MSAFIRI Profile picture
Apr 7, 2021 11 tweets 4 min read Read on X
Zilikuwa siku 100 za vilio na kusaga meno mwaka 1994, Watu wapatao 800,000 waliuliwa na kabila la Hutu, jamii ya kitutsi ililwengwa katika mauaji haya vile vile hata wale waliojihusisha na siasa.
Kwibuka neno la Kinyarwanda likimaanisha Kukumbuka, leo imetimia miaka 27 tangu mauaji hayo ya kimbari yatokee huko nchini Rwanda.
Mauji haya ya kimbari yalianzaje?
Asilimia 85 ya raia wa Rwanda wanatoka katika jamii ya kihutu, huku idadi ndogo ya jamii ya kitutsi ikiwa imeshikilia nchi katika Nyanja za siasa na sehemu nyingine nyeti.
Mwaka 1959 Jamii ya Hutu iliweza kuangusha utawala wa kifalme chini ya Mwami Kigeli V Ndahindurwa na kupelekea watutsi 330,000 kuhamia nchini Uganda katika jimbo la Mbarara.
Kundi hilo baada ya kwenda uhamishoni waliamua kuunda kikundi cha waasi kilichoitwa Rwanda Patriotic Front (RPF) ambapo kundi hili liliingia rasmi nchini Rwanda mwaka 1990 walishambulia sehemu mbalimbali mpaka pale serikali ilipoamua kuyamaliza mwaka 1993.
Usiku wa tarehe 6 April 1994 ndege iliyokuwa imembeba rais wa Rwanda kipindi hicho Hayati Juvenal Habyarimana na aliyeongozana nae kiongozi wa Burundi Cyprien Ntaryamira wote wahutu waliuwawa baada ya ndege hiyo kudunguliwa.
Baada ya tukio hilo kutokea Jamii ya Wahutu wenye msimamo mkali walililaumu kundi la uasi la RPF kuwa wamehusika na mauji ya Rais Habyarimana na hapo ndipo walijikusanya, walihamasisha jamii ya kihutu kuchukua hatua kali dhidi ya watutsi wote nchini humo.
Walijuaje kama huyu ni mhutu au Mtutsi?
Ili uandikishwe kama raia wanchi hiyo ilikuwa ni lazima kabila lako liorodheshwe kwenye kitambulisho cha utaifa hapo ndipo vikundi cha kijeshi kilichofahamika kama Ntarahamwe na Impuzamugambi waliamua kufunga njia zote, waligawa mapanga...
na kuanza kuwachinja watutsi wote waliokutana nao.
Siku hii ukumbukwa ili kusamehe yale yote yaliotokea miaka 27 iliyopita, mwenge huwashwa kuashiria kuwa wahanga wote wavita hii ya kimbari hawajasahaulika.
#kwibuka27
@threadreaderapp unroll this please

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with MSAFIRI

MSAFIRI Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @msafiriulimal

May 13, 2020
Leornardo Da Vinci mchoraji mwenye michoro maarufu isiyochuja ulimwenguni alimchora Monalisa mke wa tajiri wa Italia, aliweka nembo zinazotambulisha picha zake kwa usiri mkubwa sana.
Leonardo Da Vinci alizaliwa huko Vinci Toscana nchini Italia, 15 Aprili 1452 na alifariki akiwa hajamaliza mwaliko aliopewa na mfalme wa Ufaransa katika mji wa  Amboise, 2 Mei 1519.
Mwaka 1514 alimtembelea tajiri mmoja ajulikanae Florentine ambaye alimtaka Leornardo Da Vinci amchore mke wake mrembo Lisa Gherardini kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa. Kwakua mtu huyu alikuwa mashuhuri basi LD hakukataa kabisa.
Read 8 tweets
May 6, 2020
UZI: Michael Jackson hakuwahi kubadilisha ngozi yake bali alisumbuliwa na maradhi ya Vitiligo yaliyodhoofisha ngozi yake
Ngozi ya Jackson ilikuwa rangi ya kahawia (au sana huita maji ya kunde) katika hali ya ujana wake, ila, kuanzia katikati mwa miaka ya 1980, hatua kwa hatua ngozi yake ikaanza kudhoofika mno kwa kile kilichofikiriwa kujichubua ngozi na kujibadilisha mwonekano wake kuwa Mzungu.
Mabadiliko haya yalienea katika kila chombo cha habari.Kwa mujibu wa wasifu wa J. Randy Taraborrelli, mnamo 1986, Jackson alifanyiwa tiba ya vitiligo na lupus; vitiligo yenyewe tu tayari ishafanya ngozi iwe nyeupe, na lupus ilikuwa inaishia; magonjwa yote mawili yalikuwa ...
Read 13 tweets
Apr 30, 2020
UZI.
THOMAS SANKARA CHE GEUVARA WA AFRIKA ALIENYANG’ANYWA KIGODA KWA RISASI YA KISASI. Image
Thomas Isidore Noel Sankara kiongozi kijana aliyependwa na raia wake na kusalitiwa na rafiki yake wa muda mrefu, alijulikana pia kama Che Geuvara wa Afrika kutokana na harakati zake za kuwapambania wanyonge wa taifa lake tukufu la Burkinafaso ambapo awali lililiitwa Upper Volta. ImageImage
Alizaliwa mwaka 1949 katika familia ya watoto kumi huku yeye akiwa ni mtoto wa tatu wazazi wake walitamani sana Sankara awe Padre wa kanisa katoliki na kufuata falsafa za Mtakatifu Thomas wa Akwino lakini Thomas Sankara alipenda sana walichopenda rafiki zake. Image
Read 23 tweets
Apr 2, 2020
Fuatana nami katika Uzi huu ili ufahamu,
Uswahiba wa Rais wa kwanza wa Uganda Kabaka Edward Muteesa II na Milton Obote na mvurugano wa Idd Amin Dada. ImageImage
Kipindi Uganda ipo katika harakati za kusaka Uhuru kulikuwa na mvutano mkubwa baina yao wenyewe kutokana na kwamba baadhi ya makabila makubwa kuchukua nafasi kubwa ya kupigania Uhuru wa Taifa hilo lakini baadae wanafunzi wa Makerere waliona ni bora kuanzisha chama ambacho...
kitawapa muongozo kuelekea Uhuru.
Kikaanzishwa Chama cha Uganda People Congress (UPC) kilichukua jukumu zito la kudai uhuru, lakini kutokana na Utashi na uelewa wa siasa za ukombozi Kabaka Edward Muteesa II mfalme wa kabila la Buganda aliona atapoteza sifa hiyo na kuamua....
Read 22 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(