Mwaka jana tuliona jinsi kijana HAMZA alivyoamshaamsha pale nje ya ubalozi wa marekani.
Sababu za amsha amsha ilidaiwa ni ugaidi lakini pia ilidaiwa ni kudhulumiwa madini yake na Askari.
Katika mazingira haya ni uchunguzi huru tu ndio ungetoa utata.
UZI👇
Kuunda tume huru wala sio jambo jipya.
Rais Kikwete alishawahi kuunda tume ya Jaji KIPENKA kuchunguza utata wa mauaji ya wafanya biashara ya madini kutoka mahenge.
Tume hii ilizaa kesi maarufu kama KESI YA ZOMBE
Jambo hili limejirudia tena Mtwara.
Safari hii pia likihusisha mfanyabiashara ya madini MUSA HAMISI HAMISI mkazi wa kijiji cha RUPONDA NACHINGWEA
Polisi walimuua MUSA tarehe 5 January 2022 na kuutupa mwili wake kijiji cha HIYARI wilayani Mtwara.
And in fact wahusika ni BIG FISHES
And a BIG SUM as well
Nakutajia BIG FISHES
1. OC-CID wa mtwara ASP Charles Onyango
2. OCS mtwara ASP Nicholaus Kisinza
3. Inspector John Mganga(Mkuu wa intelejensia jinai mtwara)
4. Mkuu wa zahanati ya polisi A/ inspector Marco Mbuta.
Umeshajiuliza mtu za zahanati aliingiaje?
Kosa la marehemu lilikuwa ni kudai pesa zake zilizochukuliwa na polisi bila kujaza hati ya kushikilia mali. Certificate of seizure
Ikafata dhahama
In a very serious note Mkuu wa jeshi la polisi hatakiwi kuwa ofisini kuonyesha collective responsibility.
Then picha imeungua vibaya sana baada ya kutengenezwa tukio la askari mtuhumiwa kujinyonga kwa tambala la deki.
Inafika mahali ni bora ukutane na jambazi kuliko polisi.
Tukio hili limeliweka uchi jeshi hili.
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.