Miaka miwili iliyopita nilikutana na kampuni ya Kitanzania wakiwa wanasaka fursa za kufanya kazi na makampuni ya madini, migodi mikubwa na ya kati
Nikaomba taarifa zao, tukazipitia taarifa zao na kisha wakasajiliwa kama suppliers nilipokuwepo. Wakaanza kidogo kidogo
Nikafanya mazungumzo na Mkurugenzi wao juu ya matakwa ya #localcontent na kwa namna gani wanaweza kunufaika zaidi na sheria hizo.
Lazima watafute wabia wa nje ambao kwa sheria mpya za uwezeshaji wazawa wanaelekezwa kufanya kazi na kampuni za wazawa kwa ubia.
Nikawaunga na kampuni za Australia na Uchina. Jamaa akasafiri kwenda Uchina akafanya mazungumzo na akafunga dili. Kisha jamaa wa Australia wakaja Tanzania wakakutana wakafunga dili.
Akawa 'Sole Authorised Distributor' kwa Ukanda wa East Africa wa makampuni matatu hivi.
Leo amenipigia simu kushukuru anasema Kaka naomba nishuhudie kwako tunaanza ujenzi wa Kiwanda na mmoja wa wale jamaa na huenda mapema mwakani tukaanza uzalishaji na kuuza bidhaa zetu ndani na nje ya nchi hasa migodi ya Congo.
Ushuhuda huu umenianzishia siku vizuri sana. Wafanyabiashara wazawa tumieni fursa, tumieni wadau wanaofahamu sekta husika kupata taarifa sahihi. Malengo ya sheria #localcontent si kwa sekta ya Madini tu ni kwa sekta zote, tuchukue fursa
Ndimi mwenye furaha,
HS
Pamoja na Kushukuru akaniambia changamoto haziishi Kaka. Leo nina Containers 10 bandarini ila ukwasi ni shida bado
Nikamuambia hilo ni dogo, linazungumzika, ni suala la taasisi wezeshi kuingia.
Changamoto za ukwasi ni la kampuni nyingi na tunaangalia suluhu yake. Tutavuka
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.
