Miaka miwili tangu kuanza kwa sheria na kanuni za UWEZESHAJI WAZAWA (LOCAL CONTENT) kwenye madini hapa Tanzania je tunasonga mbele na kupata matokeo yaliyokusudiwa?
Je ushiriki wa Wazawa kwenye uchumi wa madini (manunuzi, ajira na uongezaji thamani) ukoje hata sasa?
Makampuni yanayomilikiwa na wazawa yanawezeshwaje ili kushiriki na kushindana kupata zabuni kwenye sekta ya Madini?
Makampuni yanayomilikiwa na Wazawa yanapata taarifa za kutosha juu ya fursa na zabuni mbalimbali zinazotelewa na makampuni ya madini na migodi hapa Tanzania? #localcontent
Wadau wa UWEZESHAJI WAZAWA wanatimiza wajibu wao?
Je kuna haja ya kuwa na mjadala wa pamoja wa wadau juu ya suala la UWEZESHAJI WAZAWA kwenye sekta ya Madini na sekta zingine zinazoingiliana?
UWEZESHAJI WAZAWA kwenye sekta ya madini una husiana na UWEZESHAJI WAZAWA kwenye sekta zingine za kiuchumi hapa Tanzania?
Nani anawajibika kuandaa nguvu kazi (labourers) wa kufanya kazi migodini na sekta nzima ya madini katika kuona wazawa wanakuwa tayari na ajira za sekta ya madini?
Panapo uzima tutajadili fursa, changamoto, na nini kifanyike ili mpango wa UWEZESHAJI WAZAWA kwenye sekta ya madini uweze kuwa na matokeo chanya. Hii ni kutokana na ujuzi, uzoefu na majadiliano ya hapa na pale na wadau. Kwa sasa Alamsiki!
@MadiniTanzania @neecempowerment Ni vipi suala la UWEZESHAJI WAZAWA kwenye sekta ya madini linafungamanishwa na harakati za UWEZESHAJI WAZAWA kuelekea uchumi wa viwanda? Kuna mikakati ya pamoja?
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.
