Habibu B. Anga Profile picture
Author| To Infinity and Beyond

Jul 15, 2021, 19 tweets

𝗠𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 #1: 𝗝𝗔𝗦𝗨𝗦𝗜 𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗞𝗢𝗗𝗜, 𝗨𝗝𝗔𝗦𝗨𝗦𝗜 𝗪𝗔 𝗕𝗜𝗔𝗦𝗛𝗔𝗥𝗔

#7

Majukumu wakuu, mniwie radhi.

Tuendelee,

Mara ya mwisho nilisema, kuna Mtanzania ambaye mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu alidai kwamba alinyang'anywa passport na Idara ya Intelijensia

na kisha kupewa Hati ya Kusafiria ya nchi ya Afrika Kusini

Nikaeleza kwamba mtu huyu ambaye alikwenda Afrika Kusini kutafuta maisha mwanzoni mwa miaka ya tisini, mojawapo ya harakati zake kubwa za kwanza ni pale alipomshawishi Nelson Mandela na taasisi yake ya Mandela Foundation

kutuma ombi la kuandaa pambano la masumbwi la marudiano kati ya Evender Holyfield Vs Lennox Lewis yeye akiwa kama 'promota'.

Pia nikaeleza namna gani ambavyo kampuni ya Vodacom walimdondokea kumuomba awasaidie kuwatoa korokoroni wajumbe wao wa Bodi ya Wakurugenzi nchini Congo...

na pia kumaliza mgogoro wao na serikali ya Rais Kabila.

Nikaeleza pia kuhusu mkasa wa huduma ya "Please Call Me" ambayo kijana Nkosana Makate alikuwa anawashutumu Vodacom kwa kutumia wazo lake bila kumlipa.

Kwenye kuchimba skandali hiyo, ikatufikisha mpaka hapa Tanzania ambako

Moto Mabanga alifanya ujasusi adhimu wa kibiashara kwenye uuzaji wa vitalu vyetu vya gesi.
Nikaeleza namna ambavyo aliwakutanisha Tokyo Sexwale, Dr. Alan Stein na Jonatham Taylor na hatimaye kuunda kampuni ya Ophir Energy ambapo Moto Mabanga akafanya vikao vya siri na viongozi..

wa nchi waandamizi kuwashawishi kuwapa Ophir Energy vitalu

Baada wale vigogo waandamizi kukubaliana na Mabanga, ikaibuka changamoto, namna gani waandamizi wetu waliofanikisha dili hiyo watanufaika.
Ndipo nikasema kwamba Moto Mabanga akatoa 'mchoro' adhimu namna ambavyo watu wetu

watahongwa fedha katika namna ambayo ni almost impossible kwa mtu kushitukia kwamba wamehongwa au hata ku-trace fedha ambazo wamehongwa.

Nikaeleza kwamba Moto Mabanga akatoa wazo la serikali kuchukua mkopo
Tukaenda kukopa kiasi cha Shilingi bilioni 60 toka African Global Capital

Jambo ambalo bado lilikuwa halijulikani kipindi kile ni kwamba, African Global Capital ilikuwa inamilikiwa na kampuni inaitwa African Management Limited, AML. Ambapo hiyo AML ilikuwa ni joint venture ya kampuni mbili ambazo zinamilikiwa pia na Tokyo Sexwale (Mvelaphada Holdings

na Palladino Holdings).

Yaani kwa lugha nyepesi ni kwamba nchi yetu ilikuwa imesaini PSA Agreement ya uchimbaji wa gesi na Ophir Energy inayomilikiwa na Tokyo Sexwale, alafu wakati huo huo Tukaenda kuchukua mkopo wa Bilioni 60 African Global Capital ambayo nayo pia inamilikiwa..

na Tokyo Sexwale kupitia kampuni zake nyingine.

Umenifahamu.?

Sasa tuendelee tokea hapo, uone viroja vya namna ile bilioni 60 ilitumika.

Kama unakumbuka nilisema kwamba mkopo huu tulichukua kwa ajili ya kuanzisha shughuli za taasisi na idara zinazosimamia sekta ya Nishati...

yani kama vile uanzishwaji wa TPDC n.k ambapo mkopo huu utatumika kununua vifaa pamoja na kugharamia huduma na utaalamu kwenye mchakato huu

Sasa, Ukipekua nyaraka utaona kwamba kampuni ambayo ililipwa fedha nyingi toka kwenye mkopo huu inaitwa Floras Bell ambayo imesajili visiwa

vya British Virgin Islands.

Nyaraka zinaonyesha kwamba wamiliki wa kampuni hii ni watu wawili wanaoitwa Mark Willcox na Ian Hannam.
Huyu Ian Hannam ni maarufu sana kwenye ulimwengu wa banking.
Kama umewahi kusoma makala yangu kuhusu mabilioni ya Roman Abramovich, huyu ndiye yule

somo ambaye alitaka kuandikisha 'float' za kampuni ya Rusal kwenye soko la hisa la London.

Mmiliki wa pili, Mark Willcox ndiye ana utata mkubwa, sababu huyu jamaa licha ya kwamba ni mmiliki wa kampuni hii ya Floras Bell, bali pia huyu somo alikuwa ni CEO wa Mvelaphanda Holdings

(Ile ya Tokyo Sexwale).

Yaani kwa lugha nyepesi ni kwamba, kampuni ambayo tuliilipa fedha nyingi toka kwenye ule mkopo tuliochukua, moja ya wamiliki wake ni mfanyakazi wa Tokyo Sexwale kupitia Mvelaphanda Holdings.

Sasa wataka kuona maajabu.?

Miezi michache baada ya serikali..

kuwalipa Floras Bell.. kampuni hii ikafanya malipo ya mabilioni ya shilingi kwenda kampuni ya usafirishaji mizigo majini ambayo imesajiliwa nchini Cyprus (tuhifadhi jina kwa sasa). Ajabu ni kwamba kampuni hii inamilikiwa na mtoto wa kiongozi mwandamizi wa enzi zile

Abracadabra..

And that my friend ndio namna gani watu wanakula "maziwa na asali" wakati sie wengine tunapigania "unga robo, dagaa fungu moja"..!!

Hiki nilichowaeleza hapa ni sehemu ndogo tu ya mchoro ambao Moto Mabanga alikuwa ameutoa wa namna gani mabilioni ya fedha yalizungushwa na kisha...

kupotelea hewani, yakiingia mifukoni mwa watu.

Sasa, baada ya mabilioni hayo kuzungushwa, hatimaye katikati ya mwaka 2005 serikali iliitisha 3rd Round ya mnada wa vitalu ambapo vitalu 7 viliwekwa sokoni.
Na kampuni ya Ophir Energy ya Tokyo Sexwale ikashinda mnada na kupatiwa..

Vitalu vya Block 1, Block 3 na Block 4.
Mwaka uliofuata 2006 wakaongeza kitalu kingine na mwaka 2007 wakaongeza tena kingine.
Vitalu viwili vilivyosalia walipewa kampuni za Petrobras na Dominion Petroleum kilatu kimoja kimoja.

Sasa, nimeeleza kwa upana kabisa.. namna gani...

Tokyo Sexwale alifaidika na huduma ya Moto Mabanga kwa kupata vitalu vya gesi. Pia vigogo waandamizi walivyo jizolea mabilioni.
Najua utabaki unajiuliza, Moto Mabanga alipata nini? Alinufaikaje.?

Naja kueleza.. be here!

Nisaidie Ku-Retweet

Habibu B. Anga
To Infinity and Beyond

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling