Habibu B. Anga Profile picture
Author
7 subscribers
May 15 25 tweets 6 min read
TISS| MAPINDUZI| MTIHANI MKUU WA KIKWETE

Mwaka wa mwisho wa utawala wa Kikwete ulikuwa ni mgumu kuliko umma unavyofahamu.

Alikuwa anapambana na mpasuko ndani ya chama, kushamiri kwa upinzani… lakini zito zaidi ilikuwa ni changamoto iliyotokea siku ya 13 May 2015.

Thread… Image Hii picha hapa chini ni picha halisi ikimuonyesha Mkurugenzi wa Idara ya Ujasusi Tanzania kipindi kile Bw. Othman Rashid akifanya suala ambalo si la kawaida na hatukuwahi kuliona hapo kabla kwa Mkurugenzi Mkuu wa TISS kufanya jukumu la ‘VIP Protection’

(Niliyemzungushia duara) Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa - TISS, akiongoza msafara wa wa Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza toka Hoteli ya Serena, Dar es Salaam
Mar 25, 2023 24 tweets 6 min read
Ukitaka kuelewa chanzo cha vita ya Ukraine basi unapaswa kufahamu mkasa wa huyu unaye muona pichani na Zitto… anaitwa Victor Yushchenko

Miaka kadhaa iliyopita huyu somo alikumbwa na kadhia ya kulishwa sumu na kupata madhara kama yale ambayo yalimkuta Dr. Mwakyembe..

Thread.. enzi zile za Richmond na Dowans mpaka akapelekwa India kutibiwa.
Ngozi ya mwili yote iliharibika na kuanza kupukutika kama unga

Huyu Yuschenko yeye kadhia hii ilimtokea mwaka 2004 kipindi hicho akiwa anagombea Urais wa Ukraine
Yushchenko alikuwa anachuana mwanasiasa Yanukovych..
Aug 18, 2022 23 tweets 5 min read
Roman Abramovich: Utajiri wa Damu Mpaka Kumuingiza Ikulu Putin

Thread,

Namna ambavyo mtoto yatima aliyelelewa katka umaskini ameweza kuibuka moja ya binadamu wenye ukwasi mkubwa duniani na mpaka kuweza kumuingiza Ikulu Vladmir Putin ni mkasa wa aina yake…

(Usisahu ku-Retweet) Image Wazazi wake wote wawili licha ya kuishi maisha yao yote nchini Russian lakini asili yao ni Waisrael. Mama yake aliitwa Irina na alifariki kipindi Roman bado angali mchanga kabisa wakati baba yake ambaye aliitwa Arkady alifariki kwa ajali ya gari miaka michache baadae Roman akiwa
Dec 21, 2021 43 tweets 11 min read
TUMEWAHI KUWA NA CHANJO KWA MALENGO YA KISHUSHUSHU

Thread..

Kadiri ulimwengu unavyobadilika, stadi ya Ujasusi inazidi kuwa complex kwa kuhusisha mbinu ambazo nyingine ukizisikia unaweza kudhani labda watazama sinema au waota, lakini ndio uhalisia wa ulimwengu ulipo sasa katika katika juhudi za mataifa na makampuni makubwa kupanua ushawishi wao juu ya dunia yote na kulinda maslahi.

Kuna kisa cha tofauti sana ningependa nikijadili leo hii. Kisa cha tofauti kabisa..

Wengi tutakuwa tumewahi kusikia shirika linaloitwa “Save the Children”. Ni moja ya…
Oct 14, 2021 98 tweets 25 min read
𝗕𝗜𝗡𝗧𝗜 𝗝𝗔𝗦𝗨𝗦𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗜𝗔𝗞𝗔 25 𝗔𝗡𝗔𝗬𝗘𝗜𝗧𝗜𝗞𝗜𝗦𝗔 𝗔𝗙𝗥𝗜𝗞𝗔 𝗠𝗔𝗦𝗛𝗔𝗥𝗜𝗞𝗜

Thread..

Siku ya 30 May 2019, maafisa Usalama Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JKIA, Nairobi walimuweka kizuizini abiria mmoja mwenye hati ya kusafiria ya kidiplomasia, mwanaume.. Image wa asili ya kisomali. Japokuwa watu wenye diplomatic passport wapata exemptions kadhaa kwenye kaguzi za uwanja wa ndege, lakini ilikuwa ni lazima kwa maafisa hawa kumuhoji abiria huyu kutokana na utata wa mzigo ambao alikuwa nao.

Huyu somo alikuwa na briefcase ambalo ndani yake
Sep 4, 2021 41 tweets 10 min read
𝗞𝗔𝗕𝗟𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗞𝗨𝗟𝗨.. 𝗞𝗪𝗔𝗡𝗭𝗔 𝗔𝗗𝗛𝗔𝗕𝗨 𝗬𝗔 𝗞𝗜𝗙𝗢

Thread..

Ukiwa unatoka Lusaka kwenda Jimbo la Magharibi, kabla hujaingia mji wa Mongu kuna kipande cha barabara kinajulikana kama Limulunga Road.
Kipande hiki cha barabara mwaka juzi kimetupa tukio la kipekee Image ambalo kwa kiwango kikubwa tukio hili limebadili mwelekeo wa siasa la bara zima la Afrika na hasa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

Pengine pasipo tukio hili huyu Hichilema tunayemuona leo asingelikuwa Rais. Lilikuwa tukio la kipekee kabisa..

Kila mwaka pale Zambia huwa wana
Aug 10, 2021 25 tweets 6 min read
𝗨𝗧𝗔𝗝𝗜𝗥𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗦𝗛𝗔𝗞𝗔 𝗪𝗔 𝗪𝗔𝗟𝗜𝗡𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗩𝗜𝗢𝗡𝗚𝗢𝗭𝗜

Thread..

Mwaka juzi kwenye hafla ya mapokezi ya ndege kwenye nchi fulani hivi hapa Afrika Mashariki kuna incident ndogo tu ilitokea lakini wengi ikatufikirisha sana.

Dakika chache baada ya Rais wa... nchi hiyo kumaliza kuongoza hafla hiyo ya mapokezi ya ndege akashuka jukwaani na akianza kuandoka.
Lakini kabla hajakwenda kupanda gari, kama ambavyo ilikuwa ada kwa Rais yule akaelekea upande waliokaa wananchi wake na ili awasalimie.
Na kusalimia huku akaanza jukwaa ambalo...
Jul 20, 2021 25 tweets 7 min read
UZI
👇👇

Tujadili kidogo Executive Protection.
Hapa chini nimeweka picha za inner cycle za ulinzi wa Rais JPM, Samia, Ndayishimiye (Burundi) na Mnangagwa (Zim).

Kwa kila Rais utaona 'First Ring' zao (hao walinzi wanaomzunguka Rais muda wote) lazima kuna afisa mmoja au wawili.. amebeba begi la mkononi

Umewahi kujiuliza hilo begi lina dhumuni gani.?

Hiyo picha hapo juu, JPM alikuwa chato na hapo alikuwa anakwenda kwenye kibanda cha simu kusajili line yake kwa alama ya vidole
Kwa hiyo hakuwa kwenye ziara au anakwenda kikaoni.. sasa hilo begi ni la nini?
Jul 17, 2021 25 tweets 5 min read
𝗡𝗔𝗡𝗜 𝗔𝗟𝗜𝗠𝗧𝗘𝗞𝗔 𝗠𝗧𝗢𝗧𝗢 𝗪𝗔 𝗥𝗔𝗜𝗦, 𝗠𝗔𝗭𝗜𝗠𝗕𝗨, 𝗠𝗢𝗥𝗢𝗚𝗢𝗥𝗢.?

FINALE

Naam, niwamalizie sasa hiki kisa. Kama haujasoma sehemu ya kwanza, angalia kwenye profile yangu juu kabisa pinned tweet.

Sasa,

Wale wakimbizi waliorejea SA, tokea hapa Morogoro... wakaeleza namna ambavyo waliishi kambini Mazimbu na kijana anayeitwa Louis Mathakoe ambaye sasa hivi wanaonyeshwa picha kwamba identity halisi kijana huyo ni mtoto wa Rais Mbeki.

Wajumbe wa Tume ya TRC walivyo endelea kuhoji kuhusu nyendo za kijana Kwanda akiwa hapo Mazimbu..
Jul 16, 2021 25 tweets 5 min read
𝗡𝗔𝗡𝗜 𝗔𝗟𝗜𝗠𝗧𝗘𝗞𝗔 𝗠𝗧𝗢𝗧𝗢 𝗪𝗔 𝗥𝗔𝗜𝗦, 𝗠𝗔𝗭𝗜𝗠𝗕𝗨, 𝗠𝗢𝗥𝗢𝗚𝗢𝗥𝗢.?

Kuna masuala huwa yanakuwa salama yakiachwa bila kuzungumzwa. Sababu ukianza kuhoji kuhusu ukweli na undani wake, unajikuta unafungua mlango wa hatari ambazo pengine hauko tayari kuzikabili... Mojawapo ya masuala haya ni madhira ambayo yanafanywa na watu tuliowapa madaraka. Nyendo zao, na siri zao ni kana kwamba haupaswi kutamani kuzifahamu.

Lakini binadamu tumeumbwa na kiu ya kutaka kujua, na kiu hii ni kama upele, hauachi kuwasha mpaka uukune
Na pia historia ya nchi
Jul 15, 2021 19 tweets 4 min read
𝗠𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 #1: 𝗝𝗔𝗦𝗨𝗦𝗜 𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗞𝗢𝗗𝗜, 𝗨𝗝𝗔𝗦𝗨𝗦𝗜 𝗪𝗔 𝗕𝗜𝗔𝗦𝗛𝗔𝗥𝗔

#7

Majukumu wakuu, mniwie radhi.

Tuendelee,

Mara ya mwisho nilisema, kuna Mtanzania ambaye mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu alidai kwamba alinyang'anywa passport na Idara ya Intelijensia Image na kisha kupewa Hati ya Kusafiria ya nchi ya Afrika Kusini

Nikaeleza kwamba mtu huyu ambaye alikwenda Afrika Kusini kutafuta maisha mwanzoni mwa miaka ya tisini, mojawapo ya harakati zake kubwa za kwanza ni pale alipomshawishi Nelson Mandela na taasisi yake ya Mandela Foundation
May 25, 2021 9 tweets 2 min read
𝐌𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 #1: 𝐉𝐀𝐒𝐔𝐒𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐊𝐎𝐃𝐈, 𝐔𝐉𝐀𝐒𝐔𝐒𝐈 𝐖𝐀 𝐁𝐈𝐀𝐒𝐇𝐀𝐑𝐀

#6

Nikasema kwamba kwenye ule mchoro wa Motto Mabanga aliowapa vigogo wetu. Sehemu ya mchoro huu ilikuwa ni kuchukua mkopo wa karibia shilingi bilioni 60 toka taasisi ya African Global.. Image Capital.

Hapa tafadhali soma kwa makini sana,

Yule Walter Hennig niliyewaeleza jana mwenye kuandaa sherehe za mwaka mpya pale Clifton, Cape Town.. huyu bwana ni CEO wa kampuni inaitwa African Management Limited.

Sasa hawa African Management Limited ndio wanaomiliki taasisi ya
May 24, 2021 22 tweets 5 min read
𝐌𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 #1: 𝐉𝐀𝐒𝐔𝐒𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐊𝐎𝐃𝐈, 𝐔𝐉𝐀𝐒𝐔𝐒𝐈 𝐖𝐀 𝐁𝐈𝐀𝐒𝐇𝐀𝐑𝐀

#5

Mara ya mwisho nikaeleza namna ambavyo Motto Mabanga aliwakutanisha Mwanasiasa wa South Africa, Tokyo Sexwale na mtaalamu wa jiolojia Dr. Alan Stein na Swahiba wake Jonathan Taylor.. Image na hatimaye kuunda kampuni ya Ophir Energy Plc.

Nikaeleza kwamba Motto Mabanga alipewa kamisheni ya 5% ya umiliki wa kila kitalu ambacho atafanikiwa kuwapatia Ophit Energy kwa mkataba mnono.

Na Motto Mabanga alipoingia kazini, target yake ya kwanza ya vitalu ilikuwa ni Tanzania
May 10, 2021 23 tweets 5 min read
𝗠𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 #1: 𝗝𝗔𝗦𝗨𝗦𝗜 𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗞𝗢𝗗𝗜, 𝗨𝗝𝗔𝗦𝗨𝗦𝗜 𝗪𝗔 𝗕𝗜𝗔𝗦𝗛𝗔𝗥𝗔

#4

Mara ya mwisho nikasema kwamba minada yetu yote ya vitalu vya mafuta ilidoda. 1st, 2nd na 4th Round.
Mwaka 2005 pekee kwenye 3rd Round kutokana na uhusika wa Motto Mabanga ndipo mnada Image Ule mpaka leo umeweka rekodi ya vitalu vyote 7 kuchukulia na PSA Agreement kusainia kati ya serikali na wawekezaji.

Sasa ni namna gani ambavyo Motto Mabanga alisuka mipango kufanya mnada wetu uchangamke, ndipo hapo sasa nikaanza kueleza.

Kwanza kwa kifupi sana niseme kwa nini..
May 1, 2021 26 tweets 5 min read
𝗠𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 #1: 𝗝𝗔𝗦𝗨𝗦𝗜 𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗞𝗢𝗗𝗜, 𝗝𝗔𝗦𝗨𝗦𝗜 𝗪𝗔 𝗕𝗜𝗔𝗦𝗛𝗔𝗥𝗔

PART 3

Wakuu, mnisamehe bure, majukumu yalibana mno. Niko na muda wa kutosha sasa.
Nitaweka Parts kadhaa mfululizo kuwafidia uraibu niliowaachia muda wote huu.

Tuendelee

Mara ya mwisho Image Nilieleza kuhusu mgogoro ambao ulitokea pale Vodacom Congo.
Ambapo Vodacom Group walikuwa wameingia ubia na kampuni ya Congolese Wireless Network kuunda kampuni ya Vodacom Congo ambapo kwenye ubia huo Vodacom Group walikuwa na 51% ya umiliki huku CWN wakiwa na 49%.

Lakini baada,
Apr 11, 2021 25 tweets 5 min read
MTANZANIA #1: JASUSI WA KUKODI, UJASUSI WA BIASHARA

Thread..

Si rahisi kuwa mahususi sana ni mwaka gani, lakini tunakadiria kwamba katikati ya miaka ya tisini hivi Mtanzania ambaye kwa sasa nimtaje kwa jina lake moja tu la Matiko aliondoka jiji Dar kwenda nchini Afrika Kusini Image Kwa ajili ya kutafuta maisha. Lakini tofauti na Watanzania wengi wanaozamia SA ambako wakifika uanza kwa kufanya shughuli za hali ya chini, ilikuwa tofauti kabisa na bwana Matiko ambaye aliingia SA akiwa na mtaji wa kuridhisha kutokana na fedha ambazo alizipata toka kwenye mauzo
Apr 5, 2021 18 tweets 4 min read
Kuna uzi niliandika hapa Mwezi March kuhusu dhana nzima ya Ulinzi wa viongozi wa juu.
Nikasisitiza sana kwamba sula la ulinzi wao sio tu kulinda wasidhuriwe kimwili bali pia kulinda hadhi zao, heshima zao na siri zao.

Kitimbwi ambacho kimetokea leo cha Rais wa nchi

Thread👇👇 Image Kuteua na kufukuza Mkurugenzi wa TPDC ndani ya masaa machache kabisa... ni failure kubwa ya kitengo cha intelijensia ya nchi ambao wana jukumu la kulinda hadhi na heshima ya Rais.
Mtu yule aliyeteuliwa huku akionekana kwamba hana sifa kabisa ya kushika wadhifa ule, ina reflect..
Apr 2, 2021 5 tweets 1 min read
Mkuu @abuu_adam anauliza nini ilikuwa hatma ya yule "Mtanzania" Al-Asad aliyekuwa anashikiliwa kwenye black site ya CIA hapo Djibouti?

Jibu: CIA baada ya kumaliza kumuhoji na Asad kutoa siri zote anazozijua, wakataka kumrudisha hapa nchini, lakini tukamkataa kwa sababu hakuwa.. raia halali wa nchi hii bali alikuwa akiishi hapa kwa nyaraka za kugushi.

Kwa hiyo CIA wakamdeport al-Asad kwenda nchini Yemen.

Huko vyombo vya usalama wakamshikilia kwa miezi michache na kisha kumuachia huru mwaka 2005.

Baada ya kuachiwa huru al-Asad alitumia muda wake wote..
Apr 2, 2021 11 tweets 3 min read
"ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA"

Nyongeza...

Mwanzoni mwa makala kabisa nilieleza kuhusu wale vijana watatu ambao walikuwa wanasafiri toka Afgooye kwa gari kuelekea Mogadishu na njiani wakakutana na check point ya jeshi na baadae kumiminiwa risasi.

Nikasema kijana mmoja Image Fouad (yule msomali aliyekaa siti ya nyuma) kwa mujibu wa CIA wanasema kwamba alifanikiwa "kutoroka" akiwa hai.

Sasa,

Kuna vitu viwili hapo nivieleza kwa haraka haraka.

Jambo la Kwanza; kama ambavyo ilikuwa kule Kenya ambavyo waliunda Renditions Operations Team ndivyo hivyo...
Apr 2, 2021 25 tweets 6 min read
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

PART 5 (HITIMISHO)

Nikiwa nahitimisha ni vyema kusisitiza kwamba, kikosi hiki cha makomando wa Kenya ambacho kinaendeshwa kwa amri ya CIA na NIS (Idara ya Ujasusi Kenya) kwa sasa kimegawanywa kwenye vitengo viwili.. Image Kitengo cha kwanza ndio ile Rendition Operations Team; hawa wanahusika sana kama target anatakiwa kukamatwa akiwa hai

Alafu siku hizi kuna RRT (Rapid Response Team) hawa wanatumika zaidi kama target anatakiwa kuwaneutralized (kuuwawa) au kuhusika kuokoa mateka kama watekaji wana
Apr 1, 2021 16 tweets 4 min read
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

PART 4

Ile taarifa ambayo Asad aliwapatia ilikuwa ya maana sana kwa CIA.

Mpaka muda huu ambapo Asad alikuwa anahojiwa (kumbuka hiyo ni mwaka Oct 2003) huyo "bwana somba" Odeh tayari alikuwa ameshakamatwa Image na yuko gerezani Guatanamo Bay (alikamatwa tangu mwaka 1998).

Taarifa hii ya Asad iliwapa CIA kitu kimoja muhimu sana.. walithibitisha intelijensia yao kuhusu shirika la al-Haramain kutumiwa na al-Qaida kusambaza fedha ulimwenguni kwa watu wao.
Ushahidi huu ulitumiwa na Marekani