Eng. Mbwambo Profile picture
Oct 1, 2020 11 tweets 2 min read
Leo Tumjue Mnyama Nyegere
RT iwafikie wengi
Ongezea unalojua zaidi
Nyegere ni moja kati ya wanyama wenye wivu sana hapa duniani. Chakula chake kikubwa ni asali,yeye hupanda juu ya mzinga wa asali na kuujambia, baada ya mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kula.
Mwili wake una ngozi ngumu sana kiasi hata nyuki akimuuma hakuna chochote kinatokea.
Sep 23, 2020 7 tweets 2 min read
FURSA YA KILIMO CHA NYOKA
Achana connection za ifm njoo connection hii...

Kilimo cha nyoka ni moja ya kilimo chenye faida sana ,mmoja anaweza akaanzisha kilimo hichi ukizingatia thamani ya "snake venom" ipo juu sana. Sumu ya nyoka inatumik kwa wingi kwenye viwanda vya famasia na viwanda vya vipodozi thamani ya "snake venom " ipo juu sana kutokana na uhitaji wake

Gram moja ya "snake venom" kwa soko la kimataifa inauzwa $1880 ,na kwenye soko la Afrika kusini inauzwa kwa makadirio ya Rand 25K
Sep 19, 2020 5 tweets 11 min read
Wana familia Twitter pamoja sanaa...I appreciate you more hata kama hauko kwa list we're together tuendelee kusongesha gurudumu letu . Image @babalao__
@FordMussa
@cyancuty
@Mnyone_og
@UGmanofficial
@kanjunju_john
@FFerein
@judiealoyce
Circle 2
@TOTTechs
@Paschals_Son
@DeucSnox
@gudume_
@KevnashEdson
@Laurent12020
@Kasilo_Honester
@evanda96340637
@frosttaz07
@IdrisSultan
@AllyMatimu
@officialsamtz
@MkutubiRajabu
Sep 17, 2020 5 tweets 1 min read
MASKINI & TAJIRI:-
1.Maskini hudhani utajiri ni bahati,tajiri hudhani umaskini hutokana na uvivu na uzembe. Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake,tajiri ni mkubwa kuliko matatizo yake. 2.Tajiri bila masikini ni maskini lakini maskini bila tajiri ni tajiri.Umaskini ni matokeo ya fursa zote ambazo hazikutumika kwa usahihi,utajiri ni jumla ya fursa zote zilizotumika kwa usahihi
Sep 14, 2020 21 tweets 4 min read
MWL.JULIUS KAMBARAGE NYERERE NI BABA WA TAIFA LA TANZANIA.
Kuelekea Kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa .Tujue machache kumhusu
1.Alizaliwa tarehe 13/04/1922 Butiama na kufariki tarehe 14/10/1999 kule London. Ni Raisi wa kwanza Afrika kuachia madaraka kwa hiari yake mwenyewe. Image 2.Ni Raisi wa kwanza kuhama Ikulu na kwenda kuishi kwenye nyumba aliyoijenga kwa mkopo akiwa bado Raisi.
3.Ni kati ya Raisi aliyekuwa analipwa mshahara mdogo duniani na pia raisi aliyewahi kulipwa mshahara mdogo barani Afrika mpaka sasa.
Sep 14, 2020 15 tweets 2 min read
Mambo Ya Msingi Unayopaswa Kufahamu Kuhusu Nidhamu Ya Pesa.
Ni bora tuwe wakweli katika somo linalohusu pesa kwani ndilo somo ambalo watu wengi hufeli sana hasa pale wanapozipata,wapo baadhi ya watu wakizipata pesa hujikuta hawana kitu au zimeisha pasipo kufanya mambo ya msingi Wengi wao wamesahau ya kwamba pesa zina kanuni na misingi yake ambapo kila mwenye kuzihitaji ni lazima aweze kuzielewa kanuni hizo, na pia kanuni hizo ni lazima aendane na misingi pamoja na nidhamu ili ziweze kujizalisha.
Sep 14, 2020 8 tweets 2 min read
NUKUU MUHIMU ZA MWALIMU J.K NYERERE KUTOKA KATIKA KITABU CHAKE “TUJISAHIHISHE MAY 1962”

1.“Kujielimisha ni kutafuta ukweli wa mambo.”

2.“Ukiondoa matatizo wayapatayo binadamu kwa sababu ya mambo kama mafuriko,nzige,kiangazi,n.k., matatizo yao mengi hutokana na unafsi.” Image 3. “Nitasema kweli daima.Fitina kwangu ni mwiko.”

4. “Wengine humwona mwenzao anafanya kosa.Badala ya kumwambia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya.Lakini hawanyamazi kimya kabisa! Watakwenda kumteta katika vikundi vya siri siri.”
Sep 11, 2020 13 tweets 3 min read
HISTORIA YA SIKU YA LEO MIAKA 19 ILIYOPITA USA NA DUNIA KWA UJUMLA...
Siku kama ya leo 2001 Dunia ilitawala huzuni na simanzi kubwa kutokana na Shambulio la September 11 2001 Shuka nao... 👇👇
Retweet ifike mbalii
#ElimikaWikiendi
#WajumbeTuinuane ImageImageImage Siku ya Jumanne, tare 11 mwezi September mwaka 2001 majira ya saa 2 na dakika 46 asubuhi mpaka saa 4 na dakika 28 asubuhi lilifanyika shambulio kubwa na baya zaidi kuwahi kutokea na kufanywa na adui katika ardhi ya nchi ya Marekani.
Sep 11, 2020 4 tweets 1 min read
DUNIA & MAISHA
————————————

1.Mbio za maisha ni za ajabu sana,anayetafuta hachoki na aliyepata anataka zaidi.Usiongeze mwendo,ongeza maarifa kwa sababu haushindani na mtu unashindana na malengo yako.
#WajumbeTuinuane #wajumbefunfriday 2.Duniani ukikosa akili utakufa kwa manung’uniko.Usipojifikiria hayupo atakafikiri kwa niaba yako kwenye duniani hii ambayo hata mtoto wa Paka anafaulu kwa njia za Panya.
Sep 11, 2020 5 tweets 4 min read
Ijue Antonov AN-225
An-225 Mriya ni ndege ya Ukraine ambayo ni kubwa kuliko zote duniani miaka ya 1988 hadi 2020.Ina injini sita. Ilitengenezwa na kampuni ya Antonov. Imepengwa kwa shughuli za mradi wa usafiri wa anga-nje wa Umoja wa Kisovyeti.
#WajumbeFunFriday
#WajumbeTuinuane ImageImageImage Ndege ya kwanza ilikamilishwa mwaka 1988, nakala ya pili ilianzishwa bila kumaliza kutokana na kuporomoka kwa Umoa wa Kisovyeti mwaka 1989 .

Ndege ya pekee iliyokwisha iliwahi kupimzishwa kwa miaka kadhaa lakini ilirudishwa kuanzia 2001.
Sep 8, 2020 5 tweets 1 min read
Wazazi wako hawakuchagua wakuzae wewe na wala wewe hukuchagua uzaliwe na wazazi wako ila Mungu aliwaamini kwa kiwango ambacho alijua wanaweza kukulea na ukakua katika mazingira hayo. Furaha ya wazazi ni kuona mtoto wao anakuwa na furaha muda wote na jukumu lake kubwa ni kuhakikisha unapata kile kilicho bora ambacho wao hawakupata kwa wazazi wao.
Sep 8, 2020 4 tweets 1 min read
SABABU ZA KWANINI TUNAPASWA KUSOMA VITABU

1. Vitabu vinakusaidia kujiamini zaidi.

2. Vitabu vinakusaidia kusafiri ulimwenguni kwa njia ya bei rahisi.

3. Vitabu huendeleza utu wako.

4. Vitabu hutoa chakula cha mawazo. 5. Vitabu vinakuchekesha vinafurahisha na kufikiria.
6. Vitabu vinakuvutia kuelekea ukamilifu.
7. Vitabu huchochea ubunifu.
8. Vitabu huleta talanta ya uandishi.
9. Vitabu vinakusaidia katika kuwasiliana.
Sep 7, 2020 4 tweets 1 min read
SHIKA HII KANUNI ITAKUSAIDIA KATIKA MALENGO YAKO

Ili upate mafanikio ambayo hukuwahi kupata maishani mwako lazima ufanye kitu ambacho hujawahi kufanya katika maisha yako. Kama unataka uongeze ufaulu wako katika mitihani yako shuleni lazima ufanye kitu ambacho hukuwahi kufanya ulipokua unafeli. Aidha usome tofauti na ulivokua unasoma au ufanye vinginevyo ambayo hukufanya awali.
Sep 5, 2020 5 tweets 5 min read
Tuanzie hapo amesoma school of Tanganyika wewe unahoji nini elimu yenyewe tunajua umeunga unga @HKigwangalla ImageImageImageImage ImageImageImageImage
Sep 2, 2020 5 tweets 1 min read
TUTAMBUE HIZI NYAKATI

Tupo kwenye nyakati zenye starehe nyingi lakini furaha kidogo.

Nyakati zenye madaktari wengi lakini wenye afya Bora wakiwa wachache.

Nyakati zenye nyumba nyingi za ibada lakini wenye imani ni wachache . Nyakati zenye wasomi wengi lakini matatizo mengi.

Degree nyingi na uelewa mwingi lakini fikra kidogo.

Nyakati zenye nyumba kubwa lakini familia ndogo.

Nyakati zenye Mambo mengi lakini Muda mchache.
Aug 31, 2020 12 tweets 2 min read
ZIJUE AINA MBALI MBALI ZA WAKE WANAVYOKUA BAADA YA NDOA

Nimejaribu kuonyesha jinsi wanawake wanavyokua baada ya ndoa na kuanza kuishi pamoja kama familia....Kikubwa ni ustahimilivu kujua ni vipi mwnaume umhandle mke wako

Shuka nao 👇👇👇 👇 1.Mke sherehe (party wife)
Hawa muda wote wanawaza sherehe na starehe tu, utawasikia kesho sendoff mara kitchen party .
Wako tayari kutumia hela ya chakula kwa ajili ya kuchangia sherehe.
Aug 31, 2020 9 tweets 2 min read
Karibu katika Taifa letu...Sijataja nchi kumbuka

1. Taifa ambalo binti zake wakimwona Mzungu wanadhani ana hela.

2. Taifa ambalo ukiongea kiingereza unaonekana umesoma.

3. Taifa ambalo bank haikutafuti we ndo unaihonga ikukopeshe. 4. Taifa ambalo ukifeli unakuwa mtangazaji wa kipindi maalumu kabisa.

5. Taifa mbalo simu kali ni dili hata kama vocha waweka za jero jero.

6. Taifa ambalo unazaliwa umeme shida, unafika miaka 30 hata huna bajeti ya Jenereta/Solar, unailaumu tu TANESCO.
Aug 30, 2020 21 tweets 11 min read
FAHAMU JUU YA SIFA NA TARATIBU ZA KUWA URUBANI
-THREAD HOW TO BE PILOT-
Leo nitapenda tuongelee mambo machache juu ya Urubani watu wengi tumekua hatuna uelewa juu ya urubani kuhofia gharama....
🔁 Retweet iwafikie wengii
#ElimikaWikiendi

Shuka nao👇👇👇 ImageImageImage Watanzania wengi hatuna uelewa tosha juu ya fani ya Urubani hii ni kutokana na kuogopa gharama kubwaa za Urubani pia na kupotoshana kwamba hatuna vigezo
Aug 23, 2020 6 tweets 1 min read
MISTARI 10 YA BIBLIA INAYO NIFARIJI NYAKATI ZA TAABU.

Mistari hii 10 ya Biblia inatukumbusha kwamba hatuko peke yetu.Daima Mungu yu pamoja nasi.Pokea nguvu kupitia neno la Mungu na umimine moyo wako kwake yeye anaye yajua mahitaji yako yote na hujibu pale unapolitia jina lake Yohana 14:18
Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.

Yoshua 1:5
Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha.
Aug 14, 2020 29 tweets 7 min read
FAHAMU MAMBO MUHIMU YA KUFANYA ENDAPO KUTATOKEA TETEMEKO LA ARDHI
-THREAD HOW TO BEHAVE DURING EARTHQUAKE-
Nimechambua machache na kuyaleta humu baada ya juzi kuona taharuki watu tukiwa hatujui nini cha kufanya endapo kutatokea earthquake.
🔁 Retweet ifike mbali
#ElimikaWeekend ImageImageImageImage Je unaufahamu juu ya tahadhari za kuchukua endapo kukitokea tetemeko la ardhi (Earthquake)
Aug 6, 2020 40 tweets 17 min read
FAHAMU JUU YA UFUGAJI WA SAMAKI YAAN AQUACULTURE/ FISH FARMING

-THREAD AQUACULTURE-
Leo tushare ideas juu ya ufugaji wa samaki moja ya biashara inayowaingizia pesa sanaaa Bara la Asia huku 🇹🇿 ikisahaulika japo tukijitahidi
#NipeDili
#KilimoFursa

🔁Retweet ifike mbali UFUGAJI WA SAMAKI

Tasnia ya ufugaji wa samaki inajumuisha ukuzaji wa viumbe vya kwenye maji (bahari na maji baridi) katika mazingira tofauti na yale ya asili. Lengo kuu ni kukuza kwa muda mfupi ili kujipatia lishe, kipato na kutunza mazingira ya bahari, mito, maziwa nk.