Nimeona bora niongee na kuomba ushauri wenu kwani nimekaa kimya siku nyingi. Hali inazidi kuwa mbaya. Nazidi kudhoofika kisaikolojia na imefikia hatua Kuna mawazo mabaya yananijia kichwani.
Ni hivi, nilikua na biashara zangu kama tatu hivi nilizokua naziendesha zikiwa eneo moja. Kwa kuwa mimi ni mwalimu wa shule binafsi (private school) muda mwingi nashinda kazini, Hivyo msimamizi mkuu wa biashara zangu alikuwa mke wangu.
Mwezi wa 7 wakati wa likizo ya Corona mke wangu alisafiri kwenda nyumbani kusalimia.
Nikawa nasimamia mimi mwenyewe.
Shule zikafunguliwa huku mke wangu akiwa bado hajarudi.
Hapo ndipo hali ilianza kuwa tofauti.
Wafanyakazi wakaamua kutumia hiyo nafasi kuniumiza kwa kushirikiana na mtu wangu wa karibu, ambaye kwangu alikuwa kama ndugu na rafiki.
Aliwashawishi wafanyakazi wangu pasipo mimi kujua.
Kwanza ikatokea hasara kubwa, hadi biashara ikayumba, kisha kwa pamoja wakaomba wote kuacha kazi. Kabla sijajua cha kufanya nikamwambia mke wangu awahi kurudi.
Kwa huo muda nikaamua nifunge ili kumngoja mke wangu.
Gafla nikapokea simu kutoka kwa mwenye fremu akisema anataka abadilishie matumizi ya sehemu hiyo hivyo natakiwa nihamishe biashara zangu na atanilipa gharama zangu za usumbufu.
Nikaamua kutoa vitu vyangu, kumbe yule jamaa yangu kanizunguka.
Niliporudi kufuatilia gharama zangu, nikamkuta nae kafungua biashara Kama zile zangu, na wafanyakazi wangu wote amewaajiri.
Sikufanya chochote, kumbe walishirikiana na mwenye fremu pia.
Sasa kibaya kabisa kinachoniuma, nilitoka kuchukua mkopo mwezi wa tano, nikaiweka kwenye biashara. Na sasa biashara imesimama.
Nilijipa muda sana wa kutomshirikisha mtu hiki kitu, ila sasa nimeona nashindwa kulihimili, akili yangu sasa hivi siielewi, inanipa mawazo mabaya.
Nifanye nini? nianzie wapi? kila mahesabu nayopiga yanakataa, nalipaje mkopo? kila nikifikilia kichwa kinauma kwa mawazo. Kahama.
#WatuNiStory
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.
