#TOTTechs 🇹🇿 Profile picture
Washauri na wataalamu wa Teknolojia || 💻 Computers ||📱 Phones || 🎮 Games ||🎯 Softwares || ⚙️ICT Hardwares || 🛡ICT Security || 📧tottechstz@gmail.com

Sep 15, 2020, 14 tweets

ANDROID 11

Android 11 imetoka, ni jambo zuri kwa watumiaji wa Android, simu za mwanzo Kabisa zilizoanza kupokea Android 11 updates ni Google pixels, OnePlus, Oppo, Xiaomi na Nokia. Simu zingine zitapata Android updates week chache zijazo

Tuangalie features zilizomo [ uzi ]👇

◾️ MEDIA CONTROL

Media players zitakuwa zinaonyesha media controls zote ( prev, stop, next etc) moja kwa moja kutoka kwenye "toggle bar" ( Sehemu ya juu ya simu kwenye notification pannel ambapo itaonyesha wimbo, media husika na control zake)

◾️MEDIA OUTPUT ( Quickly select media output)

Sehemu ya notification pannel ambayo itakusaidia ku-sitch/badili ambapo unaweza kuchagua utumie speaker ya simu au Bluetooth device au device yoyote ambayo iko connected na simu yako kwa haraka zaidi.

◾️NOTIFICATION PANNEL

Moja kati ya maboresho makubwa ni kwenye notification pannel. hapa wamegawa sehemu mbili, hapa kuna internal App notifications na messaging notifications, utapata sms notifications zote kwenye mpangilio mzuri unaweza kugroup aina ya messages au ku-pin user

◾️ CHAT BUBBLES

Chat bubble ni kama ile ya Facebook messenger, ukitumiwa message kinatokea kiduara kwenye screen na dot nyekundu, unaweza kuchat na mtu pasipo kufungua messaging app husika na pia itarahisisha kuonyesha jumbe ambazo hazijasomwa pasipo kufungua chat apps

◾️HOME SCREEN

Kwenye home screen wameongeza kipengele cha " Home screen Apps suggestion" kwenye android 11 unaweza kuchagua ni app gani ikae chini kwenye home screen ili kurahishisha matumizi kulingana na Apps uzitumiazo mara nyingi ikumbukwe home screen ilikuwa na default Apps

◾️DEVICE CONTROLS AND PAYMENT

kama unapata shida ya ku-connect smart devices nyumbani kwako ( Smart TV, Cars etc) basi android 11 ni suluhisho, power button itatumika siyo tu kwa ajili ya kuzima na kurestart bali kutakuwa na option ya ku-connect na ku-control smart home devices

Pia unaweza kupata Google Pay Card bila ya kufungua app husika, Hii itarahisisha malipo ( Google pay) pasipo kuwa na App, ni rasmi sasa power button imepata matumizi mengi zaidi kuliko awali

◾️ PRIVACY

Android 11 Privacy

Ulinzi ni kitu cha msingi kwenye kila program endeshi ( operation system) na moja ya feature iliyoongezwa ni ONE TIME PERMISSION

Je "One time Permission" inafanyaje kazi, unapofungua App kwa mara ya kwanza na kukuomba permission ya kuacess

vitu vyako ( Permission to access photos, contacts, phone book etc) unaweza kuruhusu kwa mda huo na ukifungua hiyo app kwa mara Nyingine unaruhusu "one time permission" kwa mara nyingine tena hii itazuia apps kuacess vitu vyako kwa mda wote

◾️ SCREEN RECORDING

Rasmi sasa screen recording imekuwa built-in feature ya Android 11, kuliko Kudownload Screen recording apps kutoka Play Store unaweza kupata kwenye home screen yako na ukarekodi chochote kwa mfumo wa sauti/audio au maandishi

◾️VOICE ACCESS

Ile feature ya ku-control simu yako kwa kuongea sasa imeboreshwa zaidi na inauwezo wa kutambuana screen contents na kuziweka kwenye sauti kisha ikakuletea majibu ya maulizo yako

◾️PREDICTION TOOLS

Android 11 inakurahisishia kazi. inauwezo wa ku-sort automatically apps ambazo unazitumia mara kwa mara na kuziweka kwenye smart folder, zitakaa kwenye home screen na utazipata haraka zaidi

Pia inauwezo wa kutambua apps zipi unazitumia kwa mda gani

Mfano: kama asubuhi unatumia apps za mazoezi Basi automatically hiyo app itakuwa inapop-up na kutoa notifications kama mda wa mazoezi umefika

Hizo ni Baadhi za features

Uzi umethibitishwa na @chawanyu

Cc: @Mkuruzenzi @razaqdm01 @njiwaflow @chawanyu @ITexpertTz @WizaraUUM

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling