ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI
Thread..
Kwa sasa, eneo letu la Afrika Mashariki limeguka kuwa moja ya eneo muhimu sana la kimkakati kiulinzi kwa nchi ya Marekani.
Leo nataka nikusimulie mkasa halisi wa namna gani shirika la Ujasusi la Marekani...
CIA linaendesha shughuli zake kuanzia hapa nchini kwetu Tanzania pamoja na nchi zote zingine za Afrika Mashariki.
Nataka nikusimulie mkasa wa kusisimua ili tuelewe vyema namna gani Afrika Mashariki kwa sasa imegeuka uwanja wa ushushushu wa Kimataifa kati ya Marekani na adui zake.
Ukimaliza kusoma uzi huu, utaelewa kwa nini sio kila "mtalii" umuonae ni mtalii tu kaja kushangaa swala pale Mikumi
Namna hii,
Siku fulani hivi ya tarehe 7 mwezi June mwaka 2011, kuna vijana watatu walikuwa wanasafiri kwa gari binafsi toka pwani ya Somalia kwenye mji unaitwa...
Afgooye wakiwa kwenye barabara ambayo inaelekea mji mkuu wa Mogadishu.
Vijana hawa watatu ndani ya ile gari wote walikuwa wote wanazungumza lugha ya kiswahili.
Lakini ukikisikiliza kiswahili chao utagundua kwamba mmoja anazungumza kiswahili chenye lafudhi ya Kenya, yule mwingine
anazungumza kiswahili aina ya Shikomori ambacho chazungumzwa sana kwenye visiwa vya Comoro. Na yule kijana wa tatu ambaye yeye alikaa siti ya nyuma alikuwa anazungumza Kiswahili chenye lafudhi ya Kisomali.
Vijana hao watatu majina yao ni Abu Aish(ndio mwenye kuzungumza Kiswahili
chenye asili ya Comoro), Abdullahi Dere (mwenye kuzungumza Kiswahili cha lafudhi ya Kenya) na yule ambaye alikaa siti ya nyuma mpaka sasa ametambulika kwa jina moja tu la Fouad.
Mji huu wa Afgooye ambao walikuwa wanatoka uko eneo la pwani kabisa ya Somalia.
Ndani ya ile gari..
waliyokuwa wanasafiria, pamoja nao kulikuwa na vitu ambavyo havikuwa vya kawaida.
Kwanza walikuwa wana begi limejaa fedha taslimu kiasi cha dola za Kimarekani 40,000.
Pia walikuwa na boksi limejaa madawa mbalimbali ya binadamu. Pia walikuwa na takribani simu 15 za mkononi na..
kompyuta mpakato zipatazo tatu
Muda mchache uliopita Abu Aish na Abdullahi Dere walikuwa wamewasili pwani ya Afgooye kwa boti ndogo wakitokea Mombasa na kupokelewa na yule ambaye muda huu alikuwa amekaa kwenye siti ya nyuma
Walikuwa wanapiga soga na kucheka huku wakiendesha gar
yao aina ya Toyota Mark II iliyochoka kiasi chake kuifuata barabara iendayo Mogadishu.
Hii ilikuwa yapata majira ya saa tano za usiku.
Wakiwa kilometa chache tu mahala fulani nyikani kabla ya kuingia Mogadishu wakashangaa kuona mbele yao kulikuwa na kizuizi cha ukaguzi cha jeshi
ilikuwa ni ajabu sababu siku moja tu iliyopita, Fouad alikuwa amepita njia hii hii na hakukuwa na Millitary Check Point.
Na kimsingi walikuwa wamechagua njia hii ya vumbi ya ndani ndani na kutopita barabara kuu ili kuepuka jambo hilo la vizuizi vya ukaguzi.
Lakini kwa ajabu..
kabisa mbele yao kulikuwa na gari mbili za kijeshi aina ya Humvee na nje ya gari hizo za kijeshi kulikuwa na maafisa wa jeshi wapatao nane.
Wanajeshi hao wote walikuwa wamevalia sare za jeshi la Somalia isipokuwa mtu mmoja tu kati yao ambaye alikuwa amevalia kiraia.
Na sio tu..
kwamba alikuwa anatofautiana na wale wengine kwa kuvaa kiraia, bali pia mtu huyu alikuwa ni mzungu si Msomali.
Alikuwa amevalia buti nzito, suluari ya jinzi, shati ya drafti ambayo juu yake alikuwa ameivalia bullet proof vest na mkononi akiwa amebeba silaha nzito ya kivita....
Abu Aish na wenzake hawakuwa manjuka kwenye masuala ya kiusalama, walielewa huyu mtu aliyevalia kiraia alikuwa ni nani?
Walifahamu fika kwamba mtu huyu eidha alikuwa ni afisa wa jeshi la Marekani au alikuwa ni afisa wa CIA.
Ukweli huu uliwashitua moyo.
Kwamba hiki kizuizi ni cha
kawaida tu au ni wao hasa walikuwa wanasubiriwa hapo.
Moja ya maafisa jeshi la Somalia akafuata mpaka pale walipo na kuwasalimu, kisha akawauliza majina yao.
Baada ya kutaja majina yao kila mmoja, yule afisa wa jeshi akawaomba wawashe taa ndani ya gari maana walikuwa wameizima..
Abu Aish ambaye alikuwa ndiye dereva akawasha taa za ndani ya gari. Lakini akawasha kihuni sana. Yaani aliwasha kwa muda wa kama sekunde tano hivi alafu akazizima.
Yule mwanajeshi wa Somalia akawaambia awashe tena hajawaona vyema
Abu Aish akawasha tena kihuni vile vile, akawasha
kwa sekunde kama tano hivi kisha akazima tena.
Yule mwanajeshi Somalia akakasirika haswa.
Kwa hasira akawaamuru wote washuke kwenye gari.
Abu Aish na wenzake wakiwa wanashuka kwenye gari, ghafla tu Abdullahi Dere sijui ni kwa namna gani ya haraka akatoa bastola kiunoni mwake..
kwa kasi ya ajabu na kummiminia risasi yule mwanajeshi aliyekuwa anawakagua.
Wanajeshi wengine wale ambao walikuwa pembeni ya Humvee wakajibu mapigo kwa kuwamiminia risasi akina Abu Aish na wenzake.
Isipokuwa yule Fouad aliyekaa siti ya nyuma ripoti ya jeshi la Somalia inadai..
kwamba alifanikiwa kutoroka (hapo mbele tutaona kwa nini hawakumuua na walisema "alikimbia").
Baada ya wanajeshi wa Somalia kuwamiminia risasi na kuwaua Abu Aish na mwenzake, wakaanza kupekua gari yao.
Ndani ya gari ndio wakakuta vile vitu... begi limejaa fedha taslimu dola...
za Kimarekani elfu 40, simu za mkononi 15, laptop 3 na pamoja na hivyo wakawakuta wote walikuwa na hati za kusafiria za kugushi ambazo zilikuwa zinawaonyesha kama raia wa Afrika Kusini.
Kwa hiyo wakataka kujua identity zao za ukweli.
Wakachukua alama zao za vidole na DNA alafu..
zikapelekwa maabara kupimwa.
La haula.! Achana na yule somo aliyekimbia, achana na yule Dere.. mtazame yule Abu Aish.
Vipimo vya DNA vilikuwa vyaonyesha kwamba Abu Aish jina lake halisi lilikuwa ni Fazul Abdullah Mohammed, top commander wa Al-Qaida kwa ukanda wote wa Afrika...
Mashariki.
Huyu Fazul Abdullah ndiye alikuwa moja ya mastermind wa ulipuaji wa Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam na Nairobi mwaka 1998.
Fazul Abdullah kijana mdogo msomi muhitimu wa chuo kikuu akiwa na shahada ya mifumo ya kompyuta. Akihitimu kama top student kwenye...
darasa lake.
Fazul Abdullah ambaye CIA wamekuwa wakimsaka kwa muda wa miaka 14 bila mafanikio.
Kesho yake Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani kipindi kile Bi. Hillary Clinton akafanya mkutano na wana habari kutangazia ulimwengu kuhusu ushindi huu mnono Marekani kufanya oparesheni
iliyofanikisha kuuwawa kwa Fazul Abdullah Mohammed.
Oparesheni ambayo ilifanywa na special force ya Somalia ikiongozwa na Kapteni Hassan Mohamed Abukar na mwakilishi wa CIA - Special Contractor Michael Goodboe (yule mzungu ambaye alikuwa amevalia kiraia pale kwenye kizuizi).
Sasa, kuelewa mwanzo wa tukio hili, kunatupa fursa ya kufahamu kuhusu oparesheni za CIA hapa Afrika Mshariki ambazo zafanywa kila siku mitaani kwetu.
Namna gani?
Hebu twende mwanzo kabisa,
Tarehe 14 Oct 2003 usiku wa saa sita maeneo ya Upanga mtaa wa Mfaume, Polisi wawili walio
valia kiraia walifika nyumbani kwa mwarabu anayeitwa Mohammed al-Asad na kumweleza wanahitaji kwenda naye kituo cha Polisi kwa ajili ya mahojiano mafupi.
Naomba unisaidie ku-retwee uzi huu tuwafikie watu wengi zaidi.
Nakuja kuweka PART 2.
Habibu B. Anga
To Infinity and Beyond
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.
