H Simba - MCIPS Profile picture
Consulting Procurement & Electronics (Telecom, Mining and Banking) Local Content Government Relations & Engagements
Feb 27, 2021 5 tweets 3 min read
Ili uweze kuchangamkia fursa zinazotokana na sheria na kanuni za local content kwenye madini ni lazima kwanza ujue kuna nini jikoni. Kwa ufupi madini ni sekta inayokadiriwa kuzungusha Tsh trilioni 4 kwa mwaka kwenye manunuzi. Sasa tambua ni nini kipo ndani.

#localcontent Fursa zipo za aina mbili
Moja utoe huduma kwenye migodi na sekta ya madini kwa ujumla, yaani huduma kama chakula (catering), ujenzi, Maintenance, huduma za meno na kinywa, bima, data, mawasiliano, usafirishaji, utafiti na kadhalika.

Naambatanisha tangazo hapa kama mfano
Feb 25, 2021 5 tweets 2 min read
Mining Local Content - Insurance and reinsurance opportunities A contractor, subcontractor, licensee or other allied entity engaged in a mining activity in the country shall comply with the provisions of the Insurance Act

##localcontent
Sep 30, 2020 9 tweets 2 min read
Post Tender Negotiations: Majadiliano baada ya kuwasilisha Zabuni.

Haya ni majadiliano yanayolenga kuboresha uelewa wa pande mbili za zabuni yaani MNUNUZI NA MUUZAJI (buyer/procuring entity and Seller/Supplier) Majadiliano haya hufanyika baada ya wasilisho rasmi la zabuni na kabla ya kutolewa hati ya mahindi 'award notice'. Ni lazima yafanyike kwa uwazi na kwa kushirikisha wadau wote muhimu, taarifa zitunzwe kama ukaguzi utahitajika.
Sep 26, 2020 14 tweets 3 min read
Moja kati ya njia bora ya #uwezeshajiwazawa yaani #localcontent ni ushirikishwaji na uwezeshwaji wa wafanyabiashara wa ndani. Nitaandika namna tuliwahi fanya katika safari ya uwezeshaji wazawa katika sekta ya madini hasa utoaji huduma kwenye migodi mikubwa hapa Tanzania Mwaka 2014 kulikuwa na mradi mkubwa wa uzuiaji kutu 'corrosion control' kwenye matenki ya process plant ya mgodi. Manunuzi yalikuwa yafanyike kwa manunuzi ya moja kwa moja 'sole source' kwenda kwa mkandarasi wa nje ya nchi. Gharama za mradi zilikuwa zaidi ya dola milioni moja.
Sep 25, 2020 6 tweets 2 min read
Miaka miwili iliyopita nilikutana na kampuni ya Kitanzania wakiwa wanasaka fursa za kufanya kazi na makampuni ya madini, migodi mikubwa na ya kati

Nikaomba taarifa zao, tukazipitia taarifa zao na kisha wakasajiliwa kama suppliers nilipokuwepo. Wakaanza kidogo kidogo Nikafanya mazungumzo na Mkurugenzi wao juu ya matakwa ya #localcontent na kwa namna gani wanaweza kunufaika zaidi na sheria hizo.

Lazima watafute wabia wa nje ambao kwa sheria mpya za uwezeshaji wazawa wanaelekezwa kufanya kazi na kampuni za wazawa kwa ubia.
Aug 5, 2020 6 tweets 1 min read
Mwaka 2018 nikiwa kwenye majukumu yangu nilifuatwa na supplier mmoja wa bidhaa za migodini. Akaniambia natafuta fursa ya ku-supply hapo 'kwenu'. Nikamuambia nitumie profaili yenu halafu tutawasiliana.

Baada ya wiki kadhaa ya ukimya nikakutana naye tena, nikamuuliza kimya? Mara hii akanitumia profaili yao. Ilikuwa vyema na alikuwa ameniambia wana uwezo wa kukidhi vigezo vyote.

Ili kampuni iwe mtoa huduma lazima isajiliwe kwenye mifumo ya manunuzi hivyo inapaswa supplier alete nyaraka zake za kampuni

Tukamuomba akaleta karibu zote.
May 13, 2020 4 tweets 3 min read
Business interests in hedging; time to work on developing local skills eg local drillers, operators.
Building capacity of local suppliers in local production, some products eg PPE have no reasons for not being produced locally. #Webinars #localprocurement #localcontent Gold is still a safe haven during #COVIDー19 pandemic #localprocurement #Mining
Mar 3, 2020 7 tweets 2 min read
Ujasiri ni Kuthubutu. Mwaka jana nilikutana na Mdau akaniuliza nafanyaje kupata fursa migodini? Nikamuuliza unataka fursa zipi? Akasema nataka tu 'kusupply'. Nikamuorodhoshea baadhi ya fursa na kumuambia hizi hapa nenda kasake huko duniani maana hata sasa sio wengi wanauza bongo so katafute uzipate.
Jan 22, 2020 10 tweets 2 min read
Miaka miwili tangu kuanza kwa sheria na kanuni za UWEZESHAJI WAZAWA (LOCAL CONTENT) kwenye madini hapa Tanzania je tunasonga mbele na kupata matokeo yaliyokusudiwa? Je ushiriki wa Wazawa kwenye uchumi wa madini (manunuzi, ajira na uongezaji thamani) ukoje hata sasa?
Nov 29, 2019 16 tweets 5 min read
Local Content in Mining; Stakeholders Mapping and Management. Key process in Local Content implementation Local Content in Mining; Know your stakeholders #localcontent
Nov 28, 2019 12 tweets 2 min read
10 Local Content Enablers - THREAD Mining Companies to have Standardised Procurement and Contract Management Process
Oct 29, 2019 7 tweets 1 min read
Participation of Youth, Women, Elders and People with Disabilities as a Special Social Group in public procurement has been observed to have a great impact on the economy of the country it is well managed. Having observed the importance of participation of this group in public procurement, the Public Procurement Act 0f 2011 as amended in 2016 has introduced preference that covers the special group.
Oct 11, 2019 5 tweets 2 min read
Leo nimefika Makao Makuu ya CAMARTEC- Centre for Agricultural Mechanisation and Rural Technology yaliyopo Arusha. Mapinduzi ya kilimo nchini yanategemea kwa kiwango kikubwa ufanisi wa taasisi hii. Image Hii ni moja ya zana zinazotengenezwa na CAMARTEC. Hii ni tractor ndogo yenye kazi nyingi, Multi-Role Tractor. Image
Sep 9, 2019 4 tweets 1 min read
Local Content in Mining. Ushiriki wa Watanzania kwenye fursa za ugavi na manunuzi, je kukosekana kwa taarifa za fursa bado ni kikwazo? Nini kifanyike kuongeza ushiriki. Tunaongezaje utayari wa wafanyabiashara wazawa kushiriki michakato ya manunuzi kwenye migodi? Makampuni ya kizawa yamejiandaa kupata kibali cha kukidhi mahitaji ya wawekezaji?
Jul 21, 2019 6 tweets 1 min read
Ili kujua ukubwa na kazi alizo nazo msaidizi wa ndani kwako 'housemaid' mpe off siku kadhaa kisha tembea kwenye kazi zake na uyabebe hayo majukumu yake. Kazi za ndani ni sekta nyeti inayochukuliwa poa. Kuna wakati 'mabosi' tumekuwa wepesi kuwalaumu na kuwatuhumu 'maids'. Walk a mile in her shoes. Saa nyingine inabidi kuvaa uhalisia, yajue na yafanye majukumu ya nyumba yako mwenyewe. Fanya usafi, lisha watoto, waandae kwenda shule. Zunguka ua, safisha ua, kuna kulisha mbwa, etc
Jul 9, 2019 4 tweets 2 min read
@DocFaustine Kwa ustawi wa wanawake, nadhani ni muda muafaka wa kuwazia kuwa na maeneo maalumu ya kunyonyeshea kwenye majengo ya Umma. Hii itawapa nafasi wanawake kushiriki masuala muhimu hata wakiwa MATERNITY. Nimeona jinsi ambavyo inazima mipango ya Wanawake wengi. Imagine Mama ana board meeting anashindwa kuhudhuria sababu tu ananyonyesha na mkutano ulipo hapana mazingira wezeshi. Hivi ndio vitu vinazuia wanawake kupaa na si uwezo wao binafsi. @DocFaustine @umwalimu Nawasilisha wazo. Linawezekana na litaleta matokeo chanya
Jul 1, 2019 8 tweets 3 min read
@DocFaustine Ndugu Mbunge, Naomba kuleta hoja ya kuangaliwa upya muda wa PATERNITY LEAVE. Siku 3 za sasa ni chache sana na hazimpi baba muda wa kutosha kumsaidia mama mzazi,kujenga ukaribu na mtoto, kupumzika baada ya mikikimikiki ya uzazi. Changamoto za kukosekana kwa wasaidizi wa ndani 'maids' mahiri na kuongezeka kwa changamoto za uzazi salama kuna leta umuhimu wa baba kuwepo pamoja na mama mzazi angalau kwa kipindi kirefu baada ya kujifungua na si hizi siku 3 kisheria za sasa.
May 17, 2019 9 tweets 1 min read
Do not forget where you came from. Treating your customers and employees well is the right thing to do—and it’s good for the bottom line.
Mar 25, 2019 4 tweets 2 min read
Tukiwa tunasherehekea timu ya Taifa kwenda #Afcon lazima tukubaliane ili tupate matokeo bora lazima #TFF na Nchi iwekeze kwenye michezo. Tulikuwa kundi jepesi lakini tumepita kwa kudra. Tunahitaji timu imara zaidi. Tuwekeze kwenye ufundi na ukuzaji vipaji. Kikosi tulicho nacho hatuwezi sema ni kikosi cha dhahabu.