Pool of thoughts. A commander of the hand to mouth battalion. Environmental Pioneer. Social Engineer. #CertifiedMchapaUzi . Telegram: https://t.co/aEEOOryJWO
16 subscribers
Sep 6 • 24 tweets • 9 min read
Huko Harare, Zimbabwe katika barabara ya Borrowdale, kuna eneo la maduka makubwa maarufu kwa jina la Ballantyne Park Shopping Centre
Mwaka 2008, ilikuwa ukienda katika duka No. 19 kwenye maduka haya, ungekutana na mgahawa maarufu wa Millers Cafe
Mgahawa huu umebeba simulizi
Siku moja mchana mwaka 2008, nikiwa nimeboreka, niliingia kwenye mgahawa wa Millers
Niliongoza kwenye kiti kimojawapo ndipo nikasikia sauti ya mtu aliyekuwa ameketi nyuma yangu ikiniita
Nilipogeuka nikashtuka kubaini anayeniita ni mchungaji Uebert Angel Mudzanire
Sep 5 • 13 tweets • 5 min read
𝐒𝐨𝐦𝐞𝐭𝐢𝐦𝐞𝐬 𝟐𝟎𝟐𝟑
𝐋𝐨𝐠𝐢𝐬𝐭𝐢𝐜𝐬 𝐂𝐚𝐦𝐩
𝟖𝟑𝟏 𝐊𝐉
𝐌𝐆𝐔𝐑𝐀𝐍𝐈
𝟎𝟓𝟒𝟐 𝐇𝐑𝐒
Lutueni Kanali E.A Sambila ambaye ndiye Commanding Officer wa 831 KJ anapokea taarifa nyeti ofisini kwake kutoka kwa askari wake wawili wahusikao na ulinzi amani kikosini (MPs)
Askari hawa wawili ambao ni P.12925 Captain Theresia Cylil Massawe na MT. 88710 Sergeant Mohammed Faki Haji walifika ofisini kwa Lt.Gen Msambila wakieleza kuwa wana taarifa ya dharula
Kuwa kuna uwezekano wa muda wowote amani kutoweka mle kikosini
Wakaruhusiwa kuingia
Aug 30 • 45 tweets • 18 min read
Tarehe 28 August 2025, chama tawala, CCM kilizindua kampeni zake za uchaguzi mkuu wa urais na wabunge katika viwanja vya Tanganyika packers
CCM walilazimika kutumia jukwaa hilo la uzinduzi wa kampeni kujibu mashambulizi kutoka kwa mwanachama wake mwandamizi Humphrey Polepole
Tangu kujiuzuru kwake July 13, mwaka huu kwa kile alichoeleza kama "kutoridhishwa na mienendo" ya serikali yake, balozi huyo wa zamani wa Tanzania nchini Cuba, amekuwa akitoa tuhuma mbalimbali dhidi ya viongozi waandamizi wa chama chake na serikali
Aug 2 • 25 tweets • 10 min read
Una uhakika kuwa wewe binafsi ulionana na IGP Sirro?
Unaweza kunieleza kwa ushaidi ni mara ngapi na wapi ulionana naye?
Unajua kuwa tuhuma unazotoa ni nzito ukihusisha watu wakubwa sana nchini?
Ilikuwa zamu yangu kuanza kumhoji mwanamama Jeannie Pollaert raia wa Netherlands
Nililazimika kumuuliza mama huyu maswali haya usiku wa manane baada ya kumaliza kusoma makabrasha mengi aliyonitumia kwa njia ya barua pepe.
Nilichokikuta ndani ya makabrasha yale kilifanya usingizi uliokwishaanza kunitongoza utoweke
Infact niliogopa sana
Nilihitaji ushaidi
Jun 27 • 76 tweets • 25 min read
Mwaka 2012, Blandine Nyoni akiwa katibu mkuu wizara ya afya, alinukuliwa akitoa kauli tata ya kuwabeza madaktari kuwa "wanajiona bora wakati ni wachafu na hawajui kiingeleza"
Katibu huyu akaendelea kusema kuwa hata yeye alisoma mchepuo wa PCB na kufaulu vizuri tu lakini kwa kutambua ubovu wa Medicine mzazi wake akamsomesha Accounts so hajui madaktari wanalalamikia nini.
Kauli hii ikang'oa kilaka kwenye jeans ya bishoo!
May 9 • 34 tweets • 13 min read
Wiki hii tumeshuudia waliokuwa wanachama wa Chadema wakitangaza kuachana na chama hicho huku wakiahidi kuelezea hatima zao za kisiasa siku za mbeleni
Kati ya waliohama ni waliowahi kuwa viongozi waandamizi wa chama hicho
Hii inamaanisha nini?
Kabla sijajibu swali hilo ni vyema tukipitia kwa ufupi mtiririko wa matukio (A quick refresher)
1. Dec 12,2024, Tundu Lissu anatangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti CHADEMA taifa
Nia hii ya Lissu ilikuja baada ya kuwa uchokozi wa wazi dhidi yake ndani ya chama
Mar 12 • 13 tweets • 5 min read
Monday, 24th,
June 1996 10:30 AM
Central Police post, Dsm
Majira ya saa nne asubuhi, anaingia kituoni hapa mfanyabiashara mwenye asili ya Asia ndugu Walji D Ladwa
Hapa kafika ili kutoa taarifa juu ya kuibiwa kwa gari lake lenye namba za usajili TZG 50
Polisi katika upelelezi wao wakatajiwa kuwa gari ile imeonekana akiwa nayo jambazi mmoja sugu sana ambaye alikuwa kwenye radar za polisi kwa muda mrefu.
Mar 11 • 28 tweets • 10 min read
Jan 22, 2024 kwenye kikao cha baina ya CDF na makamanda kwa upande mmoja, na Amiri Jeshi mkuu kwa upande mwingine,Mkuu wa majeshi alitoa kauli iliyoibua udadisi
"Kuna wakimbizi wameteuliwa serikalini kwenye nafasi za maamuzi"
Kauli hii ilikuwa ni nzito kutoka kwa mtu mzito.
Nasema mtu mzito kwa kuwa, mtu aliyetoa kauli hii ni mwenye nafasi ya kupata taarifa zote za intelejensia za nchi hii
Kwanza kama mwenyekiti wa kamati ya majeshi ya ulinzi
Pili akiwa kama kiongozi kwenye taasisi yenye chombo kinachofanya "military intelligence" siku zote.
Feb 25 • 8 tweets • 4 min read
Kumekuwepo na taarifa za kukamatwa kwa wahusika wa kampuni ya LEO BENEATH LONDON (LBL) inayoendesha biashara ya upatu, kukusanya amana, na kutoa riba kwa wanachama wake.
Victims wengi wa kampuni hii wakiwa ni watumishi wa kada ya ualimu
Pia Benki kuu imetoa taarifa ya kutoitambua wala kuipatia leseni kampuni hiyo.
Hapa ndipo napata maswali kuhusu umakini wa taasisi zetu zinazohusika na ukusanyaji wa taarifa za kiitelejensia
Taasisi hizi huwa hazipati fununu ya uwepo wa kampuni hizi kabla watu hawajatepeliwa?
Feb 24 • 40 tweets • 14 min read
Sometimes March 2013 Wakili Fatuma Karume alisafiri kutoka Dar kwenda mkoani Kilimanjaro. Wakili huyu alikuwa amesafiri akiwa amebeba nyaraka furani ya muhimu. Nyaraka ile alikuwa anaenda kumsomea na kumkabidhi mzee fulani aliyefahamika kwa jina la Juma
Actually, Mzee Juma naye alikuwa ni wakili ambaye sasa amestaafu akiwa amefanikiwa kurithisha taaluma hiyo pia kwa mwanae ambaye alikuja kuwa ni wakili maarufu sana mkoni Arusha. Fatma hakujua kama nyaraka aliyobeba ingeleta taflani kubwa ndani ya familia ya Mzee Juma.
Feb 21 • 22 tweets • 9 min read
Ni mara ngapi tumesikia watu wakitoa shuuda kuwa gari fulani lilimuacha na kisha mbeleni gari hilo likapata ajali? Hili ndilo lililomtokea Moses John miaka miwili iliyopita. kijana huyu ni muuza simu katika jengo la CHINA PLAZA lililoko mtaa wa Aggrey Kariakoo. Thread👇
Kuna wakati unaweza unaweza kushindwa kusafiri kwa sababu tu basi ulilopanga kusafiria limekuacha baada ya kuchelewa. Hupaswi kujilaumu kama hili litakutokea. Mara nyingine Mungu huwa anaingilia kati ili kukuepusha na baya ambalo lingeweza kukutokea ndani ya basi hilo.
Jan 31 • 20 tweets • 7 min read
Ukweli mchungu
Kabila la Watusi halina asili ya Kongo hata kidogo kabla au hata baada ya Berlin Conference.
Makabila asilia ya Kongo yalikuwa ni Wambuti, Wabaka na Watwa
Sasa nifatilie kwa makini na achana na "manipulative propaganda"
Kama tumesoma history vizuri, kadili binadamu alivyoweza kuimprove zana za uzalishaji (After Iron age) aliongeza uzalishaji
Jamii zikaanza kukua from nuclear family to Clanship ambapo waliongozwa na machifu, hadi Kinship societies
Jan 18 • 21 tweets • 8 min read
Ilikuwa ni mara ya kwanza nchini kushuhudia tukio hili la tarehe 6 December, 2016 ambapo maiti 15 zilivuliwa mto Ruvu- Bagamoyo mkoani Pwani ikiwa imefungwa kwenye viroba.
Naam!
Baadae miili mingine ikaokotwa kwa nyakati tofauti katika maeneo mbalimbali hasa fukwe za bahari ya Hindi.
Miili mingi ikiwa kwenye viroba.
Same style, same fashion!
Kuanzia hapo ikawa si ajabu tena kuanza kusikia fulani katoweka bila hatima yake kujulikana.
Jan 14 • 36 tweets • 12 min read
Saa 12 na dk 31 alfajiri ya tarehe 24 mwezi May 2014, msafara wa
malori 16 yenye namba za usajili wa Urusi yalivuka mpaka wake na
kuelekea eneo la Donetsk inchini Ukraine.
Malori 10 kati ya haya yalikuwa yamefunikwa kwa maturubai
yenye nembo zilizoandikwa kwa lugha ya Kirusi “гуманитарная
помощь”
Maana ya maneno hayo kwa kiingereza ni :Humanitarian Aid"
Jan 9 • 25 tweets • 9 min read
Majira ya usiku tarehe 25 june 2019, Kabendera alikuwa akirudi nyumbani kwake Mbweni.
Akiwa anapita chuo cha National defence akabaini gari tatu zinamfata kwa spidi kali.
Kabendera akaamua kuongeza mwendo lengo lake akimbilie hoteli ya Bahari beach kwa usalama wake
Moja ya gari lililokuwa linamkimbiza lilipita gari ya Kabendera kwa ubavuni ambapo watu wawili kati ya waliokuwemo garini mule walimtolea bastola kumtaka asimame
Kabendera akaamua kuongiza gari katika eneo la nyumba isiyo na uzio
Mwenye nyumba ile naye akatoka na bastola
Dec 29, 2024 • 19 tweets • 6 min read
Kuanzia mwaka 2016, Watu maarufu kama MAPEDEJEE walikuwa na wakati mgumu sana.
Watu hawa ambao walikuwa wakiimbwa na kusifiwa na wanamziki wa dansi Walianza “kusomeshwa namba”
Nani asiyekumbuka kesi za kina Ndama mtoto wa ng’ombe na Papaa Msofe Chuma Cha Reli Laini ya Mwisho?
Watu hawa walikuwa wakinong’onwa kuwa wanajihusisha na dili za gizani zinazowapa ukwasi wa kumwaga pesa hovyo kwa wanamziki na pisi kali.
Minong’ono hii haikuwahi kuthibitishwa nami sitaki kuwahukumu.
Uzi huu ni maalumu kwa ajili ya PEDEJEE YANGA OMARY RAIS WA TANGA (RIP)
Dec 25, 2024 • 31 tweets • 11 min read
It all started with just one phone call conversation
Saturday, 19th September 2020
Makokola
Tabora Urban
Siku hiyo kulikuwa na match ya mpira wa miguu kati ya Man U na Crystal Palace
Watu wawili wakapigiana simu majira ya saa 1 jioni
Mazungumzo yao yalikuwa hivi👇
DIDA: Mambo Gabriel....Leo tunaenda kuangalia mpira?
GABRIEL: Poa!....Tukaangalizie wapi?
DIDA: Tukutane Oksjen Pub
GABRIEL: Poa, natoka sasa hivi
Ingekuwa ni bora sana kama Gabriel asingepokea simu hii
Dec 21, 2024 • 31 tweets • 12 min read
Kiistoria, kila unapobaki mwaka mmoja au miwili kuelekea uchaguzi mkuu wa rais na wabunge nchini, ndani ya chadema kunaibuka minyukano.
Hii ilikuwa kweli mwaka 2008 na 2009, kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010
Na Ikawa kweli 2013 na 2014, kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
Naam!
Na sasa ni kweli pia mwaka huu ukiwa umebaki mwaka mmoja tu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, tunaona minyukano
Makala hii inawajia kujibu ombi la waliotaka maoni yangu juu ya kinachoendelea ndani ya chama hicho baada ya Tundu Lissu kunuia kugombea uenyekiti.
Dec 17, 2024 • 15 tweets • 6 min read
Kwa siku chache zilizopita, zilisambaa taarifa juu ya kutoweka kwa "mfanyabiashara" Daisy Simon Ulomi.
Neno "Mfanyabiashara" sijaliwekea kwa bahati mbaya alama za kufungua na kufunga semi.
Ni kwa sababu inadaiwa Daisy Ulomi alikuwa ni zaidi ya "Mfanyabiashara"
Tutajadili...
Taarifa ya kutoweka kwake ilieleza kuwa bwana Ulomi alipigiwa simu kutoka TRA akifahamishwa juu ya kuwasili kwa kontena lake kwenye bandari kavu ambayo haijatajwa.
Ilielezwa kuwa Ulomi aliondoka kwenda kufatilia kontena lake akitumia usafiri wa pikipiki yanye usajili MC 415 DQC
Dec 16, 2024 • 7 tweets • 3 min read
As I am writing, the dude is in police custody pending interrogation
Kuna mengi juu yake
Hata gari ya Ractis aliyokuwa akiendesha kabla ya kadaiiwa kutekwa ilikutwa ikiwa inabadilishwa rangi from silver to black
Hili halikuwekwa wazi for investigation purposes
Iko hivi👇
Ni maisha yaliyojaa controversy.
Nanukuu
"Kabla ya mwaka jana alikuwa anaenda China... So hapa ofisini alikuwa anakuja siku mojamoja."
"Kipindi hicho alikuwa analenga magari aina ya Brevis tu."
"Kuna wakati alifikisha hadi Brevis 10"
Anaendelea👇
Dec 14, 2024 • 48 tweets • 16 min read
Angekuwa @bajabiri sijui angekipa marks ngapi kitongoji cha Mwandiga, Kigoma.
I normally say this,
In the entire animal kingdom, a human is a very complex animal.
Kwa nini nasema haya?
Just read me..
Of all the animals in the animalia kingdom, instead of being equipped with the capabilities of distinguishing good deeds from evil ones, a human can perform very unimaginable mayhem on his fellow being without any sense of amnesty.