Habibu B. Anga Profile picture
Author| To Infinity and Beyond

May 1, 2021, 26 tweets

𝗠𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 #1: 𝗝𝗔𝗦𝗨𝗦𝗜 𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗞𝗢𝗗𝗜, 𝗝𝗔𝗦𝗨𝗦𝗜 𝗪𝗔 𝗕𝗜𝗔𝗦𝗛𝗔𝗥𝗔

PART 3

Wakuu, mnisamehe bure, majukumu yalibana mno. Niko na muda wa kutosha sasa.
Nitaweka Parts kadhaa mfululizo kuwafidia uraibu niliowaachia muda wote huu.

Tuendelee

Mara ya mwisho

Nilieleza kuhusu mgogoro ambao ulitokea pale Vodacom Congo.
Ambapo Vodacom Group walikuwa wameingia ubia na kampuni ya Congolese Wireless Network kuunda kampuni ya Vodacom Congo ambapo kwenye ubia huo Vodacom Group walikuwa na 51% ya umiliki huku CWN wakiwa na 49%.

Lakini baada,

ya muda kukaibuka mgogoro. CWN wakiituhumu Vodacom Group kuendesha Vodacom Congo kana kwamba ni mali yao peke yao.
Lakini pia waliwatuhumu Vodacom kwa kutoingiza kiwango chote cha fedha za uwekezaji ambazo walikuwa wanatakiwa kufanya kwenye makubaliano ya mkataba.

Mgogoro huu..

Ukamfikia mpaka Rais Kabila.

Mwishowe yakafikiwa makubaliano kwamba Vodacom wanunue 49% ya umiliki wa CWN na kisha watafute mbia mwingine mzawa.

Lakini mwishoni ulipowadia wasaa wa kufanya malipo, Vodacom wakatangaza kutokubaliana na makubaliano ya awali ya kunununua 49% ya CWN

Serikali ya Congo ikaja juu na kumkamata Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom na Bodi nzima ya Wakurugenzi na kuwasweka Lupango.

Ndipo wakapewa taarifa kwamba yuko mtu mmoja tu mwenye uwezo wa kuwatoa kwenye shimo hilo. Mtu huyu ni Moto Mabanga.

Sasa tuendelee tokea hapo..

Ili kuelewa Vodacom na uhuni ambao waliufanya pale Congo na pia ili kumuelewa Moto Mabanga kuna matukio mawili kwanza nataka niwape.
Yaani kwamba matukio haya mawili yatatusaidia kuelewa sawia zaidi kwa nini Vodacom walifanya kile ambacho walifanya pale Congo na pia tutaelewa

kwa nini ni Moto Mabanga pekee alikuwa ana uwezo wa kuwatoa Vodacom kwenye kile kizungu mkuti pale Congo.

Matukio haya mawili, moja limetokea hapa kwetu Tanzania na la pili limetokea nchini Afrika Kusini.

Matukio haya mawili ni muhimu sana kuyaelewa kadiri tunavyoendelea na hii

Makala.

Nitaanza kwa kueleza tukio ambalo lilitokea nchini South Africa.

Miaka ya nyuma hapa kidogo pale SA kulikuwa na kijana mmoja anaitwa Nkosana Makate (mtu mzima sasa yuko kwenye 40s)
Miaka ya mwanzoni kabisa ya 2000's kijana huyu alipata nafasi ya kufanya internship makao

Makuu ya Vodacom hapo South Africa. Intership hii alikuwa anaifanya kwenye idara ya uhasibu ndani ya Vodacom

Kipindi hicho hicho pia kijana huyu alikuwa na mpenzi wake ambaye alikuwa anaishi mjini Polokwane (yeye alikuwa akiishi Midrand).
Polokwane na Midrand umbali wake ni kama

Dar na Tanga hivi. Kwa hivyo mahusiano yao kwa kiwango kikubwa yalikuwa ya simu.
Mara kadhaa walikuwa wakigombana kutokana na binti huyo kutompigia simu Nkosana mpaka pale tu Nkosana akimpigia, na sababu yake siku zote binti huyu alikuwa anasema hana salio la kupiga simu.

Kwenye

Kukereka kwa jambo hili Nkosana akapata wazo.
Kwamba, kwa nini mitandao ya simu isianzishe huduma ambayo itamwezesha mtumiaji akiishiwa salio kubofya namba fulani kisha mtu fulani lengwa apate 'notification' ya kumjuza kwamba fulani anahitaji ampigie simu.??

Kwenye kuwaza kwake

huku ndiko akabuni wazo la huduma ya "Tafadhali Nipigie" (Please Call me)

Aliporejea kazini akamshrikisha bosi wake wazo hili. Bosi wake akalipenda. Akamkutanisha na kigogo ndani ya Vodacom ambaye alikuwa anaitwa Philip Geissler ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Utawala na Product

Development na pia mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Vodacom.

Geissler naye akalipenda hili wazo. Akamwambie Nkosana aliandike wazo lake hili vizuri ili amsaidie kulifikisha kwenye vikao vya ngazi za juu.

Nkosana akajipinda akaandika proposal ambayo aliipa jina la Buzz Talk Time

Kisha akawasilisha andiko lake kwa Geissler.
Wakakubaliana kwamba kama wazo lake hili alilobuni litapitishwa na kutumiwa na Vodacom basi atapata 15% ya faida ambazo zitapatikana kutokana na simu ambazo zitapigwa kutokana na mtu ku-respond baada ya kupata "Tafadhali Nipigie"...

Kisha Geissler akachukua proposal na kuiwasilisha kwa Alan Knott-Craig ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Vodacom Group kipindi hicho.

Alan naye akalipenda wazo na kuagiza lifanyiwe kazi haraka

Miezi kadhaa baadae Vodacom wakazindua huduma yao mpya ya "Tafadhali Nipigie". Kwamba hata

Kama mteja hana salio anaweza kutuma ujumbe wa kuomba kupigiwa kwenda kwa jamaa na marafiki.

Huduma hii ikapendwa mno pale South Africa na kufanya Vodacom kuianzisha pia kwenye nchi nyingine ambako wana matawi.
Hata hapa Tanzania tukafikiwa na hii huduma ya "Tafadhali Nipigie"

Na tuliipenda haswa kama wakumbuka.
Punde si punde mitandao mingine nayo ikaiga.

Lakini kuna masuala mawili ambayo Vodacom walifanya uhuni.

Mosi, wakati wanazindua hii huduma nchini South Africa, waliwaeleza kwamba wazo hili lilibuniwa na CEO wao bwana Alan baada ya kuwaona..

walinzi wake nyumbani wakitaabika kuwasiliana na ndugu zao pindi wakiishiwa salio.

Pili, ile 15% ya kijana Nkosana hawakumlipa.

Kitendo hiki kilimuuma sana Nkosana. Kwanza wamekataa kumpa credit yeye kama mbunifu wa hiyo huduma na pili wamekataa kumpa hela yake 15% ya faida.

Kwa muda wa karibia mwaka mzima alijaribu kuonana na Geissler au Alan, lakini wote walikuwa wanamkwepa.

Ndipo akaamua kugeukia nguvu ya umma.
Kijana Nkosana akongea na vyombo vya habari na kueleza mkasa mzima namna gani alibuni wazo la tafadhali nipigie na ahadi ambazo alipewa..

akaonyesha na uthibitisho.

Umma wa watu weusi nchini SA ulilipuka kwa hasira. Nchi nzima iliwaandama Vodacom kwa unyonyaji na ukandamizaji wa haki ya kijana huyo mweusi.
Makampuni ya uwakili yakajitokeza kujitolea kumsimamia kesi kijana Nkosana. Hatimaye mwaka 2008 Nkosana..

akafungua kesi ya madai dhidi ya Vodacom kwenye Mahakama Kuu ya South Gauteng akidai fidia ya mamilioni ya Rand.

Hili ni tukio la kwanza ambalo nataka ulikumbuke.
Muhimu sana.

Nimesema yako matukio mawili.

Tukio la pili lilitokea hapa Tanzania. Nieleze,

Katika mwaka wa mwisho

wa utawala wa Mzee Mkapa, yaani mwaka 2005, nchi yetu ilifanya 3rd Round ya mnada wa vitalu vya gesi huko kusini mwa nchi.

Jambo moja ambalo watu wengi hawalifahamu ni kwamba vitalu vyetu vilikuwa haviuziki.. yaani vilikuwa havichangamkiwi.
Licha ya kelele zote za wanasiasa..

unazosikia wanapiga kuhusu gesi, ila vitalu vyetu vilikuwa vinadoda havichangamkiwi na makampuni uchimbaji gesi na mafuta. (Ndio maana siku hizi husikii sana kelele za gesi sababu hata mnada wetu wa mwisho wa vitalu (4th Round) uliofanyika mwaka 2014 nao ulidoda pia. Nitaeleza..

Vivyo hivyo pia ilikuwa kwenye mnada wetu wa kwanza 2001. Tuliweka mnadani vitalu 6 tukapata bid kwenye kitalu 1 tu.
Pia mnada wetu wa pili 2002 tuliweka sokoni vitalu 11 lakini tulipata bid kwenye vitalu 4 tu.

Mnada pekee ambao ulikuwa wa mafanikio ni huo wa 2005. Tulikuwa na..

Vitalu 7 tulipata bid vitalu vyote.

Jambo ambalo halijulikani ni kwamba mnada huu ulifanikiwa kutokana na uhusika wa Moto Mabanga.

Siku chache baada ya mnada kutangazwa, Moto Mabanga alifunga safari kwenda Huston, Texas kuonana na mtu anaitwa Dr. Alan Stein

Nisaidie ku-Retweet

Usiku huu naweka Part 4. Nitaweka mfululizo Part nyingi niwezavyo kuwafidia uraibu wa siku kadhaa hizo ambazo nimekuwa kimya.

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling