#FAHAMU: UGONJWA VIDONDA VYA TUMBO
Ni ugonjwa unaopelekea ukuta wa tumbo kuvimba (inflammation) au kulika (ulceration) kutokana na kiwango cha asidi kuzalishwa kwa wingi tumboni.
Tatizo hili niweza kusababishwa na sababu mbalimbali kama....
• Kunywa pombe,
• Kuvuta sigara,
• Mkazo/msongo wa mawazo (stress)
• Kuungua mwili (curling ulcer)
• Kuumia kwa ubongo hupelekea 'Cushing ulcer',
• Matumizi ya dawa za maumivu (NSAIDS) kama diclofenac, ibuprofen kwa muda mrefu
• Gastrinoma; uvimbe unaozalisha ASIDI
• Maambukizi ya bakteria aina ya HELICOBACTER PYLORI. Huyu ni bakteria ambaye anaambukizwa kwa njia ya kula chakula/matunda,/kachumbari au kunywa kinywaji yenye mdudu huyo.
Kuna aina kuu mbili za vidonda vya tumbo; vidonda kwenye ukuta wa mfuko wa chakula (gastric) na duodenal
BAADHI YA DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO NI;
• Maumivu ya tumbo kama moto; baada ya kula kwa mwenye gastric ulcer na kabla ya kula kwa mwenye duodenal ulcer. Muda mwingine maumivu kuelekea mgongoni.
• Kujihisi mchovu hasa kwa vidonda vilivyosababishwa na bakteria
• Kutapika damu
• Kupata choo chenye damu (hematochezia) au choo cheusi (melena). Hii hutokea hasa ikiwa vidonda vimetoboka.
JE, MAZIWA 'FRESH' NI TIBA?
Jibu ni HAPANA. Maziwa hayatibu kabisa vidonda vya tumbo bali huleta nafuu ya muda tu. Na hatushauri matumizi ya maziwa kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo kwani hupoza kwa muda na kuchochea uzalishwaji wa ASIDI kwa wingi zaidi na hivyo kuongeza tatizo
TIBA YAKE NI NINI?
•Hutegemea na sababu iliyopelekea. Huweza kuwa dawa za kupunguza kiwango cha asidi tumboni au mchanganyiko wa damu kwa ajili ya kuua wadudu.
• Epuka vyakula/vinywaji vinavyopelekea uzalishwaji wa ASIDI kwa wingi. Mfano, vyakula vyenye wanga sana, dagaa n.k
Pia kuacha vinywaji vyenye gesi kwa wingi (carbonated drinks) kama soda n.k
USHAURI
• Kama una dalili za ugonjwa huu nenda hospitali mapema kwa uchunguzi na matibabu,
• Epuka pombe, sigara, stress n.k
• Fuata ushauri wa wataalamu.
RETWEET KWA WENGINE KUJIFUNZA...
*dawa not damu
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.