#FAHAMU: ATHARI ZA UTOFAUTI WA KUNDI LA DAMU KATI YA MUME NA MKE.
Kuna baadhi ya wanawake wanapoteza mimba zao na wengine kupoteza watoto wao baada ya kujifungua sababu ikiwa ni utofauti wa kundi la damu kati ya mume na mke. Katika makundi ya damu kuna kitu kinaitwa RHESUS FACTOR
Kulingana na rhesus factors kuna makundi yafuatayo ya damu A+, A-, B+, B-, AB+, AB-, O+, O-.
Katika makundi ya damu mara nyingi mtoto hufuata damu ya baba. Hivyo, ikiwa kundi la baba lina antigen ya rhesus factor (A+, B+, AB+, O+) na mama akiwa hana hiyo antigen(A-,A-,AB-,A-)
Mtoto katika ujauzito wa kwanza atakuwa kama kundi la baba (rhesus positive) na hivyo mwili wa mwanamke utatengeza kinga (antibodies) dhidi kundi la baba. Hivyo katika mimba zinazofanya kiumbe kitakuwa kinashambuliwa na kinga ya mama (Rhesus incompatibility)
#ElimikaWikiendi
Hii haitegemei na matokeo ya mimba ya kwanza;kama kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza salama, mimba kuharibika kutokana na sababu zingine/ mwanamke kuamua kutoa mimba.
Mimba zitakazofuatia zitakuwa katika hatari kubwa kuharibika au mtoto kufariki baada ya kujifungua.
#ElimikaWikiendi
Damu ya mtoto itakuwa inavunjwa vunjwa (hemolysis) na kupelekea damu kupungua na kutengenezwa chembechembe (bilirubin) zinatakazomfanya apate manjano, kuvimba mwili kwa kujaa maji (edema). Kitalaamu hufahamika kama ERYTHROBLASTOSIS FETALIS
#ElimikaWikiendi #ElimikaWikiendi
JINSI YA KUEPUKA TATIZO HILI
- Wezi wapime makundi yao ya damu kabla ya kuamua kuoana au kupata watoto,
- Ikigundulika wana utofauti wa makundi ya damu hatarishi mwanamke atashauriwa kuchomwa sindano (Anti-D) wiki ya 28-34 na masaa 72 baada ya kujifungua ili kulinda ujauzito ujao
Zaidi kwa mwanamke mwenye kundi (group O) anapopata mume mwenye kundi jingine la damu inaweza kuleta shida (ABO incompatibility) kwa mtoto kwa kupelekea ugonjwa wa manjano (Neonatal jaundice) na hata degedege ikiwa bilirubin ikikaa kwenye sehemu ya ubongo wake (Kernicterus).
@threadreaderapp compile it
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.