Gavriel E. Toviel Profile picture
Human Rights Advocate. Rule of Law. Freedoms.

Aug 22, 2021, 13 tweets

Siasa za Tanzania katika jicho la tatu: Nini kinaendelea?

1. Mkuu wa Nchi anafariki akiwa madarakani. Huyu ndio Amiri Jeshi Mkuu wa Taifa hili. Sasa anafariki akiwa madarakani. Hiki kiti ndio cha juu zaidi kwenye kila nchi. Hiki kiti ndio nchi yenyewe.

2. Katibu Mkuu Kiongozi anaaga Dunia akiwa kwenye kiti chake. Kwa wasiofahamu, huu wadhifa ni mkubwa sana kwenye utawala wa nchi, hata Waziri Mkuu ni mdogo kwa kiti hiki. Naweza kusema hata Makamu wa Rais ni mdogo kwa umuhimu wa kiti hiki kwa Rais.

Huyu ni Rais mwenyewe kwa sura nyingine. Huyu ni mshikaji mkubwa wa Rais wa kupika na kupakua (Usidanganywe na protokali unayoona machoni hali ni tofauti sana katika uhalisia)

3. Waziri wa Katiba na Sheria anaaga Dunia akiwa kwenye kiti chake. Hiki kiti ni alama ya utamaduni na ustaarabu wa nchi katika kujitawala; sasa anafariki akiwa madarakani. Yaani huyu ni ustaarabu wa nchi katika kila eneo. Sasa, anafariki akiwa kwenye kiti chake.

4. Waziri wa Ulinzi anafariki Dunia akiwa kwenye kiti chake. Hiki kiti ni alama ya utekelezaji na uimara wa majukumu ya kiulinzi ya nchi. Kwa maneno mengine, huyu ndio mbeba mikoba ya ulinzi kwa ajili ya Rais.

Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi n.k. ni kama vitengo vya ulinzi tu, na Msimamizi wake mkubwa kwa niaba ya Rais ni Waziri wa Wizara hii.

5. Waziri wa Afya na Naibu wake naona wanapuyanga na Corona. Leo wanasema ipo Kesho wanasema haipo na Corona inaendelea kuwadondosha raia makumi kwa mamia. Kwa maneno mengine ukuta wa Afya wa nchi una-tikisika, nyufa kila mahali mithili umekumbwa na tetemeko kubwa.

7. Hatujakaa sawa, mwanamke anakaa kwenye kiti cha ukuu wa nchi (usiniambie hii ni kawaida). Mwanamke mwenyewe anatoka kwenye Imani ya watu wasioamini ukuu katika mwanamke. Na kama haitoshi, mwanamke mwenyewe anatoka kwenye nchi ambayo ni ndogo kiushirika wa Muungano (Zanzibar)

kulinganisha na mshirika mwenzie (Tanganyika). Sio kwamba hili haliwezi kutokea, la hasha ila hutokea kwa maandalizi mahsusi kabisa. Kinachotia fora zaidi mwanamke huyo anakaa kwenye kiti cha ukuu kwenye Jamii ya mfumo dume ulioshika hatamu.

7. Unadhani yameisha? Sikia na hii: Mjenzi Mkuu wa madaraja na barabara wa nchi anaaga dunia akiwa kwenye kiti chake. Yaani ni sawa na kusema huyu ndio anajua ramani ya namna ya kuunganisha nchi yote. Sasa, bila hili wala lile anadondoka kwenye kiti na kuhitimisha safari yake.

8. Kwa kuongezea Kiongozi Mkuu wa chama pinzani @freemanmbowetz anatiwa jela. Yes, ana kesi kubwa ya ugaidi. Hii haijawahi tokea tangu tupate Uhuru, Nini kinaendelea?

9. Kwa kuendelea mbele zaidi japo muhimu: Hivi nani anaelewa chanzo cha msimamo wa Mbunge anayepingana na Serikali yake (anayejiita askofu ‘Josephat Gwajima’). Anampinga Rais na wateule wake katika vita ya #UVIKO-19, kimaadili hii imekaaje? Mbona chama kipo kimyaaaaaa!

Kwa jicho la tatu, nabaki najiuliza: Je, kuna nini kinaenda kutokea kwenye ardhi na anga ya Taifa hili?

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling