Malembo Farms Profile picture
Our mission is to respond by feeding Africa🌍 l Agribusiness Consulting l Sustainable Agriculture l @MalemboGlobal l @AcademyFarms ll @UgaliElimu #GlobalGoals.

Aug 22, 2020, 11 tweets

#Vietnam na KILIMO.
Vietnam ni Taifa lililopata Uhuru wake 1945 kutokana na Mapinduzi,limekuwa katika kipindi kirefu na vita vya wenyewe kwa wenyewe kasikazini na kusini Mwa nchi yao vita hivyo vilikuwa vikichangiwa na Mataifa Kama,Marekani,Korea,China,Ufilipino,Thailand.

Ni Taifa lenye wananchi zaidi ya Milioni 91,Mwanzoni Mwa mwaka 1970 vita hivyo vilikwisha Nchi hiyo ikiwa na hali Mbaya kiuchumi,Miundombinu,Ukame,Mfumuko mkubwa wa bei,kudorola kwa pato la Taifa kutokana na uzarishaji hafifu.@ayubu_madenge @MarekaMalili @masoudkipanya

Tanzania na Vietnam ni Mataifa ambayo yemekuwa na urafiki wa muda mrefu toka enzi za utawala wa Mwl Julius Nyerere,Kuanzia 1960 tulikuwa na urafiki wa kisiasa na baadaye 1965 ikawa rasmi tukawa na urafiki wa kidpromasia.Tumekuwa na ushirikiano wa Muda mrefu.

Tumekuwa na ushirikiano wa Muda mrefu,1980 Vietnam ilituma Wataalamu wake kuja kujifunza Tz kwenye sekta ya kilimo Uvuvi,Walijifunza kilimo cha Korosho,Mpunga na Uvuvi walienda kwenye vyuo vyetu vya kilimo pia walijifunza namna ya kumfuga na kuzarisha samaki aina ya sato.

Mwaka 1970 ilizinduka kutoka usingizini,Serikali yake ikaangalia rasimali ndogo zilizopo wanaweza zitumiaje kunyanyuka kiuchumi wakaanzisha Sera iliyoitwa kwa lugha ya kivietnam #DOIMOI kwa tafsiri yake #Mabadirikonakufanyaupya.

Sera ya Doi Moi ilijikita zaidi katika Maswala ya #Kilimo #Viwanda #Biashara.sasa hivi Vietnam inatamba kwenye soko la Dunia kwa kuuza Mchele,kahawa,korosho na bidhaa Nyingine za Kilimo na viwandani.kufanikiwa kwa Sera hiyo Vietnam Imekuwa mfano wa kuigwa kila duniani.

Walitilia Mkazo na utekelezaji,Mfn
Kwenye kilimo walijikita zaidi kwenye hatua tatu 1.Walianzisha kilimo cha Mshikamano wa vikundi vya uzalishaji Serikali ilitoa Aridhi na Vitendea kazi 2.Ushiriki wa vikundi vidogo vidogo. 3.kilimo cha ushiriki wa Kimataifa.

#Magumu #waliyopitia.
Vietnam wamepitia Magumu mengi sana hadi kufikia hapo ilipofikia kiuchumi haikuwa kazi rahisi kufikia kwenye uchumi wa kati kutokana na Historia yake Sifa moja kuu ya Vietnam ni UTHUBUTU NA UWEZO WA KUSIMAMIA MIPANGO YAO.

Mpaka Mwaka 1993 walifanikiwa kupunguza Umasikini kwa karibu ya 60% ya wananchi wake.Mwaka 1999 walikuwa Ni miongoni Mwa mataifa yanayoangiza Mchele kwa wingi lakini Mwaka 2014 imeweza kuuza Mchele na kuliingizia Taifa dolla za Kimarekani Milioni 1.2

Robo tatu ya Mchele waliozarisha Mwaka 2014 ulinunuliwa Tz,Mbegu wamechukua kwetu na walijifunza kwetu .Tz na Vietnam 2014 tulifanya biashara yenye thaman ya dolla za kimarekani Milioni 152 sawa na bilioni 320 Tz tukiwa tumeuza bidhaa zetu Vietnam zenye thamani ya Bilioni 100

Mwaka 2014 Tz iliuza korosho kwenye soko la Duniani tan 189000 na kuliingizia Taifa Bilioni 450 lakini Vietnam waliweza kuuza tan 257000 na kuliingizia Taifa lao dolla za Marekani milioni 1.8 Sawa na Tilioni 4 za Tanzania,Mbegu wamechukua kwetu wamejifunza kwetu.

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling