Dr. Mlaluko, MD Profile picture
|MedicalDoctor|Author|TheResident|Poet|HealthJournalist|Father (Ammar, Raiyyan&Rufaydah)|HealthEyeAdvocate|SelfMotivated|Founder @jukwaalaafya|
May 4, 2022 12 tweets 8 min read
#FAHAMU: UGONJWA VIDONDA VYA TUMBO

Ni ugonjwa unaopelekea ukuta wa tumbo kuvimba (inflammation) au kulika (ulceration) kutokana na kiwango cha asidi kuzalishwa kwa wingi tumboni.

Tatizo hili niweza kusababishwa na sababu mbalimbali kama.... • Kunywa pombe,
• Kuvuta sigara,
• Mkazo/msongo wa mawazo (stress)
• Kuungua mwili (curling ulcer)
• Kuumia kwa ubongo hupelekea 'Cushing ulcer',
• Matumizi ya dawa za maumivu (NSAIDS) kama diclofenac, ibuprofen kwa muda mrefu
• Gastrinoma; uvimbe unaozalisha ASIDI
Oct 9, 2021 7 tweets 7 min read
#FAHAMU: VYAKULA BORA KWA WATOTO WADOGO KULINGANA NA UMRI WAO.

Watoto wanahitaji vyakula maalumu tangu wakiwa wadogo kwa ajili ya kuboresha afya zao na kuimarisha kinga ya miili yao ili kuepusha udumavu na kumkinga dhidi ya magonjwa mbalimbali kama PNEUMONIA, kuharisha n.k
#UZI ImageImageImageImage MIEZI SITA YA AWALI
Mtoto anahitajika kupata maziwa ya mama yake pekee bila kuhitajiwa kupewa kitu kingine kama maji/ juisi katika kipindi hiki. Isipokuwa anahitajika kupata chanjo ya matone au dawa. Mtoto anyonyeshwe usiku na mchana isiyopungua mara 10 kwa masaa 24. ImageImageImage
Sep 18, 2021 8 tweets 6 min read
#FAHAMU: ATHARI ZA UTOFAUTI WA KUNDI LA DAMU KATI YA MUME NA MKE.
Kuna baadhi ya wanawake wanapoteza mimba zao na wengine kupoteza watoto wao baada ya kujifungua sababu ikiwa ni utofauti wa kundi la damu kati ya mume na mke. Katika makundi ya damu kuna kitu kinaitwa RHESUS FACTOR ImageImageImageImage Kulingana na rhesus factors kuna makundi yafuatayo ya damu A+, A-, B+, B-, AB+, AB-, O+, O-.

Katika makundi ya damu mara nyingi mtoto hufuata damu ya baba. Hivyo, ikiwa kundi la baba lina antigen ya rhesus factor (A+, B+, AB+, O+) na mama akiwa hana hiyo antigen(A-,A-,AB-,A-) Image
Oct 19, 2020 7 tweets 5 min read
TATIZO LA MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI VIZURI (HEART FAILURE).
Moyo ni kiungo muhimu ktk mwili kinachotumika kusambaza/kupokea damu sehemu mbalimbali mwilini (mapafu, ubongo, figo, matumbo n.k). Hivyo, moyo kushindwa kufanya kazi hupelekea mwili kukosa hewa na chakula.
#Thread SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA MOYO KUSHINDWA KAZI.
1. Shinikizo la damu lisilothibitiwa barabara
2. Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital)
3. Magonjwa ya mishipa ya moyo (coronary artery d'se/ischemic heart d'se)
4. Magonjwa ya tezi shingo (thyroid dysfunction) n.k
Oct 18, 2020 7 tweets 5 min read
TATIZO LA FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI (KIDNEY FAILURE).
Figo ni kiungo muhimu sana kwenye mwili wa binadamu kwani hutumika kutoa takamwili kama; urea, maji ya ziada, chumvi n.k. Kushindwa kwa figo hupelekea takamwili kubakia mwilini hivyo kumletea shida mgonjwa.
#Thread SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI.
1. Kisukari
2. Shinikizo la damu
3. UKIMWI
4. Matumizi ya muda mrefu ya dawa zinazoweza kuathiri figo mfano; dawa za maumizi (diclofenac, ibiprofen n.k)
5. Matumizi ya miti-shamba
6. Pombe yaliyozidi
Aug 1, 2020 7 tweets 4 min read
FAIDA ZA KUNYONYESHA KWA MAMA NA MTOTO KIAFYA
Kutokana na utandawazi na harakati za maisha wanawake waliojifungua wamelazimika kutokunyonyesha watoto wao sawa sawa. Kitaalamu mtoto anatakiwa kunyonya miezi sita bila kupewa chakula isipokuwa dawa na chanjo tu
#UZI FAIDA KWA MAMA
1. Kumpunguzia hatari ya kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua
2. Ni njia moja wapo ya kupanga uzazi
3. Kumlinda dhidi ya kansa ya matiti na kansa ya kizazi
4. Kumjengea uhusiano mzuri na mtoto