Kuduishe Kisowile Profile picture
MD | WHO Fides Influencer | P1L1 | Health Communications Consultant | #MeToo | Program Lead #MweleMalecelaDOA | #KuduAfyaTips | #DaktariMwandishi 🇹🇿 #RadFem

Sep 15, 2020, 5 tweets

Nilivyokuwa form 3, nilipendekezwa kuwa kiranja wa afya msaidizi, kiukweli nilikuwa sitaki, umoniter wa darasa ulikuwa unanitosha.
Tukaitwa ofisini kujinadi kwa staff, nikasema, "naitwa Kuduishe Kisowile, nimependekezwa kuwa kiranja msaidizi wa afya, na sitaki."
Nikasikia, (1/5)

mwalimu anasema, "unasema?"
Nikarudia, "sipo tayari, sitaki kuwa kiranja."
Wote wakacheka. Hakuna aliyetegemea lile jibu nadhani.
Wakaniruhusu nikaondoka.
Matokeo yalivyotoka nikachaguliwa.😂😭
Nikaenda ofisini kwa mwalimu mkuu msaidizi nalia, sitaki kuwa kiranja. 😂😂😭 (2/5)

Nikamwambia, "kwanini mmenichagua wakati nilisema sitaki?"
Akasema, "ulidhani kusema vile kungefanya jina lako likatwe, lakini sisi tuliona kitu tofauti. Tuliona binti mwenye msimamo, anayejiamini ambaye haogopi kusema mawazo yake mbele ya viongozi wa shule, tukaona unafaa" (3/5)

Nilijaa upepo balaa. Nikamsihi anifute tu kwasababu hata hivyo nilikuwa moniter tayari siwezi kuwa na kazi mbili.
Akasema sawa, niende kesho atatangaza mtu wa kupokea majukumu.
Nikashusha pumzi.
Kesho yake akatangaza moniter mpya badala ya kiranja mpya. 😂😂😂 I WAS FURIOUS (4/5)

Lakini nikakubali kishingo upande, nikaanza kazi.
Nilikuwa naona aibu kuamrisha mstarini, sidhani kama nimewahi hata.
Lakini mwisho ya yote, niliipenda ile kazi na ilinisaidia sana kunijenga kujiamini.
Nikajifunza, kila mtihani una kusudi lake na RIZIKI YAKO NI YAKO TU. 💙 (5/5)

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling