Zilikuwa siku 100 za vilio na kusaga meno mwaka 1994, Watu wapatao 800,000 waliuliwa na kabila la Hutu, jamii ya kitutsi ililwengwa katika mauaji haya vile vile hata wale waliojihusisha na siasa.
Kwibuka neno la Kinyarwanda likimaanisha Kukumbuka, leo imetimia miaka 27 tangu mauaji hayo ya kimbari yatokee huko nchini Rwanda.
Mauji haya ya kimbari yalianzaje?
Asilimia 85 ya raia wa Rwanda wanatoka katika jamii ya kihutu, huku idadi ndogo ya jamii ya kitutsi ikiwa imeshikilia nchi katika Nyanja za siasa na sehemu nyingine nyeti.
Mwaka 1959 Jamii ya Hutu iliweza kuangusha utawala wa kifalme chini ya Mwami Kigeli V Ndahindurwa na kupelekea watutsi 330,000 kuhamia nchini Uganda katika jimbo la Mbarara.
Kundi hilo baada ya kwenda uhamishoni waliamua kuunda kikundi cha waasi kilichoitwa Rwanda Patriotic Front (RPF) ambapo kundi hili liliingia rasmi nchini Rwanda mwaka 1990 walishambulia sehemu mbalimbali mpaka pale serikali ilipoamua kuyamaliza mwaka 1993.
Usiku wa tarehe 6 April 1994 ndege iliyokuwa imembeba rais wa Rwanda kipindi hicho Hayati Juvenal Habyarimana na aliyeongozana nae kiongozi wa Burundi Cyprien Ntaryamira wote wahutu waliuwawa baada ya ndege hiyo kudunguliwa.
Baada ya tukio hilo kutokea Jamii ya Wahutu wenye msimamo mkali walililaumu kundi la uasi la RPF kuwa wamehusika na mauji ya Rais Habyarimana na hapo ndipo walijikusanya, walihamasisha jamii ya kihutu kuchukua hatua kali dhidi ya watutsi wote nchini humo.
Walijuaje kama huyu ni mhutu au Mtutsi?
Ili uandikishwe kama raia wanchi hiyo ilikuwa ni lazima kabila lako liorodheshwe kwenye kitambulisho cha utaifa hapo ndipo vikundi cha kijeshi kilichofahamika kama Ntarahamwe na Impuzamugambi waliamua kufunga njia zote, waligawa mapanga...
na kuanza kuwachinja watutsi wote waliokutana nao.
Siku hii ukumbukwa ili kusamehe yale yote yaliotokea miaka 27 iliyopita, mwenge huwashwa kuashiria kuwa wahanga wote wavita hii ya kimbari hawajasahaulika.
#kwibuka27
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.