#TOTTechs Profile picture
Jukwaa la washauri na wataalamu wa Teknolojia || 💻 Computers ||📱 Phones | Softwares | ICT Hardwares | ICT Security || Partnership with Kukeke Gang and L.M.S

Jul 10, 2021, 18 tweets

UZI:

RADAR NA MATUMIZI YAKE

RADAR
Radar ni kifupisho cha (Radio Detection and Ranging)
Ni mfumo ambao unatuma signal/ishara kwenye kitu (object) na kuchambuliwa kisha kurudisha majibu ya hicho kifaa kwa mfumo huo wa signal kupitia hewa 👇

#ElimikaWikiendi

Ili kugundua uwepo, mwelekeo, umbali, na kasi ya ndege, meli, na vitu vingine

Signal ni mawimbi (radio waves) ambayo hutumwa kwa kifaa kilicho kwenye coverage ya Radar/eneo Radar inapofika na kukichambua hicho kifaa na kurudisha majibu kwenye chanzo/muongozaji

#ElimikaWikiendi

Kwa hapa Tanzania radar zinatumika kwenye viwanja vya ndege, jeshini na kwenye Meli. Na radar zilizopo zimegawanyika katika makundi mawili: Primary na Secondary radar

Tunapozungumzia hizi primary radar tunamaanisha ni zile Radar ambazo

#ElimikaWikiendi

Zina uwezo wa kutambua kitu kilichoingia kwenye eneo lake (coverage area) na kutuma taarifa za umbali wa kilipo hicho kitu. Hizi zinatumika jeshi, Viwanja vya ndege na kwenye meli

#ElimikaWikiendi

Pia Secondary Radar kutokana na mabadiliko ya kasi ya teknolojia hawa jamaa waliamua kuiwekea hii radar vitu vingi sana kama (DME Transponder)

Ambapo hichi ni kifaa kinachosaidia kutuma taarifa zote za kitu kilichokuwa target kwenye eneo la hiyo Radar.

#ElimikaWikiendi

Hii kwa hapa Tanzania inatumika Airport. Ambapo hizi Radar zinaweza kubadilishana taarifa na ndege inayokaribia kutua kwenye Uwanja wa ndege au ndege iliyopita kwenye eneo la hiyo Radar (coverage area)

#ElimikaWikiendi

Ambapo ndege lazima iwe na hicho kifaa ambapo kinabeba taarifa zote muhimu za ndege iyo mfano: Idadi ya abiria, ndege ilipo toka - inapoelekea, muda wa kutua n.k

Kwaiyo watu wa kituo cha aridhi watazipata hizi taarifa baada ya ndege kuingia kwenye anga Lao.

#ElimikaWikiendi

Kama ndege haina hicho kifaa hawatoweza kupata Hizo taarifa.

Ndio maana sehemu kama KIA mwanzo walikuwa wanatumia Primary Radar miaka ya hapa nyuma walichofanya sio kuitoa na kuiweka Secondary Radar Bali wamezifunga zote kwa pamoja.

#ElimikaWikiendi

Kwasababu hii secondary haiwezi pata taarifa za Ndege ambayo haina hicho kifaa ndio maana wakaibakisha primary radar. Ambayo ina uwezo wa kupata taarifa ya kitu kilichoingia angani japo sio kwa undani kama secondary

#ElimikaWikiendi

Pia hata jeshini ndizo wanazozitumia. Radar za jeshini hazina uhusiano wowote na Radar za Viwanja vya ndege. Labda wakitaka kushirikiana kama kutakuwa na serious issues hilo linawezekana.

Mfano Radar ya sasa hivi iliyopo KIA imebeba anga lote la mkoa ya Kaskazini hadi Nairobi

Ndege inapotaka kutua KIA kama kuna mwingiliano hapo Kati mtu wa Ardhi ana uwezo wa kumuongoza rubani akaituishe ndege Uwanja wa Kisongo, Arusha.

Uzuri wa hizi Radar kama ndege ndiyo Imefika Anga la Tanga

#ElimikaWikiendi

Mtu wa Ardhi anaweza kuona itatumia dakika ngapi kutua KIA, Kilimanjaro na dakika ngapi kutua Kisongo, Arusha

Huwa wanawasiliana tu kawaida kama mtu anavyoongea na simu kwa kutumia Radio signal.

#ElimikaWikiendi

Na pia mtu wa Aridhi anaweza kumtengenezea rubani barabara huko angani kama rubani akishindwa kuona mbele kwa sababu ya mawingu.

Huwa wana kuwa na vipimo vyao kuzingatia maeneo ya milima na njia ambazo ndege nyingine zinatakiwa zipite.

#ElimikaWikiendi

Suala la Helicopter na Drone
Kisheria hivi vitu kabla hazijarushwa angani lazima zipatiwe vibali kutoka TCAA ( Tanzania Civil Aviation Authority) bila hivyo ni kuvunja sheria na kutishia Hali ya usalama.

#ElimikaWikiendi

Helicopter ikiwa angani bahati mbaya ikawa inaelekea kwenye njia ambayo ndege itapita mtu wa ardhini anaweza mwambia pilot wa helicopter arudi nyuma au asimame kwasababu helicopter ina inaweza kusimama sehemu moja angani na pia Drone

#ElimikaWikiendi

Vibali vya kurusha kifaa chochote angani hutolewa TCAA.

Tanzania yote imekuwa coverage na Radar, Kuna radar ipo Songwe inacover eneo lote la kusini, Radar ya mwanza Kanda yote ya ziwa, ya KIA hii ni kubwa inafika karibia na mwanza, shinyanga mpaka Nairobi.

#ElimikaWikiendi

Radar ya Airport Dar es salaam inaenda mpaka inaungana na Radar ya Songwe

Kuhusu bandari meli ndizo zinakuwa na Radar ambazo zinawasaidia mabaharia kuweza kudetect meli nyingine, ardhi, umbali na pia kusaidia mwongozaji wa Ardhi kuwasiliana na Nahodha

#ElimikaWikiendi

Maana ya Radar
ni mfumo wa kugundua vitu ambao hutumia mawimbi ya redio kuamua aina, angle, au kasi ya vitu. Inaweza kutumika kuchunguza ndege , meli , ndege za ndege , miamba iliyoongozwa , magari , mafunzo ya hali ya hewa , na ardhi.

AHSANTENI

#ElimikaWikiendi

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling