Bonge La Afya Profile picture
Elimu, Mijadala na taarifa za afya

Apr 4, 2020, 19 tweets

#FahamuNaFesto | Zifahamu plates number za Tanzania

1. Magari Serikali ya Tanzania - Magari haya huwa na kibandiko chenye Herufi za mwanzo na baada ya hapo hufuatiwa na namba kadhaa mbele.

SU - Shirika la UMMA.
STK - Serikali Kuu Tanzania (Hiyo K,J au L ni series tu)
SM - Serikali za Mitaa

2. Magari ya viongozi - Huwa na Herufi ambazo uonesha cheo cha muhusika wa gari hiyo.

i) Magari ya Rais, Makamu Rais na Waziri mkuu huwa na nembo ya bibi na bwana pekee.

S-Spika
NS-Naibu Spika
CS-Chief Secretary (Katibu mkuu kiongozi)
JM-Jaji Mkuu Tanzania

Gari la Waziri huwa na herufi W ikifuatia na kifupisho cha jina la Wizara yake. Gari la Naibu waziri huwa na herufi NW ikifuatiwa na kifupisho cha jina la Wizara yake

Zanzibar pia huwa hivyo japo plate number huwa za rangi nyeupe tofauti na bara ambapo huwa njano

Magari ya balozi/wanadiplomasia.

i) Mabalozi wanaowakilisha nchi huwa na namba zenye rangi ya njano kwenye plate ya kijani.

TZ kwenye namba hizo humaanisha Tanzania-Zanzibar, magari haya hufanyia kazi Zanzbar na T humaanisha Tanzania.
CC/CD-Cors Diplomatique

ii) Wanadiplomasia wa mashirika ya kimataifa UN huwa na namba nyeupe kwenye plate za blue. Mfano shirika la Afya Duniani (WHO)

Magari kwa ajili ya matumizi ya Miradi inayofadhiliwa na watu to nje ya nchi huwa na kibao chenye herufi DFP (Donor's Fund Project) ikifuatiwa na namba tofauti tofauti. Pia tofauti na DFP utakuta mengine yana DFPA

3. Magari ya Wakuu wa Mikoa huwa na kibandiko ambacho kuanza na herufi RC na kisha hufuatiwa na herufi ambazo ni kifupi cha mkoa wake.

4. Magari ya Jeshi.

PT-Polisi Tanzania
JWTZ-Jeshi la wananchi wa Tanzania
ZM-Zima moto

Mkuu wa Majeshi (CDF) kibao hakina namba bali kunakuwepo na Nyota nne kwenye kibao cha gari lake

Kenye picha kidogo hapo ndo mtihani, wasije wakanifata 😂😂😂sema mnazifahamu sio

MT-Magereza Tanzania
JR- Jaji wa Mahakama ya Rufaa
JK- Jaji Kiongozi
J- Jaji wa Mahakama Kuu
WN (abc) ni waziri wa nchi
JM ni Jaji mkuu
CAG ni Chief Auditor General

CGP-Commissioner General of Prison(Mkuu wa Magereza)

E-Escort ni namba za magari ya ikulu yanayokua katika misafara ya viongozi kama rais,makamu wake na waziri mkuu. Bila kusahau rais na makamu wake wa Zanzibar.

SMZ ni namba za magari ya afisi zilizo chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Magari yenye plate number za Rangi ya Njano
•Magari ya Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu
•Spika wa Bunge la Tanzania na Naibu wake
•Waziri na Naibu Waziri wa Wizara mbalimbali
•Gari za Serikali za Mitaa
•Mashirika ya Umma. Mfano; TANESCO
•Magari ya Wakuu wa Mikoa

Magari yenye plate number za rangi ya Kijani
•Magari ya balozini Mbalimbali nchi Tanzania
•Magereza Tanzania

Magari yenye plate number za rangi nyeusi
•Magari ya Police wa Tanzania (Maandishi ya rangi ya njano)
•Magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania (Maandishi ya rangi nyeupe)

Magari yenye plate number za rangi nyekundu
•Mkuu wa Majeshi (CDF) (Nyota zilizopo huwa na rangi ya dhahabu)
•Magari kwa ajili ya matumizi ya Miradi inayofadhiliwa na watu toka nje ya nchi

Magari yenye plate number za rangi nyeupe
•Magari kwa ajili ya biashara (Commercial Use)
•Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Ongezea hii

CGI-Commissioner General Immigration

IGP-inspector General Police

CDF- Chief of Defence Forces

CGF- Commissioner General Fire

CGP- Commissioner General Prisons

CS- Chief Secretary

CAG- Comptroller and Auditor General

AG-Arttoney General

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling