Habibu B. Anga Profile picture
Author| To Infinity and Beyond

Apr 11, 2021, 25 tweets

MTANZANIA #1: JASUSI WA KUKODI, UJASUSI WA BIASHARA

Thread..

Si rahisi kuwa mahususi sana ni mwaka gani, lakini tunakadiria kwamba katikati ya miaka ya tisini hivi Mtanzania ambaye kwa sasa nimtaje kwa jina lake moja tu la Matiko aliondoka jiji Dar kwenda nchini Afrika Kusini

Kwa ajili ya kutafuta maisha. Lakini tofauti na Watanzania wengi wanaozamia SA ambako wakifika uanza kwa kufanya shughuli za hali ya chini, ilikuwa tofauti kabisa na bwana Matiko ambaye aliingia SA akiwa na mtaji wa kuridhisha kutokana na fedha ambazo alizipata toka kwenye mauzo

ya sehemu ya shamba lake la karibia Ekari 300 zilizoko kijiji cha Ghesaria Wilayani Serengeti.

Matiko akatumia mtaji huo akiwa hapo SA kuanzisha biashara ndogo ndogo
Moja ya biashara aliyoanzisha ambayo ilipanda mbegu ya kumbadilisha Matiko na kumfanya aingie kwenye ulimwengu wa

Ujasusi wa Kibiashara ilikuwa ni kampuni ndogo ya promotion aliyofungua iliyoitwa 80th Punch
Wahenga kama mie mnakumbuka kwamba hakujawahi kutokea nyakati bora kwa mchezo wa ngumi kama miaka ya tisini. Mapambano ya ngumi yalikuwa na msisimko na umaarufu kuzidi hata mechi za mpira

wa miguu.

Matiko hakutaka upepo huu umpite. Akaanzisha kampuni hiyo ndogo ili kuandaa mapambano ya ngumi pale Afrika Kusini

Mwaka 1999 kuna fursa adhimu sna ilijitokeza ambayo karbia kila mtu hakuiona
Mwaka ule lilifanyika moja ya pambano maarufu zaidi kuwahi kutoke. Pambajo la

ndondi kati ya Evender Holyfield vs Lennox Lewis. Pambano ambalo lilisha kwa majaji kutoa uamuzi unahosehabika wa hovyo zaidi kwenye historia ya ndondi, majaji hao wakisema matokeo ni Sare ingali ikiwa wazi kabisa Lennox Lewis alishinda pambano

Ulimwengu wote ulilpuka kwa hasira

watu wakitaka pambano lirudiwe na yatolewe maamuzi ya haki. Uhalali wa bodi zinazosimamia mchezo wa ngumi duniani ulikuwa uko rehani kwa kuonekana ni wala rushwa

Matiko akaona fursa. Na hii ilikuwa ni deal yake ya kwanza kubwa kabisa.

Nimesema huyu bwana alikuwa na kampuni yake

inaitwa 80th Punch inayoandaa mapambano ya ngumi. Hiki kikampuni chake kilikuwa kidogo cha mtaani. Hata kilikuwa hakijulikani wala hakina hadhi kubwa

Lakini akaona fursa.

Kipindi hicho Nelson Mandela alikuwa lulu ya dunia na ndio ametoka kupewa tuzo ya Nobel.
Nelson Mandela pia

alikuwa na NGO ya Nelson Mandela Foundation.
Mandela pia anajulikana alikuwa ni shabiki mkubwa haswa, shabiki kindakindani wa mchezo wa ndondi.

Matiko akamfuata Mkurugenzi Mtendaji wa Nelson Mandela Foundation. Akamweleza kwamba ana wazo adhimu.

Wazo lake lilikuwa kwamba..

Kwa kuwa ulimwengu mzima unapiga kelele kwamba lifanyike pambano la marudiano kati ya Evander na Lewis na haki safari hiyo itendeke wao kama Mandela Foundation wanaweza kutumia fursa hiyo.
Akamweleza kwamba ulimwengu ulikuwa hauna imani tena na vyombo vinavyosimamia mchezo huo..

Kwa hiyo Mandela Foundation waandae ‘mkanda’ wao wa ubingwa wa uzito wa juu. Kisha watumie ushawishi wa Madiba kuandaa pambano la marudiano.

Na pambano lisihusishe chama chochote cha ngumi duniani kwa kuwa watu hawana imani navyo tena, bali lisimamiwe 100% na Mandela Foundation

Kampuni yake yeye ya promotion (yaani 80th Punch) watalipwa commission tu ya kuandaa pambano.Mapato mengine yote yatakwenda kwa Mandela Foundation.

Mkurugenzi wa Mandela Foundation akalipenda hili wazo. Akalipeleka kwa Mzee Mandela. Mandela naye akalipenda wazo.

Watu wa Mandela

Wakakaa na Matiko kuandaa proposal ya kupeleka kwa Lennox Lewis na Evender Holyfield.

Wakaandaa na design ya mkanda utakaoshindaniwa. Mkanda utapambwa na vito vya thamani tofauti tofauti vya thamani ya dola milioni 3.Katikati ya mkanda kutakuwa na picha ya Mandela

Walipo maliza

Kuandaa hii proposal wakaipeleka Wizara ya Michezo ipewe baraka. Wizara ikakubali.

Kwa hiyo ikaandaliwa barua maalumu ambayo iliambatanishwa na ile proposal. Barua hii ilikuwa na signatures za Waziri wa Michezo na Katibu wa Rais (Rais alikuwa ni Mandela mwenyewe).

Baada ya hapo

Matiko akiwa kama Mkurugenzi wa 80th Punch ambao walikusudiwa kuwa waandaaji wa hilo pambano, akasafiri kwenda London kuonana na Meneja wa Lennox Lewis aliyeitwa Panos Eliades.

Menejiment ya Lennox wakalipenda wazo na kukubali.
Kama wakumbuka mwaka huo 1999 mwezi March, Lennox..

Lewis akafanya mkutano na wanahabri akiwa begani amebeba mkanda ambao katikati una sura ya Mandela. Akatangaza kutaka rematch na Evander na pambano hilo lifanyike Afrika Kusini na lisimamiwe na Mandela Foundation.
Press ile maarufu ya Lennox waafrika wengi tuliifurahia, kwamba...

hatimaye pambano la ngumi la kihistoria linakuja kufanyika kwenye ardhi yetu

Lakini menejiment ya Evander Holyfield lilikataa ile proposal. Na baada ya majadiliano ya menejiment ya mabondia hawa wawili,pambano lilikwenda kufanyika Las Vegas Marekani bila kuwahusisha Mandela wala

Matiko na 80th Punch yake.

Sasa,

Japo dili hii ilifeli, lakini ilipanda mbegu ndani ya Matiko. Kitendo cha kuishawishi serikali nzima ya Nelson Mandela, na menejimenti ya moja ya bondia mashuhuri kuwahi kutokea, kukubali wazo lake.. ilikuwa ni hatua kubwa ambayo ilimbadili..

Matiko kutoka kuwa promoter mganga njaa pale SA na kugeuka kuwa jasusi bora wa kibiashara barani Afrika.Akawa mtu ambaye anaweza kukupatia kitu chochote, au dili lolote alimradi tu uwe na uwezo wa kumudu fee yake.
Karibia kila madili makubwa makubwa unayoyaona kati ya serikali..

na kampuni binafsi, kuna mkono wa Matiko (nitasimulia deals kadhaa na uhusika wa Matiko)

Huyu Matiko nina imani wengi mmewahi kumsikia. Majina yake kamili ni Moto Matiko Mabanga.. au maarufu kama Moto Mabanga.

Kwa ambao mmewahi kumsikia lazima mtashangaa nilivyosema kwamba huyu

somo ni Mtanzania. Wengine watasema wamewahi kusikia huyu bwana ni Mrundi. Wengine watasema ni Mkongo. Wengine Mzulu na kadhalika.

Swali kama hilo pia limewahi kuulizwa na Jaji Kassim Nyangarika wa Mahakama Kuu ya Tanzania divisheni ya Biashara mwaka 2014. Alimuuliza Matiko...

inakuwaje yeye Mtanzania awe na passport ya Afrika Kusini.??
Moto Mabanga akiongozwa na wakili wake Mabere Marando akajibu kwamba Idara ya Intelijensia ya Afrika Kusini (NIA) walimlazimisha kuchukua passport ya South Africa.

Namna gani? Kwa nini wamlazimishe.? Kwa maslahi gani.?

Niwape mikasa kadhaa kuhusu huyu jasusi wa kibiashara. Mikasa kadhaa ili tuone namna gani biashara kubwa kubwa unazoziona, dili kubwa kubwa.. zina siri nzito na ujasusi mwingi nyuma yake.
Niwasimulie ni namna gani hata vitalu vyetu vya gesi tunavyoringia kule mikoa ya kusini..

Huyu bwana ndiye ambaye ameviuza..ameviuza kwa watu awatakao kana kwamba anauza karanga. Yes, kiuhalisia huyu bwana ndiye ameuza sio serikali yenu

Tuanze na mkasa huu..

Mwezi May 2007 Kampuni ya Vodacom iliingia kwenye moja ya skandali mbaya zaidi kuwahi kuwapata. Mkurugenzi wa

Vodacom na Wajumbe wote wa Bodi walikuwa wamesekwa lupango kwa amri ya mahakama.
Katika kutapatapa kutafuta suluhu ndipo wakaelezwa kwamba yuko mtu mmoja tu hapa barani Afrika mwenye uwezo wa kuwaokoa.. mtu huyo waliambiwa ni Moto Mabanga

Nitaweka PART 2..

Nisaidie Ku-Retweet

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling