Discover and read the best of Twitter Threads about #elimikawikiendi

Most recents (24)

Habari ndugu , karibu jamvini tuelezane kidogo juu ya uelewa wa jamii juu ya HEDHI na HEDHI SALAMA. Utakuwa nami Salome Mosha @Sally_mosha .
#ElimikaWikiendi

Karibu thread 👇..
HEDHI NI NINI?
Hedhi ni muunganiko wa yai ambalo halikurutubishwa pamoja na damu inayotokana na kumomonyoka kwa tishu laini za ukuta wa mfuko wa mimba (uterus). Kitendo hiki hutokea kila mwezi kwa mwanamke huitwa mzunguko wa hedhi (Menstruation period).
#Elimikawikiendi
MZUNGUKO WA HEDHI NI NINI?
kipindi ambacho wanawake hutokwa na damu ukeni. Wanawake wengi hupata hedhi kila baada ya siku 28. Kwa baadhi ya wanawake huchelewa hadi 30. Wasichana wengi huanza hedhi katika umri wa miaka 12 wengine huanza katika umri mdogo au mkubwa
#Elimikawikiendi
Read 14 tweets
Mitandao ina fursa nyingi sana, na moja ya fursa kwa vijana leo hii ni #blogging.

Kutengeneza $100 hadi $1,000 kwa mwezi kwenye blogu ni kitu kina wezekana kabisa.

Basi ungana nami katika #ElimikaWikiendi nikufundishe jinsi gani unaeza tengeneza pesa kwenye blogu.
Kwanza kabisa tuanze kwa kufahamu blogu ni kitu gani?

Blogu ni aina ya Mtandao unaokuwezesha kuandika makala, kuweka picha, videos na kadhalika katika mlolongo maalumu.

Blogu ni teknolojia inayowezesha watu kuchapa maoni na fikra zao katika mtandao.

#ElimikaWikiendi
Na blogu zipo za aina nyingi tu na zina endeshwa kwa kutumia majukwaa tofauti tofauti.

Endapo unataka kunza blog leo hii basi hii hapa ni makala inayo elekeza hatua kwa hatua nama ya kuanza blogu yako ndani ya dk 15 tu.

kidigitali.com/2021/09/Blogge…

#ElimikaWikiendi
Read 23 tweets
🦅KINACHOTOKEA WAKATI WA KU BOFYA NA KUSAMBAZA LINK ILI KUPATA ZAWADI📚

Kuna links nyingi sana ambazo hua watu wanaambiwa ku share na watu labda 10 au kwenye baadhi ya ma group ya WhatsApp ili kujishindia zawadi au kupata udhamini wa kusoma nje ya nchi

#Elimikawikiendi
Links hua zipo nyingi sana kuna zingine ni kujishindia simu flani mpya iliyotoka wakati huo,gari ya thamani,kwenda kutizama mechi ulaya live,au kampeni zingine ni kuataka kutabiri namna mtoto wako atakavyokua ama zingine kutabiri utakua tajiri kiasi gani moja kati ya kitu ambacho
Hua kinafanyika nyuma ya pazia ni kutekwa nyala(enslavement )kwa kifaa chako cha ki electronic kinachotumika kusambaza link hio inaweza kua ni pc,smartphone,ipads ama tablet na aina hii ya utekaji nyala wa mtandaoni tunaita Distributed denial of service attack(DDOS)
Read 11 tweets
🦅VITU VYA KUFANYA ILI KUOKOA MATUMIZI YA BANDO KWENYE SIMU!
📚📚📚

Kuisha haraka kwa internet Bundles imekuwa ni malalamiko ya wengi, lakini pia unaweza kufanya settings kadhaa kwenye simu yako kuokoa bundle kuisha haraka
Twende pamoja hapa chini 👇

#ElimikaWikiendi
Tuanze na simu za android then nitamalizia na iphone

ANDROID
1.Zima accounts syncing

Baadhi ya apps kama Facebook, Google Fit data, Google Play Movies, na Google Play Music ambazo mara nyingi wengi wetu hua hatuzitumii

#ElimikaWikiendi
na kila muda kama ziko on zinakua zinatumia data na
battery pia kufanya updates kati ya simu yako na server,namna ya kuzima nenda settings >accounts then Zima syncing ya apps ambazo muda mwingi hua huzitumii kama inavyoonekana hapo juu

#ElimikaWikiendi
Read 12 tweets
⚡Kuna Kipindi Nilidhani 150K ni Nying Sana Kumcharge Mteja Kwa Picha 10,

✅Hizi ni Siri 5 Ambazo Mentor Wako Hataki ujue 99%
.
#Uzi 👇🏽
⚡Ni Miaka 8 Imepita Sasa Tangia Nianze shika Kamera Kwa Mara Ya Kwanza,
.
Along the way nimejifunza Vitu Vingi Sana...
.
Ambavyo Leo Nataka nikumegee Kidogo, Ili ujue Siri ya Mtungi.
⚡Katika Miaka nane Kuna Miaka hapo kati Nilikata Tamaa Kabisa,
.
Nikatemana na Photography Mazima.
.
Lakini Moyo wangu Ulikuwa unaniuma Sana, nimefanya Kazi za Hapa na Pale.
.
Lakin Bado Moyo Ulikuwa Haujakubali kuachana na Photography.
Read 21 tweets
Leo katika #ElimikaWikiendi nakuletea "Mambo Muhimu ya Kuzingatia kwa Vijana wanao Ingia kwenye FURSA za Mtandaoni."

Vijana wengi sana wana tamani au wameingia katika kuzisaka fursa mbali mbali za mtandaoni.

Basi ungana nami tuchambue mambo muhimu ya kuzingatia.
1. Jinsi ya Kuchagua kitu gani ujikite nacho mtandaoni.

Hapa ndipo wengi sana waka anza kukosea. Mtandaoni kuna mambo mengi sana.

Huwezi kujihusisha na kila kitu, hivyo ni muhimu sana kuchagua ni kitu gani ufanye.

#ElimikaWikiendi
Kuna fursa nyingi sana.

Mfano;
- Freelancing
- Blogging
- Affiliate Marketing

Na vingine vingi tu.

Hapa ndipo wengi hushindwa kuchagua nini hasa afanye. Hauzuiliwi kufanya vitu vingi ila jikite na vichache kwanza.

#ElimikaWikiendi
Read 17 tweets
Wakati huu tunapo kwenda likizo za sikukuu za Christmas na mwaka mpya, huwa ni muda mzuri kukaa na familia zetu, ndugu, jamaa na marafiki kutafakari mwaka ulivyokuwa na kujiandaa na mwaka unaofuata.

#ElimikaWikiendi

STADI/SKILLS ZA MUHIMU KUJIFUNZA

UZI [THREAD] 👇
Pia ni kipindi ambacho watu wengi hupendelea kuwepo mitandaoni. Wakati unatumia mitandao ni vyema ukapata ujuzi mpya wa namna unaweza faidika na mitandao.

Tutakuelezea baadhi ya ujuzi wa mtandaoni unaoweza kuwa na faida kwako kwa namna moja ama nyingine.

#ElimikaWikiendi
ONLINE SHOPPING

huu ni ununuzi wa bidhaa na huduma mtandaoni bila ya wewe kuwepo katika duka au biashara husika kimwili.

Ni rahisi sana kujifunza namna ya kununua vitu mtandaoni kutoka sehemu yoyote ile Duniani na malipo hufanyika kwa njia ya mtandao.

#ElimikaWikiendi
Read 18 tweets
#FAHAMU: VYAKULA BORA KWA WATOTO WADOGO KULINGANA NA UMRI WAO.

Watoto wanahitaji vyakula maalumu tangu wakiwa wadogo kwa ajili ya kuboresha afya zao na kuimarisha kinga ya miili yao ili kuepusha udumavu na kumkinga dhidi ya magonjwa mbalimbali kama PNEUMONIA, kuharisha n.k
#UZI ImageImageImageImage
MIEZI SITA YA AWALI
Mtoto anahitajika kupata maziwa ya mama yake pekee bila kuhitajiwa kupewa kitu kingine kama maji/ juisi katika kipindi hiki. Isipokuwa anahitajika kupata chanjo ya matone au dawa. Mtoto anyonyeshwe usiku na mchana isiyopungua mara 10 kwa masaa 24. ImageImageImage
MIEZI 6-9
Mtoto anyonyeshwe kwa jinsi atakavyohitaji.Muanzishie uji au vyakula vya kupondwa(Viazi,ndizi, samaki,nyama) kwa kuanzia vijiko 2-3 vya mezani kila baada ya masaa 12.Akifiksha miezi 7 ongeza kiasi mpaka 2/3 ya kikombe cha 250mls kila baada ya masaa 8.
#ElimikaWikiendi ImageImageImageImage
Read 7 tweets
Karibuni kwenye #ElimikaWikiendi na leo nitakielezea kwa ufupi kitabu cha A knight in Africa, ambacho kimeandikwa na Sir Andy Chande akielezea historia ya maisha yake kutokea kuzaliwa mpaka uzee wake. Kitabu hiki kina chapters 13 na utangulizi wake, uliandikwa na Rais Mkapa. Image
Chapeter 1: BUKENE HOMETOWN AND CHILDHOOD.

Sir Andy Chande alizaliwa Mombasa Tarehe 7, May, 1928, ila wazazi wake walikua wakiishi Bukene, Tabora. Licha ya kuzaliwa tarehe 7-5-1928, cheti chake kinaonyesha kazaliwa tarehe 17-8-1929. Hivyo ana birthday 2, kama Malkia Elizabeth!
Baba yake Sir Chande, alitokea India Gujarat, na alipande meli mwaka 1919 kuja Tanzania kutafuta maisha. Akaenda mpaka Bukene ambapo ni kituo kikubwa cha treni kuanza biashara. Sir Chande alisoma elimu ya msingi huko Bukene, shule ya wahindi tupu. #ElimikaWikiendi
Read 31 tweets
Maduka ya rejareja yanayouza vitu vinavyonunulika kwa haraka,hua ni mengi sana mitaani tunamoishi na yamekaribiana yahitaji akili & mbinu zakufanya biashara katka mazingira ya namna hii. Image
yafuatayo ni mambo kadhaa uwezayo kufanya ukajiweka kweny nafasi nzuri yakuhakikisha unashindana vilivyo vyema na kua na mzunguko mzuri wa pesa...
Epuka kufanya kijiwe sehemu ya biashara yako kwa gharama yeyote ile, ushikaji na ushosti haupaswi kufumbiwa macho sehemu ya biashara na ukumbuke hili ukiwa muuzaji ni wa kike na mashosti hujaa kweny biashara yako kupiga stori basi tambua kabisa......
Read 18 tweets
Kubalehe ni hatua muhimu sana kupitia ili kuweza kupata mtoto. Wastani wa kubalehe na kuvunja ungo kwa wasichana ni miaka 9-12 kwa sasa, ingawa miaka ya zamani ilikuwa kuanzia miaka 12-14. Wavulana huanza kubalehe wakiwa na miaka 12-14. #ElimikaWikiendi Image
Mbegu za mwanaume zina kromosomu (nyuzi nyuzi katika kiini seli cha kila kiumbe ambazo hubeba viiniurithi yaani jeni) aina mbili X na Y. Mayai ya mwanamke yana kromosomu aina moja tu ya X. #ElimikaWikiendi Image
Kromosomu X ya mwanaume ikiungana na kromosomu X ya mwanamke hupatikana mtoto wa kike ila kromosomu Y ya mwanaume ikiungana na kromosomu X ya mwanamke hupatikana mtoto wa kiume. #ElimikaWikiendi Image
Read 21 tweets
#FAHAMU: ATHARI ZA UTOFAUTI WA KUNDI LA DAMU KATI YA MUME NA MKE.
Kuna baadhi ya wanawake wanapoteza mimba zao na wengine kupoteza watoto wao baada ya kujifungua sababu ikiwa ni utofauti wa kundi la damu kati ya mume na mke. Katika makundi ya damu kuna kitu kinaitwa RHESUS FACTOR ImageImageImageImage
Kulingana na rhesus factors kuna makundi yafuatayo ya damu A+, A-, B+, B-, AB+, AB-, O+, O-.

Katika makundi ya damu mara nyingi mtoto hufuata damu ya baba. Hivyo, ikiwa kundi la baba lina antigen ya rhesus factor (A+, B+, AB+, O+) na mama akiwa hana hiyo antigen(A-,A-,AB-,A-) Image
Mtoto katika ujauzito wa kwanza atakuwa kama kundi la baba (rhesus positive) na hivyo mwili wa mwanamke utatengeza kinga (antibodies) dhidi kundi la baba. Hivyo katika mimba zinazofanya kiumbe kitakuwa kinashambuliwa na kinga ya mama (Rhesus incompatibility)
#ElimikaWikiendi ImageImage
Read 8 tweets
ARTIFICIAL INTELLIGENCE (AI) [ AKILI BANDIA ]

Akili Bandia (AI) hii ni Teknolojia inayozipatia mashine uwezo wa akili ya kibinadamu ili kuweza kufikiria na kutenda matendo kama kibinadamu.

Je, hizi AI zikoje na zianatumika wapi?

THREAD [ UZI ] 👇

#ElimikaWikiendi
Watu wengi wakiona neno AI ( Artificial Intelligence) hufikiria moja kwa moja ni roboti. Ili iwe AI inahitaji Software(Program endeshi) na Hardware. Software ndio kama ubongo unahitaji kupachikwa data ambazo zitakuwa zinatoka command/maelekezo kwenye hardware.

#ElimikaWikiendi
AI ina jifunza (learning), Fikiri (reasoning) na mtazamo (perception). Ndivyo hivyo sehemu ya akili ya binadamu inafanya kazi. Kwa miaka ya sasa hii Teknolojia inakuwa kwa kasi sana.

Imefikia hatua wataalamu wanataka AI iwe na uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi kama mwanadamu,
Read 23 tweets
BITCOIN, BLOCKCHAIN AND CRYPTOCURRENCIES

Turudi nyuma mwaka 2008, Bwana mmoja aitwaye Santoshi Nakamoto mtaalamu wa Computer na Hesabu alitengeneza Program na kuiita jina la BITCOIN

Je, Bitcoins ni nini na zinafanyaje kazi ?

Twende na uzi 👇

#ElimikaWikiendi
Bitcoin ni toleo la pesa taslimu ya ki-mtandao ( peer-to-peer version of electronic cash ) ambayo unaweza kutuma moja kwa moja kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine pasipo kupitia taasisi za fedha kama benki, Mobile money etc, unahitaji kuwa na internet tu

#ElimikaWikiendi
Kitu muhimu kwenye Bitcoin huwezi kugushi/forge, miamala fake haiwezi kufanyika, siyo lazima uwe na kitambulisho cha Taifa ( National ID) wala Bank account, Bitcoin iko decentralized ( imegawanyika ), mwamala ukifanyika hauwezi kubadilishwa na ina ulinzi sana

#ElimikaWikiendi
Read 25 tweets
NAMNA YA KUTENGENEZA PESA MTANDAONI

Kutoka michezo ya Betting mpaka uuzaji wa nguo katika mitandao. Kuna namna nyingi sana za kutengeneza pesa mtandaoni, nyingine zina ahadi ya kukupa utajiri mkubwa ndani ya muda mfupi., lakini je, ni kweli zinafanya kazi? 👇

#ElimikaWikiendi
Jibu: Sio siku zote.
Je, Utatengeneza pesa ukifata njia hizo?
Jibu: Labda, maana ni kitu kimekaa kimtego sana. Inawezekana kabisa kwamba ile kazi yako inayokupa mshahara kila mwisho wa mwezi ikakupa pesa zaidi ya hizi njia za mitandaoni au kinyume chake

#ElimikaWikiendi
Ukweli ni kwamba kuna njia za kweli zinazofanya kazi na zinazowapa watu pesa kupitia mitandao. Kuna Freelancer(Wafanyakazi huru), wajasiriamali wadogo wadogo, waandishi, Walimu, Wahasibu, Wanasheria, N.K hutumia mitandao kupata kipato

#ElimikaWikiendi
Read 25 tweets
Mbinu (10) za kukabiliana na ugumu wa maisha:

1. Epuka kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao

2. Punguza matumizi ya umeme au maji

3. Punguza matumizi ya simu kwa kutokupiga simu zisizo na ulazima

4. Punguza starehe zinazogharimu

5. Nunua vyakula kwa bei ya jumla sokoni
6. Lipa bili na madeni uliyokopa kwa wakati

7. Wekeza pesa unazokusanya katika mradi wowote ili kujiongezea kipato

8. Acha kabisa matumizi ya vitu au vilevi vya gharama

9. Unapoona fursa yoyote itakayokupunguzia gharama itumie

10. Acha matumizi au manunuzi yasiyo ya lazima
MUHIMU: Funzo hapa ni kumakinika katika kubana matumizi na si kuwa bahili. Huo ni ushauri tu, unaweza kuuchukua au kuuacha.

>>KUMBUKA: “Ukijinyima kupita kiasi, huwezi kufurahia maisha.”

>>@ElimikaWikiendi | #ElimikaWikiendi.
Read 3 tweets
UZI:

RADAR NA MATUMIZI YAKE

RADAR
Radar ni kifupisho cha (Radio Detection and Ranging)
Ni mfumo ambao unatuma signal/ishara kwenye kitu (object) na kuchambuliwa kisha kurudisha majibu ya hicho kifaa kwa mfumo huo wa signal kupitia hewa 👇

#ElimikaWikiendi
Ili kugundua uwepo, mwelekeo, umbali, na kasi ya ndege, meli, na vitu vingine

Signal ni mawimbi (radio waves) ambayo hutumwa kwa kifaa kilicho kwenye coverage ya Radar/eneo Radar inapofika na kukichambua hicho kifaa na kurudisha majibu kwenye chanzo/muongozaji

#ElimikaWikiendi
Kwa hapa Tanzania radar zinatumika kwenye viwanja vya ndege, jeshini na kwenye Meli. Na radar zilizopo zimegawanyika katika makundi mawili: Primary na Secondary radar

Tunapozungumzia hizi primary radar tunamaanisha ni zile Radar ambazo

#ElimikaWikiendi
Read 18 tweets
Mambo kumi (10) muhimu ya kuwa nayo makini kabla ya kuingia kwenye ndoa:

1. Sherehe ya harusi ni ya siku moja, ndoa
ni ya maisha yote

2. Upole na ukimya si kiashiria cha tabia njema

3. Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa au kuolewa na mtu asiye sahihi
4. Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu

5. Kuoa au kuolewa na mchekeshaji hakutakufanya uwe na ndoa yenye furaha

6. Kuoana kabla ya kuwa marafiki ni kama anga
bila jua

7. Usiolewe au usioe pesa au mali, olewa au oa mtu
8. Uchumba uliovunjika ni bora zaidi kuliko ndoa
isiyo na amani na furaha

9. Asili ya mikono inayojali ni moyo unaojali

10. Ukiwa rafiki mwema, utawavutia marafiki
wema

MUHIMU: Mambo haya 10 sio sheria, ni ushauri kutoka kwa wazoefu.

>>@ElimikaWikiendi | #ElimikaWikiendi.
Read 3 tweets
UZI

SOCIAL ENGINEERING
[ utumiaji wa madhaifu ya Mwanadamu kufanya wizi]

◾️Social engineering huchukua faida ya kitu dhaifu kabisa katika ulinzi wa taarifa za kila aina ya taasisi ambacho ni MTU

Social engineering ni "PEOPLE HACKING" na inahusisha 👇

#ElimikaWikiendi Image
Madhaifu ambayo binadamu tunayajenga sisi kwa sisi na kuweza kuyatumia hayo madhaifu kupata taarifa ambazo hutumika kwa faida binafsi

◾️Social engineering ni moja ya wizi mgumu kufanyika, kwa Dunia ya sasa imekuwa ni vigumu sana mtu kumwamini mtu mgeni kwake

#ElimikaWikiendi Image
Kutokana na hali halisi ilivyo hata hivyo hii imekuwa hacking ngumu sana kuizuia kutokana na uaminifu tunaoujenga baina yetu

◾️Social engineering, typically yule malicious attacker/mwizi hujiweka kama mtu mwema sana ili kupata taarifa anazotaka

#ElimikaWikiendi Image
Read 25 tweets
Kikundi cha watalii kilitembelea mto wa kufugia mamba na walikuwa wakielea kwenye meli ndogo katikati ya mamba wenye njaa. Ikasikika sauti ya mmiliki wa eneo hilo ikisema: "Atakaye ruka kwenye maji na kuogelea kutoka nje atazawadiwa dola milioni 10".
Kila mtu kimya, ghafla mwanaume mmoja akajirusha majini. Alikimbizwa na mamba kwa bahati nzuri alitoka salama. Akatangazwa mshindi. Wakati anarudi hotelini na mkewe akamwambia mkewe "Aisee sijajirusha mwenyewe majini, kuna mtu alinisukuma nikapambana niokoe maisha yangu".
Mke wake akatabasamu na kusema "Ni mie ndio nilikusukuma". Wewe ungemfanyaje kama ni mkeo? Simulizi linatufundisha: "Nyuma ya kila mwanaume mwenye mafanikio kuna mwanamke anayemsukuma kufikia mafanikio". #ElimikaWikiendi
Read 3 tweets
Mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kufanya kazi na shirika la Anga za juu ‘NASA’

Fadji Maina amekuwa mwanasayansi wa kwanza kutoka nchini Niger kufanya kazi na Shirika la Anga za Juu,NASA.
#ElimikaWikiendi
#WajumbeTuinuane Image
Bi maina mwenye umri wa miaka 29 alipata shahada ya uzamifu(PHD) mwaka 2016 na alijiunga na shirika hilo maarufu la anga za juu nchini Marekani mwisho wa mwezi uliopita.

Ameiambia BBC atatumia kazi yake mpya kurudishia shukurani sio tu nchi yake bali pia kwa bara zima la Afrika.
"awaasa wanawake wenzangu wasikate tamaa kufikia ndoto zao kwa sababu hakuna mtu angelifikiria mwanamke kutoka Niger, au msichana mdogo kutoka Niger, anataweza kufika mahali kama hapa. Siri ni kujiamini na kutafuta mazingira ambayo itakusaidia kufikia ndoto yako”
Read 3 tweets
HISTORIA YA SIKU YA LEO MIAKA 19 ILIYOPITA USA NA DUNIA KWA UJUMLA...
Siku kama ya leo 2001 Dunia ilitawala huzuni na simanzi kubwa kutokana na Shambulio la September 11 2001 Shuka nao... 👇👇
Retweet ifike mbalii
#ElimikaWikiendi
#WajumbeTuinuane ImageImageImage
Siku ya Jumanne, tare 11 mwezi September mwaka 2001 majira ya saa 2 na dakika 46 asubuhi mpaka saa 4 na dakika 28 asubuhi lilifanyika shambulio kubwa na baya zaidi kuwahi kutokea na kufanywa na adui katika ardhi ya nchi ya Marekani.
Majira ya saa 2 na dakika 46, ndege aina ya Boeing 767-223ER (A.A. Flight 11) iliyosajiliwa kwa namba N334AA, mali ya shirika la American Airlines ambayo iliruka kutoka Boston katika uwanja wa ndege wa Logan International Airport ikitegemewa kutua katika uwanja wa ndege
Read 13 tweets
FAHAMU JUU YA SIFA NA TARATIBU ZA KUWA URUBANI
-THREAD HOW TO BE PILOT-
Leo nitapenda tuongelee mambo machache juu ya Urubani watu wengi tumekua hatuna uelewa juu ya urubani kuhofia gharama....
🔁 Retweet iwafikie wengii
#ElimikaWikiendi

Shuka nao👇👇👇 ImageImageImage
Watanzania wengi hatuna uelewa tosha juu ya fani ya Urubani hii ni kutokana na kuogopa gharama kubwaa za Urubani pia na kupotoshana kwamba hatuna vigezo
Urubani ni kazi zilivyo kama kazi nyingine na inaingiza kipato kikubwa mno ikiwa ipo miongoni mwa kazi zenye kulipa vizuri na hulipa kuanzia $20,000-$40,000 per year hii inaongezeka kulingana na shirika husika
Read 21 tweets
JINSI YA KUANZISHA BIASHARA UKIWA UMEAJIRIWA: Biashara yoyote iwe mpya au ya zamani ina changamoto zake especially kwenye mazingira yetu. 50% Ya biashara zote ndogo zinakufa katika mwaka wake wa kwanza kuanzishwa. UZI #ElimikaWikiendi
Mtandao wa Investopedia ulitoa sababu ya biashara ndogo kufa, 1. Mtaji Mdogo, 2. Uendeshaji Mbovu, 3. Mpangilio Mbovu wa Biashara na Bidhaa yako au huduma yako haihitajiki sokoni (Hakuna wateja wanahitaji bidhaa zako). Pamoja na sababu zingine nyingi.
Sasa kama tulivyoona hapo juu changamoto ni nyingi. Kabla ya kufikiria kuanzisha biashara ukiwa umeajiriwa inabidi ujipange. Kitu kimoja kikubwa ambacho Ajira itakusaidia kipindi unataka kuanzisha biashara ni MTAJI pamoja na muda wa kujipanga kabla ya kuanza biashara full time.
Read 16 tweets

Related hashtags

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!