Moja kati ya njia bora ya #uwezeshajiwazawa yaani #localcontent ni ushirikishwaji na uwezeshwaji wa wafanyabiashara wa ndani. Nitaandika namna tuliwahi fanya katika safari ya uwezeshaji wazawa katika sekta ya madini hasa utoaji huduma kwenye migodi mikubwa hapa Tanzania
Mwaka 2014 kulikuwa na mradi mkubwa wa uzuiaji kutu 'corrosion control' kwenye matenki ya process plant ya mgodi. Manunuzi yalikuwa yafanyike kwa manunuzi ya moja kwa moja 'sole source' kwenda kwa mkandarasi wa nje ya nchi. Gharama za mradi zilikuwa zaidi ya dola milioni moja.
Wakati tunaanza hatua za majadiliano akabadilishwa Meneja Mkuu wa mgodi na huyu mpya alipoingia moja ya kitu aliona kinaweza badilishwa ni pamoja na utekelezaji wa mradi huu. Alikuwa na mawazo tofauti. Kwa wasifu yeye ni mbobezi wa sekta nje na ndani ya Tanzania
Meneja Mkuu mpya aliniita na kutaka nimpatie utaratibu na hatua tuliyofikia upande wa manunuzi na mkataba juu ya mradi. Nikiwa afisa mwandamizi nilikuwa na taarifa hizi.
Akaelekeza tutafute Wakandarasi Wazawa waoneshwe mradi na namna wanaweza kufanya.
Katika mchakato ule ilipatikana kampuni moja ambayo iliwahi kushiriki mradi kama huo mgodi mwingine lakini kama mkandarasi wa mdogo 'sub contractor'. Mkandarasi mkuu kwenye mradi huo ilikuwa kampuni ya nje na ndio hiyo ilikuwa ipate huu mradi mpya.
Tulipoongea na hii kampuni ya Kitanzania wao wakasema wanaweza kufanya kazi yaani 'services' part ya mradi ila kupata 'materials' itakuwa changamoto.
Tukawauliza je tukisema mgodi ununue 'materials' na wao wafanye kazi tu wanaweza? Wakajibu hilo inawezekana kabisa na watamudu
Tukawaomba wafanye ziara mgodini, wapitie maeneo yote yanayotakiwa kufanyiwa 'corrosion control' na kisha watoe gharama za kazi.
Kama sehemu ya kuwawezesha tukawaambia waanishe maeneo ambayo watahitaji msaada wa uwezeshaji ili tuone namna gani mpango utatekelezwa kwa usahihi
Tukaandaa ripoti na kumpatia Meneja Mkuu wa Mgodi. Kwa Wasifu huyu ni mmoja kati ya Wahandisi wa Madini waandamizi wazawa waliofanikiwa sana katika uwezeshaji wazawa na uchimbaji endelevu 'Sustainable Mining'. Nitaandika nyingine siku juu ya mwana huyu wa nchi.
Meneja Mkuu akaangalia ripoti kisha akauliza nini maoni yako Bwana Mnyama, alipenda kuniita Mnyama Mkali 😀😀. Nikamuambia nadhani tugawe mradi kwa sehemu mbili.
Moja ni manunuzi ya vifaa 'materials' na mbili upande wa ufanyaji kazi 'implementation/services'
Ila cha tatu ni lazima kuwa na mtu wa mwingine atakayesimamia utekelezaji yaani 'consultant' na pia timu ya ndani itakayofanya kazi kwa karibu na huyu Mkandarasi Mzawa.
Tukakubaliana yote na mikataba ikatengenezwa.
Mkataba wa kwanza ni wa manunuzi ya 'materials'ukaenda kwa kampuni ya nje ile ilikuwa ipate mradi wote awali
Mkataba wa pili ukawa ni 'Provision of Corrosion Control Services' huu ulipewa kwa kampuni ya kizawa
Na tatu ikaundwa timu ya ndani ya kusimamia mradi akiwemo GM.
Safari ya mradi ikaanza. Mradi ukakamilika kwa ufanisi mkubwa. Kubwa zaidi ulifanyika kwa ya 60% ya gharama ya awali.
Baada ya hapo shughuli za 'corrosion control' zikabaki historia kufanywa na wakandarasi toka nje. Wazawa walijenga uwezo na ikiwemo kuagiza 'materials' nje
Miaka minne baadae nikiwa mgodi mwingine kampuni ile ya Kizawa ya 2014 ilipata zabuni nyingine kubwa ya kujenga 'CIL TANK' kwa watu wa migodi wataelewa hili. Mchakato wake nitaandika siku nyingine.
Swali langu litakuwa je kampuni ile ya Kizawa bado wanaendelea kukua?
Nihitimishe kwa kusema ili kuwa na uwezeshaji wazawa wenye kutoa matokeo ni muhimu uwepo ushirikishwaji wenye nia na tija.
Kampuni za kizawa ziwe na uwezo wa kujifunza na kujiendeleza
Viongozi wa kampuni za madini wawe tayari kutoa fursa.
Wadau wote wafanye kwa nafasi zao.
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.
