Mwaka 2018 nikiwa kwenye majukumu yangu nilifuatwa na supplier mmoja wa bidhaa za migodini. Akaniambia natafuta fursa ya ku-supply hapo 'kwenu'. Nikamuambia nitumie profaili yenu halafu tutawasiliana.
Baada ya wiki kadhaa ya ukimya nikakutana naye tena, nikamuuliza kimya?
Mara hii akanitumia profaili yao. Ilikuwa vyema na alikuwa ameniambia wana uwezo wa kukidhi vigezo vyote.
Ili kampuni iwe mtoa huduma lazima isajiliwe kwenye mifumo ya manunuzi hivyo inapaswa supplier alete nyaraka zake za kampuni
Tukamuomba akaleta karibu zote.
Katika nyaraka zile hakukuwepo na hati safi ya mlipa kodi 'tax clearance certificate'. Nikamuomba, akaituma.
Nikamuuliza swali lingine je una mashine ya EFD? Na naweza pata nakala ya risiti ya EFD ya kampuni yako ikionesha unatoa risiti zinazokubalika? Maana bila EFD hakuna kitu
Jibu la baada ya swali hili ni... kama hutaki kunipa hizo kazi za huko kwa 'mzungu' we niambie tu sio tunaulizana maswali hayaishi. Ukweli ni kwamba 'compliance' ni jambo muhimu sana katika kufanya kazi na makampuni ya madini. Na Wafanyabiashara wengi wana changamoto za nyaraka
Katika uwezeshaji wazawa jambo lingine muhimu ni urasimishaji wa biashara, utunzaji nyaraka na 'compliance'. Ni vitu vidogo ila vinawakwamisha wengi.
Kwenye hili la kuomba nakala ya risiti ya EFD ieleweke inatokana na experience ya suppliers wengi kusema tunatoa risiti za EFD ila muda ukifika wa malipo kama ameshapata kazi analeta risiti ya kawaida. Mnaanza kuvutana na majibizano yasiyo ya lazima. Ndio utaratibu huu ukaanza.
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.
