Discover and read the best of Twitter Threads about #FahamuNaFesto

Most recents (3)

#FahamuNaFesto: Herd immunity (population immunity, herd effect, community immunity or social immunity ) au kwa tafsiri ya kiswahili kinga ya jamii, kinga ya kundi.
Nianze kwa mfano: Nyumbani mnaishi watu 10, ikatokea umeingia ugonjwa unaoweza kuambukiza. ukawapata watu sita kati yenu, lakini hawa watu sita walioambukizwa miili yao ikatengeneza kinga dhidi ya ugonjwa huo. (Mwili wenyewe ukaweza kutengeneza kinga dhidi ya ugonjwa)
Kutengeneza kinga ina maana mwili umeweza kupambana na ugonjwa hivyo kuzuia mtu huyo kupata athari zinazotokana na ugonjwa huo lakini pia mtu huyu hataweza tena kuambukiza watu wengine. Hivyo nyie wengine wanne mliobaki hamtapata ugonjwa.
Read 13 tweets
#FahamuNaFesto: Je unalifahamu kundi lako la damu (blood group)? Ni moja ya maswali mengi sana ambayo wengi wetu tunajiuliza. Wengi tunaenda mbele zaidi kutaka kujua Je kwa kundi ulilonalo unaweza kumpa damu mwenye kundi gani. Basi leo nakujibu maswali yote haya.
Katika sayansi ya makundi ya damu kwanza tutaanza na mifumo ya ugunduzi wa makundi ya damu. Mpaka julai mwaka jana tafiti zinaonesha kuna takribani mifumo 39 ya damu. Nikukumbushe tu kuna mfumo wa ugunduzi wa kundi la damu na kuna kundi la damu hivi ni vitu viwili tofauti.
Mfumo wa ugunduzi wa makundi ya damu ni njia tofauti ambazo wanasayansi walibaini zinaweza kutumika kugundua kundi la damu mfano kuna MNS,Rh, KELL, LEWIS na ABO. ABO ndio mfumo unaotumika sana. Ndio mfumo unaotupatia makundi ya damu kama vile A, B, AB na O.
Read 20 tweets
#FahamuNaFesto | Mohammed Iqbal Dar.
Mshindi na mbunifu wa jina "Tanzania" katika mashindano yaliyotangazwa mwaka 1964 akiwa kijana wa miaka 18 tu akisoma shule ya sokondari Mzumbe mkoani Morogoro.
Baada ya muungano mwaka 1964 serikali ilikusudia kutangaza mashindano ya ubunifu wa kutafuta jina litakalotumika baada ya muungano.

Mohammed alisema nanukuu "Wakati huo nilikua maktaba nikisoma gazeti la Standards (sasa Daily News) nikaona tangazo la shindano hilo...
...Nikiwa na karamu na karatasi nilimuomba Mungu kisha nikafanya majaribio pasipo kushirikisha familia yangu" mwisho wa kunukuu.

Ilimchukua dakika 5 tu kupata jina "TanZan" ikiwa ni muunganiko wa "Tan" (Tanganyika) na "Zan" (Zanzibar).
Read 7 tweets

Related hashtags

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!