Nini kinaendelea SRILANKA..?
Uzi🧵
#Trustory labda umeshaona story nyingi kuhusu SRI LANKA na labda hujui tumefikaje hapa na ndiyo sababu unasoma hapa,au unajiuliza hivi nchi inawezaje ku collapse kiasi cha kukosa hela?kwanza nchi inakosaje hela?inamaana noti zimepotea?
Mwingine hata huelewi SRI LANKA yenyewe ndo wapi. So twende nikupe historia simpo yenye MASUALA Mazima ya uchumi ndani yake. Sri lanka ni kisiwa kipo kusini mwa INDIA zamani sana inasemekana kulikuwa na barabara kabisa kutoka INDIA hadi SRI LANKA ya sasa
lakini #Trustory maji yalifukia hilo eneo na sasa wana mpaka wa kwenye maji,ni sawa na kusema SRI LANKA zamani ilikuwa #peninsula na sasa ni kisiwa, ukiangalia watu wake wanafanana na jamii ya wahindi.Ushaskiaga wahuni wanaitwa Tamil Tigers?
Yes hawa waasi waliotaka kujitenga walihit sana miaka ya nyuma,kutokea jamii ya wa TAMIL ambao walikua wanaonewa sana na serikali so wakakinukisha kutaka kujitenga waunde taifa lao.
Ni nchi ambayo mwenzi march mwaka huu ilifikia kuahirisha mitihani ya taifa kwenye shule za miji kadhaa kwasababu serikali ilikosa karatasi na wino wa kuchapisha mitihani,so wanafunzi wakala bata.Kama ulikuwa hependi mitihani labda utatamani enzi zako yangetokea ya SRI LANKA
lakini ni zaidi ya uwazavyo ,kila kitu kilipanda bei mara dufu,(unajua maraDufu wewe?) kuanzia mafuta, mchele,dawa za binadamu na Umeme unakata kwa saa 15 kwa siku, kudadadeki(in haji manara’s voice)
Hali ya maisha imekuwa ngumu kiasi cha kuwaleta pamoja watu wa dini zote
wakristo,waislam,wahindu,Budha na wasio na dini ambao miaka 10 nyuma walikuwa wanapigana wenyewe kwa wenyewe,leo wameungana kuingia mitaani kukinukisha dhidi ya serikali. Wahuni wameandamana hadi kwenye makazi ya rais na wanapiga mbizi kwenye swimming pool la rais
na rais ameamua kusarenda na kusema anaachia ngazi.
Shida ya SRI LANKA inazunguka ndani ya familia 1 ama ukoo wa mzee RAJAPAKSA ,hii ni familia ambayo imekuwa ikiongoza sri lanka kwa miaka 20 sasa,undugu-naization wao ndo unadaiwa chanzo cha kuiingiza nchi kwenye madeni
yasiyolipika na uchumi wake umecolapse kwenye kiwango cha kushindwa kununua karatasi za mitihani.Serikali imejaa ndugu ambao wanalaumiwa kwa upendeleo a.k.a undugu-naizesheni ,rushwa na matumizi mabaya ya ofisi.
Mahinda Rajapaksa ndiye aliyeanzisha safari ya undugulaizesheni aliingia kwenye urais 2005-2015 na wakati huu alihakikisha kila ndugu yake ambaye alikuwa na ‘potensho’ ya uongozi alipata nafasi nyeti serikalini,wakatafuna nchi na mwaka 2015 ndo wananchi wakaamua kuchagua
‘PIPOZ PAWA’ YAO akaingia madarakani kiongozi wa chama pinzani
MAITHRIPALA SIRISENA akaingia white house.Hata hivyo hakuna maajabu, miaka 4 mbele 2019 ukafanyika uchaguzi akapigwa chini, na aliyeshinda ni GOTABAYA RAJAPAKSA ,ambaye ni mdogo wake na Mahendra RAJAPAKSA
aliyekuwa rais before,so familia ikarudi madarakani.GOTABAYA alipoingia ofisini akafanya uteuzi, jopo lake la mawaziri likiongozwa na waziri mkuu na gues what,akamteua MAHINDA kuwa waziri mkuu wake,yaani aliyekuwa rais kwa miaka kibao amerudi kuwa waziri mkuu
Unaweza kushangazwa na hili ukiwa Africa au pengine, lakini kumbuka SRI LANKA ina historia ya kuongozwa na KILE WANAITA Dynasty(Familia inaongoza nchi) km unavyoona korea, Japan na bara la ASIA kiujumla.Uarabuni wanaita Emirates.
Akamteua mwanaye wa kiume kuwa waziri wa michezo,na kifupi uwe shemeji,binamu nyama ya hamu au yeyote unayehusiana na familia ya RAJAPAKSA ujue mashavu yapo nje nje.Ukumbuke miaka yote wanachaguliwa kwa kura na mifumo ya kiserikali lakini undugulaizesheni umefanya imeonekana
kama SRI LANKA ni serikali ya familia. Both GOTABAYA na MAHINDA wanalaumiwa kwa hapa tulipofikia kwasababu mbalimbali.Kuelewa kilichotokea SRI LANKA, kiliwahi kutokea UGIRIK. Ni kitu real kwamba uchumi wa nchi unaweza kucolapse ndiyo maana kila nchi ina watalam wa uchumi
na taasisi zinazodeal na mambo hayo.Hii itakupa kuelewa uchumi wa nchi yyte unavyofanya kazi.Mzunguko wa uchumi wa nchi yoyote una sura au makundi 2.Nchi inapokuwa ina IMPORT zaidi, yaani inanunua VITU nje kuliko inavyotoa ndani kupeleka nje (export) wanaita TRADE DEFICIT.
Nchi ambayo wana EXPORT vitu kuliko wanavyo IMPORT inaitwa TRADE SURPLUS .Kwa harakaharaka tumezoea hutakiwi kutumia kuliko unachoingiza, lakini kwenye uchumi ni complicated kidogo.Mfan MAREKANI wana DEFICIT kubwa kinoma,yaani wanaingiza bidhaa nyingi kuliko wanazouza nje,
Lakini JAPAN wana SURPLUS KUBWA yaani wanauza nje kuliko wanavyoingiza ndani, Sri Lanka ni nchi iliyokuwa kwenye kundi la TRADE DEFICIT yaani wanaagiza vitu vingi kutoka nje.Nchi za aina hii zipo nyingi duniani sio kitu kigeni wala kibaya kivile,shida ni kinapokosa balancing
so pesa ya kigeni ilihitajika kwenye mzunguko muda wote.Kwa kesi ya Marekani wao ndo Center ya pesa ya kigeni yenyewe na wana sera zinazoilinda Dola na mzunguko wake unafanya dola kuwa pesa inayoaminika msimamo wake sokoni.Ndio maana USD ni SI UNIT ya pesa nyingi duniani.
Kifupi Biashara duniani inafanyika kwa DOLA ya kimarekani (USD).Na haijatokea bahati mbaya,niliwahi kukwambia KIHISTORIA kwanini USD ndo pesa inayotumika zaidi duniani.
Kwahiyo tunaposema pesa za kigeni mara nyingi ni ile ambayo inapokelewa sehemu kubwa duniani ambayo nchi husika
inategemea kupata bidhaa hizo. So ni dola ya kimarekani.Sri lanka wanaimport dawa,mafuta yote,vyakula na mambo kibao.Kinachofanyika kwenye nchi za aina hii ya uchumi ambao unahitaji PESA nyingi za kigeni, hukopa pesa za kigeni ili ziwepo kwenye hazina kuu.
Wakati waziri mkuu MAHINDA alikuwa rais alianzishaga miradi mingi ya miundombinu ambayo iliishia kufeli so hela zilizotumika hazijawahi kurudi kwenye mzunguko.Mbali na hilo rushwa ilikuwa nyingi serikalini.Alijenga majengo makubwa kwa nia ya uwekezaji na biashara lakini
hawakupata walichotarajia,akajenga kiwanja cha cricket ,akatanua bandari na kote alipowekeza return ilikuwa ndogo,ana skendo ya kupoteza zaidi ya BILIO 87 za kitanzania kwenye ujenzi wa barabara na hazikuonekana zimepitia chocho gani.
Hiyo skendo ilikuja kuwekwa wazi baadaye kwamba alikua ameandaa hadi majeshi kufanya mapinduzi,jamaa anapenda madaraka kuliko kula, alipomaliza urais akagombea ubunge wa eneo linaitwa KURUNEGALA na akarudi bungeni kama mbunge. Ni rais wa kwanza kufanya hivyo.
Hopefully umepata mwanga, hii kama intro tu #PichaLINAENDELEA madudu mengi sana kutoka kwenye hii familia.
Usikose kutuskiliza kila jumamosi kuanzia saa 9 alasiri mpaka saa 10 jioni kupitia @earadiofm
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.