π€ Naomba Tuongee kuhusu Piston za gari yako.
Piston ni mfumo muhimu sana kwenye engine ya gari lako, na kama vilivyo vifaa vingine Piston pia inahitaji maintenance.
Leo hii nitakupa dalili 3 za piston inayohitaji kubadilishwa.
Are you ready?
β Thread β
Piston ni sehemu ama kifaa mojawapo katika engine ya gari ,ambacho hutumika kudhibiti hewa na mafuta ndani ya cylinder.
Pia kutoa nguvu itokanayo na kuungua kwa mafuta kupitia connect rod hadi kwenye crankshaft.
Piston hufanya kazi kwa ushirikiano katika engine na kusababisha kuizungusha crankshaft.
Crankshaft inapozunguka hupeleka nguvu katika gear box hadi kwenye differential kupitia propeler na hatimaye tairi kutembea.
Piston inapopanda juu na kushuka chini
Hatua hii husababisha mapigo manne ndani ya chemba za cylinder.
1. Pigo la kwanza.
Piston inashuka chini. Kitendo hiki huruhusu valve kuingiza hewa safi au hewa iliyochanganywa na fuel. (inategemeana na injini kati ya petrol au diesel)
2.Pigo la pili.
Piston inapanda juu
Kitendo hicho kinasababisha ile hewa safi iliyo ingia kwenye chemba kukandamizwa kwa mgandamizo mkubwa sana, na hewa hiyo kuwa na joto kubwa sana.
Kisha plug inatoa cheche au nozeli inanyunyiza mafuta (plug au nozel, hapa inategemeana na engine ya petrol au diesel.
3 Pigo la tatu.
Baada ya ile hewa yenye joto kali kukutana na cheche kutoka kwenye plug au mafuta kutoka katika nozel husababisha mlipuko mkubwa uliosababishwa na kuchomwa au kuunguzwa kwa hewa hiyo.
Mlipuko huo husababisha piston kusukumwa kwa nguvu kubwa kushuka chini na chemba za cylinder kubaki wazi ikiwa na hewa chafu iliyochomwa.
4 Pigo la nne
Baada ya piston kushushwa chini, hupanda juu na valve hufunguka ili kutoa ile hewa chafu ndani ya chemba na kuitoa nje kupitia bomba la kutolea moshi (exhaust).
Baada ya hapo piston hurudia mzunguko wake tena kuanzia pigo la kwanza hadi la nne.
Piston zinaposhirikiana katika kukamilisha mapigo haya ndio husababisha kuizungusha crank shaft na kusababisha mwendo wa gari.
Utaona dalili zifuatazo iwapo pistons zimeharibika:
1. Gari yako itaanza kutoa moshi mwingi wenye rangi nyeupe au kijivu.
2. Gari lako kupoteza nguvu hasa ukiwa kwenye mwendo mkubwa, ghafla tu unaona mwendo unapungua.
3. Matumizi ya mafuta hapa yataongezeka kwelikweli.
Jambo la kuzingatia zaidi hapa ni kwamba unapoona dalili hizi unapaswa upeleke gari yako kwa fundi ili wazibadili hizo pistons.
Fundi mzuri ni yule atakayekusikiliza na kupima kwanza tatizo lilipo, as always I recomend that uende kwa Trusted mechanic.
Asante kwa kusoma thread hii. π
Kama umependa kuisoma thread hii...
1. Follow me @Mentormania123 for more contents about cars and how to maintain it.
2. Retweet the first tweet, so as to share this thread with your audience.
Drive safe and be safe
From ππππ‘ππ to You
Β€ Images courtesy
Cc.
- @BobWaMagari
- @SpaceYaMagari
- @TDIplug
- @Caradvicekenya
- @alexmwanzo
- @Kevoh_254
- @MpgKe
- @esnahmoraa
- @GSaruni
- @Stan_Subru
- @SangKip4
-@joshuasultanPT
-@samatimemagari
- @VanillaCars
For #SpaceYaMagari and #ThreadYaMagari
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.