James Munisi Profile picture
Creator & Innovator | Electronics & Telecom Engineer | Business Administrator | 1+1=11 | All about Techs | Founder @Njiwa_Store | We are @TOTTechs |#SimuZaNjiwa

Feb 25, 2022, 17 tweets

#UZI
πŸ’¨ KISANGA CHA TAIWAN NA CHINA

Taiwan ni kisiwa kidogo ila ni moja kati ya sehemu hatari zaidi duniani.

Mama wa Taiwan ni jeuri plus kiburi anayopewa na Marekani, China naye anasema ni jimbo lake na lazima atalirudisha kundini.

Hii colabo ya Urusi na China πŸ‘‡

Twende chap chap
Miaka hiyo baada ya vita ya pili ya dunia kuna vita vilikuwa vinaendelea huko China vya wenyewe kwa wenyewe kulikuwa kuna People's Republic of China (PRC) iliyokuwa chini ya Chinese Communist Party (CCP) walikuwa wanapigana vita na Republic of China (ROC).

PRC ilikuwa chini ya Mwamba mmoja wa kuitwa Mao Zedong mtu katili zaidi duniani aliuwa watu milioni 78 ndiye anayeongoza duniani akifuatiwa na Jozef Stalin milioni 23

1949 wakafanikiwa kuuteka mji mkuu wa China Beijing na kuitawala China na baadhi ya members wa ROC kawakimbilia

Taiwan. Hawa jamaa ni Wachina kabisa kinachowatofautisha na Wachina bara ni huo uadui. Wana chuki kubwa mno na Chama cha Communist wanaweza wakakubali kutambulika kama sehemu ya China lakini sio chini ya Communist.

Raisi wa China Xi Jinping huwa anasema Taiwan ni sehemu yaC

China na itarudi China.

Huko Taiwan wanaongozwa na Raisi Mother mmoja mtata sana anaitwa Tsai Ing-wen ngoja kwanza.

Wao ROC waliokimbilia Taiwan wa miaka ile wengi wao walikuwa ni watu wenye akili mingi sana kwenye issue za Teknolojia walikuwa wana formula kibao

Ndani ya muda mchache tuh waliweza kuionyesha dunia wao ni wakina nani.

Jamaa walianzisha viwanda vingi vinavyohusiana na masuala ya Teknolojia leo hii Taiwan ina husika zinatengeneza 92% ya semiconductors duniani.

Hapo Taiwan kuna kiwanda kinachoitwa TSMC ndicho kiwanda pekee duniani chenye Teknolojia ya hali ya juu kwa kutengeneza Chipsets (processor) za simu, computer na za vifaa vingine vya electronics pia na semiconductors nyingine.

TSMC inaziunda processor kama A Bionic (Apple πŸ‡ΊπŸ‡Έ), intel πŸ‡ΊπŸ‡Έ, Snapdragon πŸ‡ΊπŸ‡Έ, Kirin πŸ‡¨πŸ‡³ n.k kampuni ni nyingi mno.

Pia kuna viwanda vingine kama MediaTek, (Foxconn na Wistron) hivi ndivyo viwanda pekee vinavyounda simu zote za iPhone duniani.

Pia kuna Acer watengezaji wa Computer

Kuna makampuni zaidi ya 50 yanayoitumikia dunia hapo Taiwan. Vuta picha ichi kisiwa China akiweke kati tukizingatia pia na mchango alio nao China kwenye nchi nyingi duniani.

Je hapo Marekani atathubutu kuiwekea China vikwazo kama alivyofanya kwa Urusi?

Ndio maana kila wakati China anapitisha ndege zake kwenye Anga la Taiwan πŸ‡ΉπŸ‡Ό kifanya doria.

Marekani ndiye anayempa jeuri Taiwan anampa msahada mingi ya kijeshi na mingine kitu ambacho China aliiambia Marekani inacheza na moto.

Taiwan ni nchi ambayo ina Raisi, jeshi, pesa yake na sifa nyingine zinazoifanya itambulike kama nchi.

Lakini ni nchi chache sana duniani zinazoitambua Taiwan kama nchi. Maana China bado anaendelea kutaka ku-master issue za Taiwan kimataifa.

Kuna baadhi ya nchi zinazotambua uwepo wa Taiwan kimataifa huwa zinaingia kwenye mgogoro na China.

China anatumia nguvu nyingi sana kulitawala lile eneo la bahari ya Kusini ya China kwasababu Marekani ana kambi nyingi karibia na hayo maeneo pia na nchi anazoshirikiana nazo

Kama Japan hii kitu China anaona itahatarisha usalama wa nchi yake ndio maana anapambana kwa kila hali ili kuiweka Taiwan kwenye himaya yake.

China ina watu bilioni 1.4 na Taiwan ina watu milioni 23.57 ila Taiwan itabaki kuwa moja ya maeneo hatari zaidi duniani.

CHINA KWENYE VITA YA 3 YA DUNIA?

Jana wakati Urusi anaivamia Ukraine China naye alipeleka ndege zake 9 kwenye anga la Taiwan kinyume na sheria kuangalia usalama wake.

Huwa ni kawaida yake kupitisha ndege zake kwenye anga la Taiwan.

Marekani ameitaja China pamoja na nchi nyingine kama Urusi, Iran, North Korea na vikundi vya ISIS kuwa zisitake vita naye watajuta.

Urusi anasubiria Marekani aingize jeshi lake Ukraine ndivyo China anasubiria Marekani aingize jeshi lake Taiwan.

Wakati nchi nyingine zikitafuta njia ya kiwatoa raia wake Ukraine, China imewaambia wakae ndani kisha waweke Bendera ya China πŸ‡¨πŸ‡³ nje ya hizo nyumba walizopo.

Je China anataka kuingia naye Ukraine kimkakati? Pia Xi Jinping amefanya mazungumzo ya simu na Putin.

Huyu Raisi wa Taiwan President Tsai Ing-wen na Udogo wa nchi yake hajawahi iogopa China.

Tusubirie nini kitatokea
Kwa simu zote kali Brand new tucheki

πŸ“Infinix Tower, Kariakoo | Tunasafirisha Mikoani 🚚
@SimuZaNjiwa
πŸ“ž 0745100757

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling