1/10 “Naitwa William Adam Lukoo ,mzaliwa wa mkoa wa Morogoro. Mwaka 2003 familia yetu ilihamia jijini Tanga kwa ajili ya harakati za kimaisha. Haikua rahis kwa sababu ya ugeni lakini wazazi walipambana kuhakikisha napata elimu bora. Licha ya kutoka kwenye familia ya kimaskini...
2/10 ..nilihakikisha nafanya vizuri kwenye masomo kiasi cha kuwavutia walimu na kujizolea umaarufu shuleni. Nilifanikiwa kuhitimu mwaka 2010 shule ya msingi Majani Mapana wilayani Tanga mjini. Mwaka 2011 nilianza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Usagara..
3/10 ..lakini kutokana na ugumu wa maisha, wazazi wangu wote hawakuwa na kazi. Ikawalazimu kufikia hatua ya kuuza vitu vya ndani ili kuweza kunilipia ada. Maisha yalikuwa magumu mno nyumbani kiasi cha kufikia hatua ya kushindwa kupata chakula na kodi.
4/10 ..Lakini Mungu hamtupi mja wake mimi niliendelea kupambana kwenye masomo yangu na kuendelea kufanya vizuri sana. Na bahati nzuri wazazi wakapata kazi zingine tena japo majukumu yalikua mengi mno.
5/10 .. Mwaka 2014 nikachelewa kulipa ada ya mtihani wa kidato cha 4 ikapelekea matokeo yangu kufungiwa. Nilihuzunika sana. Ikabidi kupambana kupata ile pesa matokeo yakafunguliwa na nilifanya vizuri nikajiunga na kidato cha 5 shule ya sekondari Nachingwea mkoani Lindi.
6/10 ..Nilipambana sana kuhakikisha ndoto zangu zinakuwa kweli ,tulishirikiana na wanafunzi wenzangu kusoma kwa bidii na juhudi zilizaa matunda kwa kufanikiwa kufaulu vizuri..
7/10 ...na Mimi nilipata nafasi ya kujiunga chuo kikuu Cha Dar es Salaam (2017-2020) kwa ajili ya masomo ya shahada ya elimu na Mungu mwema mwaka huu nimehitimu masomo yangu.
Ushauri wangu kwa vijana wasikate tamaa na wala wasikatishwe tamaa na hali za maisha za familia zao bali wachukulie kama fursa ya wao kuongeza nguvu katika mapambano ya kufanikisha ndoto zao ili ziwe kweli na waokoe familia zao kutoka kwenye umasikini.” #WatuNiStory
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.
