Discover and read the best of Twitter Threads about #DondooZaDaktari

Most recents (4)

#DondooZaDaktari | Leo ni siku ya ugonjwa wa KISUKARI duniani #WorldDiabetesDay

➡️Siku maalumu ambayo wanajamii tunaelimishana kuhusu tatizo hili la kiafya.

➡️Tatizo hili linaongezeka na moja ya kisababishi kikuu cha magonjwa ya figo,moyo, upofu na ulemavu wa kupoteza viungo.
#KISUKARI NI NINI?

➡️Kisukari ni ugonjwa wa kudumu ambao hutokea pale kiwango cha sukari (glukosi) katika damu
kipo juu zaidi kutokana na kukosekana au mwili kushindwa kutumia homoni ya insulini

➡️Kiwango cha glukosi kikiwa juu kwa muda mrefu, husababisha madhara katika mwili
➡️Unapokula chakula, mfumo wako wa kumeng’enya hukichakata na kutengeneza glukosi.

➡️Glukosi inapoingia kwenye damu, husababisha kongosho lako kutoa homoni inayoitwa insulini.

➡️Insulini huzunguka mwilini na kuwezesha seli kupata glukosi ili kuitumia kuleta nguvu mwilini.
Read 17 tweets
#DondooZaDaktari | Leo ni siku ya #KIHARUSI #WorldStrokeDay

➡️Tatizo la dharura la kiafya ambalo ni moja ya magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo.

➡️Mitindo ya maisha na Lishe ni vitu vinavyochangia wagonjwa wanaopata stroke kuongezeka

➡️Kiharusi huacha ulemavu au kifo
➡️KIHARUSI hutokea pale seli za ubongo 🧠 zinapokufa kutokana kuziba au kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo hivyo kukosa hewa ya oksijeni na virutubisho.

➡️Kiharusi kikihusisha mshipa wa mkubwa wa damu kwa wastani mgonjwa hupoteza seli za ubongo (neuroni 1.9) kila dakika.
KUNA AINA KUU MBILI ZA KIHARUSIBrain

1️⃣Kiharusi kinachotokana na kuziba kwa mishipa ya damu ya damu ya ubongo

2️⃣Kiharusi kinachotokana na kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo

🗒️80% ya watu wanaopata kiharusi hutokana na kuziba kwa mishipa ya damu kwenye ubongo.
Read 12 tweets
#DondooZaDaktari | #USUGU WA #DAWA

➡️ #Antibiotiki ni dawa zinazotumika kutibu maambukizi ya bakteria.

➡️Usugu wa antibiotiki hutokea pale bakteria wanapotengeneza usugu dhidi ya aina flani ya dawa.

➡️USUGU hufanya dawa kushindwa kufanya kazi

#AntimicrobialResistance
Matumizi holela ya dawa aina ya antibiotiki huchangia usugu wa dawa kutokea.

Bakteria wanapopata usugu husababisha
➡️Kutokupona ugonjwa hata baada ya kutumia antibiotiki ambazo zimekuwa zikitibu ugonjwa huo
➡️Kuongezeka kwa gharama za matibabu
➡️Kifo
Unatengeneza tatizo usugu wa dawa iwapo
➡️Humalizi dawa ulizoandikiwa na daktari
➡️Unatumia dawa zisizo na ubora/feki
➡️tumia dawa zilizoisha muda wake wa matumizi
➡️Unakula nyama, maziwa, mayai au damu yenye masalia ya antibiotiki kutoka kwa mifugo iliyotibiwa
Read 4 tweets
#DondooZaDaktari | Ugonjwa wa kisukari unaongezeka kwa kasi hata katika nchi zetu maskini.

✍️Kisukari hutokana na mwili kushindwa kutumia glukosi (sukari)

➡️Kisukari ndio sababu kuu ya:
- Kiharusi
- Upofu
- Ugonjwa wa kudumu wa figo
- Shambulio la moyo
- Watu kukatwa miguu Image
➡️Kwa mwaka 2019, takribani vifo millioni 1.5 Duniani vilichangiwa moja kwa moja na tatizo hili la kisukari.

➡️ Kuanzia mwaka 2000 hadi 2016, kuna ongezeko la 5% la vifo katika umri mdogo (premature death) kutokana na kisukari. Image
➡️ Mlo sahihi
➡️ Mazoezi ya Mwili
➡️ Kudhibiti Uzito
➡️ Kuepuka sigara na pombe

Ni baadhi ya mitindo ya maisha inayoweza kusaidia kuzuia kisukari au kupunguza athari ya kisukari aina ya pili.
Read 4 tweets

Related hashtags

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!