo meneja wa shule, Padri Damian Milliken alijitolea kumsomesha Mazinde Juu na kumhudumia hadi atakapomaliza kidato cha 6
Baada ya kupokea msiba ule, nilijadiliana na wenzangu wa chumbani na wanadarasa wenzetu tukamuomba mkuu wa shule Sister Evetha Kilamba atupe ruhusa kuhudhuria mazishi ili mwenzetu asijione mpweke kwani aliishi karibu na shule. Sr. Evetha alikubali na tukachanga rambirambi kisha
Read 33 tweets
HERD IMMUNITY (KINGA JAMII/KINGA KUNDI) kutumika kupambana na COVID19 ni mjadala unoaendelea duniani, katika kipindi hiki ambacho dunia inazunguka kwenye mhimili wa janga la #COVID19, hasa katika nchi zinazoendelea ambapo "lockdown" imeonekana kushindikana. #UZI
#DaktariMwandishi
🔅Kinga jamii (Herd immunity) inatokeaje?
Asilimia kubwa ya watu katika jamii wanapokuwa na kinga dhidi ya ugonjwa fulani, wanawalinda wale wachache wasio na kinga hivyo ugonjwa unapotea.
Kwa kielelezo cha picha hapo chini, wenye mwamvuli ana kinga, asiye nao hana kinga. Hivyo
wakisimama pamoja na kuunganisha miamvuli yao, wale wasio na miamvuli hawalowi (hawapati maambukizi).

🔅Unapataje kinga jamii?
Kwa kutegemea chanjo au kinga mwili ya asili.
Magonjwa mengi yamepotea au yamekuwa adimu kwa kupitia njia hii. Lakini kwa CHANJO, sio kwa kutegemea
Read 26 tweets
#Covid_19: HOFU Vs TAHADHARI. #UZI

Kuna mstari mwembamba kati ya kutia hofu na kuhabarisha, kutia moyo na kutoa tumaini la uongo.
Nayakumbuka maneno ya mwalimu wangu, "Usimwambie mtu atapona kama unajua hatapona wala hatapona kama kuna uwezekano akapona"
Mtanzania, Vuta Pumzi.😷
Siku chache zilizopita, niliandika #Uzi mrefu kuelezea kuhusu #coronavirus, naamini umewasaidia.
Juzi, Mh. waziri alipotangaza tuna mgonjwa, mlango wa waandishi wa habari na wasemaji wa sekta ya Afya ukafunguka. Kila mtu na lake. Nimejitahidi sana kurekebisha taarifa potofu. KAZI
HALI IPOJE DUNIANI? Kwa mujibu wa @WHO hadi tarehe 16/03/2020, kulikuwa na maambukizi jumla 167,511 na vifo 6,606 tangu mlipuko ulipoanza.
Huku @WHOAFRO wakiripoti kuwa hadi sasa idadi ya watu walioambukizwa barani Afrika imefikia 418.
Idadi ya waliopona inakadiriwa kuwa 80,000
Read 22 tweets
MATUKIO YA WANAUME KUJIUA: Tutafunika kombe mwanaharamu apite hadi lini? #Thread

Wiki chache zilizopita, vyombo vya habari vilipambwa na habari kuhusu wanaume kuongoza kwa matukio ya kujiua.
Jambo hili bado halijapewa uzito sahihi.
Ungana nami💭
#AfyaYaAkili
#DaktariMwandishi 👣
Wanaume wapo kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa ya akili kutokana na msongo wa mawazo.
Vihatarishi huanzia kwenye uchumi, ulevi, aina ya kazi wanazofanya na majukumu yanayowakumba.
Mfumo wa maisha unamshinikiza mwanaume kubeba majukumu mengi na wakati huo huo kumlazimisha
asionyeshe hisia waziwazi kama ishara ya "uanaume".
Hivyo basi, wanatembea na mizigo mikubwa ambayo baada ya muda akili zao hushindwa kuhimili na kukata tamaa.
Kuanzia mtoto wa kiume akiwa mdogo anapoumia anaambiwa, "wanaume hawalii" hivyo anakua akiamini kuwa mwanaume kuonyesha
Read 19 tweets

Related hashtags

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!