Habibu B. Anga Profile picture
Author| To Infinity and Beyond

Mar 22, 2021, 20 tweets

JIHADI JOHN: MCHINJAJI WA ISIS MIKONONI MWA WANAUSALAMA WA TANZANIA

PART 4 (HITIMISHO)

Kwa hiyo wakafanya uchambuzi wote ule kuunda "profile" ya mtu wanayemtafuta.
Kisha wakachukua hii profile na kuoanisha na orodha ya watu ambao kwa muda mrefu MI5 wamekuwa wanawashuku...

kujihusisha na mavuguvugu ya kigaidi.
Yaani wanaangalia kwamba kwenye watu ambao siku za nyuma wamekuwa wakiwalia rada pale London, ni nani ambaye ana-fit kwenye hii profile waliyotengeneza kuhusu yule mchinjaji wa ISIS anayeitikisa dunia.

Baada ya kufanya uoanishaji huu..

wakafikia conclusion kwamba mchinjaji wa ISIS ambaye alikuwa anaitikisa dunia alikuwa ni mtu anayeitwa Abdel Bary
Huyu Abdel alikuwa ni maarufu sana hapo London, kwa sababu alikuwa ni mwanamuziki wa Hip-hop anayechipukia kwa kasi sana akitumia jinan kisanii "L Jinny"

Hata kwenye

mtandao wa Youtube video zake za muziki zilikuwa zinapata mamilioni ya views.

Lakini mwishoni mwa mwaka 2012, Abdel Bary akapotea kusikojulikana na taarifa za kishushushu zilikuwa zinaonyesha kwamba alikwenda nchini Syria kujiunga na kikundi cha Daesh.

Ilikuwa ni almanusura..

serikali za Uingereza na Marekani watangaze kwa ulimwengu identity ya yule 'chinja chinja' anayejifunika manguo meusi kwamba ni Abdel Bary, lakini wakapata 'clue' mpya ambayo ikawafanya watafakari upya kama kweli Abdel ndiye yule mchinjaji.

Kuna baadhi ya watu waliochukuliwa...

mateka na ISIS walikuwa wameokolewa.

Mateka hao walitoa intelijensia muhimu sana.
Walisema kwamba mateka wote wa kimagharibi waliotekwa na ISIS kwenye jela yao walikuwa wanalindwa na wapiganaji wa ISIS wanne ambao wote wanaongea kingereza chenye lafudhi ya Uingereza...

Mateka hao wakawabatiza jina wapiganaji hao wanne wa ISIS na walikuwa wanawaita "The Beatles" (kikundi maarufu cha muziki toka Uingereza kilichotamba mno miaka ya sitini).

Kwa hivyo mateka waliwabatiza majina wapiganaji hao wa ISIS kila mmoja walimpa jina la mwanakikundi cha...

The Beatles (John, Paul, George na Ringo).

Mateka hao wakaeleza kwamba yule somo mchinjaji anayeonekana kwenye video mateka walikuwa wanamuita "John".

(Ndipo hapo vyombo vya habari wakalidaka jina hilo na kuliboresha kumuita yule mchinjaji "Jihadi John")

Mateka wale pia...

wakatoa clue muhimu sana ambayo ndio ilifanya serikali za Uingereza na Marekani wahisi Jihadi John hakuwa Abdel Bary kama walivyodhani.

Mateka walisema kwamba, yule mchinjaji, Jihadi John licha ya kwamba alikuwa mpiganaji wa ISIS lakini alikuwa na 'obsession' kubwa na Al-Shabaab

Alikuwa mara nyingi akiwalazimisha mateka kutazama video za Al-Shabaab. Alikuwa mara kadhaa akiwasimulia mikiki mikiki ya Al-Shabaab.

Sasa, kwa intelijensia ambayo MI5 walikuwa wanayo ilikuwa haionyeshi kwa namna yeyote kama Abdel Bary alikuwa na mahaba hayo mazito na Al-Shabaab

Bali yuko mtu mwingine waliyewahi kumlia rada, tena mkazi wa London, ambaye si tu kwamba alikuwa na mahaba na Al-Shabaab bali aliwahi kujaribu kabisa kujiunga nao. Lakini kwa kushirikiana na idara ya ujasusi ya Tanzania wakatibua mpango huo.

Umeshamjua.?

Naam, Mohammed Emwazi.

Mohammed Emwazi ndiye alikuwa ana-fit hii profile ya kuwa na obsession na Al-Shabaab.

Wakachukua taarifa za kimo cha Emwazi, Kilo, mjengeko wa mwili, tone ya ngozi.. kila kitu kilikuwa kinamatch profile waliyoitengeneza awali.

Hawakuishia hapo. Wakachukua sauti za hotuba ambazo

mchinjaji huwa anazitoa kabla ya kuchinja wale mateka wake. Wakazichuja vyema hizo audio kisha wakamwita mama yake Emwazi asikilize. Mama Mohammed Emwazi aka-confirm kwamba hiyo ni sauti ya mwanaye Mohammed.

Kwa hiyo, sasa kwa 100% walikuwa wameng'amua yule mchinjaji alikuwa ni

Mohammed Emwazi.

Emwazi ambaye miaka kadhaa nyuma tu tulimsekwa selo pale kituo cha Polisi Stakishari Ukonga.
Emwazi ambaye alituomba karibia alie machozi tumruhusu aingie nchini Tanzania.

Kumbe.. kumbe..

Kumbe kama tungelimuacha siku ile aingie nchini, kisha akafanikiwa...

kwenda Somalia kujiunga na Al-Shabaab. Ule ubunifu wake wa kikatili wa kuchinja watu angekuwa anaufanya hapa Afrika.. angekuwa anawakata shingo wanajeshi wetu. Angekuwa anautetemesha ulimwengu kutokea hapa tu sebuleni kwetu.. Somalia.

Kwa umombo twasema "..we dodged a bullet.."

Baada ya CIA, MI6 na Mossad kumtambua yule mchinjaji kuwa ni Mohammed Emwazi wakaanza sasa kukusanya intelijesia kumuhusu.

Wakaanza kutazama 'topography' na landscape ya maeneo anayochinjia watu na kuoanisha na mwenendo wa vikosi vya ISIS ardhini.

Wakakusanya intelijensia ya...

Kutosha kwa mwaka mzima mpaka wakaja kujua mahala gani ambapo atakuwa kwenye siku fulani mahususi.

Pasipokujua kwamba CIA wamekwisha hesabu hatua zake na wamejua nyendo zake, siku hiyo Jihadi John na msafara wake walikuwa kwenye mji wa Raqqa nchini Syaria.

Jihadi John akiwa..

anatoka kwenye nyumba aliyofikia kuingia kwenye gari iliyokuwa inamsubiri nje.. Drone ya jeshi la Marekani ikafyatua kombora na kusambaratisha gari, Jihadi John na watu wote waliokuwepo kwenye msafara

Hiyo ilikuwa ni siku ya tarehe 12 November 2015.

Kesho yake, Pentagon wakatoa

taarifa kwa vyombo vya habari juu ya shambulio la mafanikio la kumuua Jihadi John. Mchinjaji wa ISIS aliyeutikisa ulimwengu na kupanda hofu kwa kila mtu ulimwenguni.
Jitu la maguo meusi ambaye aligeuka kufanyika kama nembo ya ISIS na ukatili.

Miezi miwili baadae ISIS kupitia..

jarida lao la Dabiq walitoa taarifa juu ya kifo cha Mohammed Emwazi na kwa mara ya kwanza wakaweka picha yake sura ikiwa wazi na amevalia mavazi nadhifu.

Na huo ndio ulikuwa mwisho wa Jihadi John Mchinjaji.

Tukutane tena kwenye simulizi nyingine hapa hapa.

- Habibu B. Anga

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling