Discover and read the best of Twitter Threads about #bongelaafya

Most recents (6)

UZI: Jana tumesikia Tanzania imejiunga kwenye mpango wa COVAX.

COVAX = Covid Vaccine (chanjo ya corona)

Je COVAX ni nini? 👇
#BongeLaAfya @BongeLaAfya
COVAX ni mpango wa mapatano (partnership) kati ya shirika la afya la dunia (WHO) na mashirika mawili ya kimataifa – Gavi vaccine alliance na Coalition for Epidemic Preparedness Innovation (CEPI), mapatano haya yanalenga kusambaza chanjo kwenye mataifa yanayoendelea.
COVAX inakusudia kutoa dozi za chanjo bilioni mbili kwa watu katika mataifa 190 kwa mwaka huu, hii ni kuhakikisha angalau asilimia 20 ya watu imepata chanjo (vaccinated). Zaidi pia, inalenga kusambaza chanjo kwa mataifa 92 yenye kipato cha chini bure kabisa.
Read 10 tweets
UZI: Red eye au bloodshot kwa kitaalamu, hutokea pale ambapo mishipa midogo ya damu inayoonekana kwenye uso wa jicho kupanuka au kujawa na damu. Hali hii hutokea kutokana na uwepo wa kiwango kidogo cha oxygen inayotolewa na tishu zinazofunika jicho au maambukizi. #BongeLaAfya Image
Hali hii huwa ya kawaida na inaweza kutokea katika jicho moja au macho yote mawili. Hiyo rangi nyekundu inayoonekana ni rangi ya damu katika mishipa yake hapo kwenye jicho, inaweza kuwa sababu ya kupikicha jicho au maambukizi fulani. Image
Red eye kwa ujumla isikupe wasiwasi saana, lakini hali hii ikiambatana na maumivu ya macho, au kupungua kwa uwezo wako wa kuona nakushauri umuona daktari kwani inaweza kuwa dalili ya magonjwa kama pinkeye (conjuctivitis au kwa kiswahili Kiwambo), Corneal ulcer, Dry eye syndrome. Image
Read 8 tweets
UZI: Zifahamu njia za kuzuia mimba: Wote tunahitaji taarifa sahihi na zinazoeleweka kuhusu matumizi au njia mbalimbali za kuzuia mimba. Jambo la kuzuia mimba sio la mwanamke pekee bali hata mwanaume ana wajibu wa kujifunza mambo yanayotokea wakati wa tendo la ndoa. #BongeLaAfya Image
Mwanamke yeyote ambaye ameanza kupata hedhi ya kila mwezi anaweza kutumia njia za kudhibiti mimba. Njia hizi hutofautiana kutokana na upendeleo wa mtu binafsi au umri pia. Leo nitakusaidia kuwa na uwezo wa kuzuia mimba kwa kukupa taarifa sahihi. Image
1. Kondomu - Kuna kondomu za kike na kiume ambazo hufanya kazi kwa ufanisi kabisa zinapotumika. Kondomu zinapatikana sehemu nyingi na nina hakika wengi tunazifahamu. Kikubwa kondomu ya kike haitumiki wakati mmoja mnapotumia kondom ya kiume. Chagueni mmoja avae. ImageImageImageImage
Read 14 tweets
UZI: Dalili za mimba: Ujauzito ni ndoto ya wengi, huku kwa wengine ni jambo wanaloepuka na kuzingatia sana. Wadada wengi wanaonesha kuhitaji watoto tofauti na wanaume. Leo nimekuletea dalili 10 za ujauzito ambazo huashilia uwepo wa ujauzito #BongeLaAfya Image
1. Kutoona siku zako: Kukosa siku zako ni moja ya dalili za kwanza kabisa ambazo wengi wetu wamezoea. Katika kipindi cha mzunguko kuta ya mfuko wa uzazi huvunjika na kujiengua na kutoka nje katika mfumo wa damu, hudumu kwa siku tatu mpaka saba. Unapopata ujauzito hujishkiza hapo. Image
2. Misuli ya miguu kubana/cramps: Katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito mwanamke anaweza kuona dalili za miguu kukaza au kubana, Hii inatokana na mabadiliko ya mwili katika kuchakata calcium ambayo huitajika kwa wingi kuunda mifupa ya mtoto, meno na viungo. Image
Read 13 tweets
UZI: Kwa nini mnapaswa kuaminiana mnapoenda kupima UKIMWI: Miaka mitatu sasa nikifanya kazi hospitali na taasisi za tafiti kuna mambo nimekuwa nikikumbana nayo ambayo leo acha niyaweke mbele yenu ili wote tupate kujifunza. Nitaongelea tukio la upimaji wa UKIMWI. #BongeLaAfya Image
Kwa hii kadhaa nikiwa nafanya kazi za upimaji maabara, Upande wa upimaji UKIMWI kuna changamoto nyingi sana ambazo zinawakumba watu wanaokuja/wanaoleta rafiki/wapenzi wao kupima virusi vya ukimwi. Changamoto hizi nyingi zinatokana na kukosa uaminifu lakini pia udanganyifu. Image
Siku moja walikuja kupima UKIMWI mwanaume na mwanamke ambao kwa kuwaangalia tu unajua ni wapenzi. Baada ya ushauri na kuchukua sampuli ilibidi waende nje wakasubiri majibu. Sasa wakati naendelea kupima ghafla alirudi yule mwanamke na kutaka kuongea na mimi. Image
Read 8 tweets
UZI: Nadhani umekutana na picha za hii couple zikizunguka mitandaoni, picha hizi zinawaonesha wapenzi wakiwa na tofauti ya kimuonekano.

Hali aliyonayo huyu mwanaume kitaalamu inaitwa "PROGERIA", Ni moja ya hali zinazotokea kwa nadra sana ambapo mtu huonekana mzee. #BongeLaAfya ImageImage
Hali hii huanza kuonekana kwa mtoto miaka miwili baada ya kuzaliwa, Matatizo ya moyo na kiharusi (stroke) huwa sababu kubwa ya kupoteza maisha kwa watu wenye hali hii. Tafiti zinaonesha hali hii humpata mtoto 1 kati ya milioni 4 dunia nzima. Image
Ugonjwa huu hutokana na hitilafu katika jini ambayo hupelekea kutengenezwa kwa aina ya protini (progerin), Progerin ni abnormal mwilini, seli zikitumia protini hii hufa kwa urahisi na hivyo mtu kuzeeka haraka. Mtu harithi ugonjwa (not inherited). Image
Read 7 tweets

Related hashtags

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!