HISTORIA YA SIKU YA LEO MIAKA 19 ILIYOPITA USA NA DUNIA KWA UJUMLA...
Siku kama ya leo 2001 Dunia ilitawala huzuni na simanzi kubwa kutokana na Shambulio la September 11 2001 Shuka nao... 👇👇
Retweet ifike mbalii
#ElimikaWikiendi
#WajumbeTuinuane
Siku ya Jumanne, tare 11 mwezi September mwaka 2001 majira ya saa 2 na dakika 46 asubuhi mpaka saa 4 na dakika 28 asubuhi lilifanyika shambulio kubwa na baya zaidi kuwahi kutokea na kufanywa na adui katika ardhi ya nchi ya Marekani.
Majira ya saa 2 na dakika 46, ndege aina ya Boeing 767-223ER (A.A. Flight 11) iliyosajiliwa kwa namba N334AA, mali ya shirika la American Airlines ambayo iliruka kutoka Boston katika uwanja wa ndege wa Logan International Airport ikitegemewa kutua katika uwanja wa ndege
Los Angels International Airport ambamo ndani yake kulikuwa na abiria 81 na wafanyakazi 11 ilijibamiza na kulipua jijini New York kwenye jengo la Kaskazini (North Tower) la kituo cha kibiashara cha kimataifa (World Trade Center) jengo ambalo lilikuwa na ghorofa 110
Dakika chache baadae, ndege nyingine aina ya Boeing 767-222 (U.A Flight 175) iliyosajiliwa kwa namba N6126UA inayomilikiwa na shirika la United Airlines ambayo pia iliruka kutoka Boston katika uwanja wa ndege wa Logan International Airport
Ikitegemewa pia ikatue katika uwanja wa ndege wa Los Angeles International Airport ambamo ndani ilikuwa na abiria 56 na wafanyakazi 9 ilinibamiza na kujilipua pia jijini New York South Tower la kituo hicho hicho cha biashara cha kimataifa. Jengo hili pia lilikuwa na ghorofa 110.
Kujibamiza kwa kwa ndege hizi na kulipua majengo haya kulisababisha maghorofa haya kudondoka kabisa (total collapse) na yalisababisasha kudondoka kwa majengo mengine kama vile ghorofa la 7 WTC Tower na maghorofa mengine kumi yaliyomo ndani ya kituo cha cha kimataifa (WTC Complex)
Wakati haya yakitokea jijini New York, ndege nyingine aina ya Boeing 757-223 (A.A. Flight 77) iliyosajiliwa kwa namba N644AA inayomilikiwa na shirika la American Airlines ambayo iliruka kutoka katika uwanja wa ndege wa Washington Dulles International Airport ikitegemewa
Ikatue kwenye uwanja wa Los Angels International Airport ambmo ndani yake ilikuwa na abiria 58 na wafanyakazi iligeuza njia na kurudi nyuma na kwenda kujibamiza na kulipua jengo la Pentagon, ambalo ndio Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani (US Department of Defense).
Muda huo huo pia, ndege nyingine aina ya Boeing 757-222 (U.A Flight93) iliyosajiliwa kwa namba N591UA mali ya shirika la United Airlines ambayo iliruk
a kutoka Newark Intenational Airport ikiwa na abiria 37 na wafanyakazi 7 na ikitegemewa ikatue
katika uwanja wa San Fransisco International Airport ilidondoka karibu na eneo la Shanksville, Pennsylvania na inasadikiwa ndege hii ilikuwa njiani kwenda kujibamiza katika Ikulu ya marekani.
Mfululizo wa mashambuluo haya ya
siku hii yalikuwa ni tukio baya zaidi katika historia kwa Marekani kushambuliwa na adui katika ardhi yake mwenyewe.
Jumla ya watu 2997 walifariki na watu 6000 wengine walijerehiwa vibaya mno.
Hasara hii inafikia jumla ya shilingi za kitanzania Quadrillion 6 (Trilioni elfu sita za kitanzania).
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.
