WatuNiStory Profile picture
By @djtee255 #ShujaazTZ / Simulizi halisi za vijana kuhusu kazi, maisha, ndoto, msukumo, nguvu na udhaifu kuhusu maisha yao. #WatuNiStory #Shujaaz #Hatukuchori

Sep 24, 2020, 5 tweets

1/5 “Nilisoma chuo UDSM hadi mwaka wa tatu lakini sikuhitimu. Sikuhitimu kwa sababu ukweli ni kwamba, sikuzingatia masomo ipasavyo, nilipata ajira nikashindwa ku-balance kati ya shule na kazi. Nikaishia kufeli mitihani kadhaa. Ilikua nihitimu mwaka 2015. Miaka yote nimeendelea..

2/5 ...kufanya kazi mbalimbali kwa kutegemea kipaji changu tu. Japo kuna nyakati nilikosa kazi zilizohitaji mtu mwenye degree na sikua na hizo sifa. Ni jambo ambalo limekua likiniumiza na kunifanya nijiskie vibaya. Familia yangu pia iliumizwa na hilo sababu walilipa ada miaka..

3/5 ..yote mitatu ya chuo. Na niliumia sana kuiumiza familia yangu. Namshukuru Mungu mwaka huu baba yangu amenipa nafasi tena ya kurudi chuo na kunilipia ada. Nime-apply tayari nangoja majibu. Japo naona kama miaka mingi imeshapita, nina miaka 28 sasa..

4/5 ..Ila naamini ni nafasi nyingine ya kusahihisha makosa yangu. Naanza safari ingine ya miaka mitatu kuitafuta degree. Nawashauri watu wanapokua na nafasi ya kusoma, wazingatie masomo. Na hata ambao walianguka kama mimi, kama watapata nafasi ingine, wajitie nguvu na wasiogope..

5/5 ...kuanza upya. Naamini Mungu atanisaidia.” #WatuNiStory

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling