Coxstore ο£Ώ Profile picture
πŸ‘¨πŸΏβ€πŸŽ“ Comp Engineer |Laboratory scientist UDSM | Tech Reviewer | Found by Jesus Christ,

Jul 30, 2022, 12 tweets

πŸ¦…VITU VYA KUFANYA ILI KUOKOA MATUMIZI YA BANDO KWENYE SIMU!
πŸ“šπŸ“šπŸ“š

Kuisha haraka kwa internet Bundles imekuwa ni malalamiko ya wengi, lakini pia unaweza kufanya settings kadhaa kwenye simu yako kuokoa bundle kuisha haraka
Twende pamoja hapa chini πŸ‘‡

#ElimikaWikiendi

Tuanze na simu za android then nitamalizia na iphone

ANDROID
1.Zima accounts syncing

Baadhi ya apps kama Facebook, Google Fit data, Google Play Movies, na Google Play Music ambazo mara nyingi wengi wetu hua hatuzitumii

#ElimikaWikiendi

na kila muda kama ziko on zinakua zinatumia data na
battery pia kufanya updates kati ya simu yako na server,namna ya kuzima nenda settings >accounts then Zima syncing ya apps ambazo muda mwingi hua huzitumii kama inavyoonekana hapo juu

#ElimikaWikiendi

2.ZUIA automatic updates ya apps

Moja kati ya settings inayokula internet bundle bila wewe kujua ni hii maana inakua inafanya updates mpaka kwenye apps ambazo hua huzitumii badilisha settings na uweke kwenye kutumia wi-fi kufanya updates

#ElimikaWikiendi

Kufanya hilo nenda Settings >>Auto-update apps na uweke option ya Auto-update apps over Wi-Fi only au wakati mwingine unaweza chagua Do not auto-update apps kama hutaki hata ku update app zako mara kwa mara ,il option nzuri ni ku update kupitia wi-fi

#ElimikaWikiendi

3.Tumia data compression kwenye Chrome

Hii ni inbuilt feature kwa watumiaji wa chrome ambayo inasaidia kupunguza traffics na kukuzuia kwenda kwenye malicious sites mfano hapa chini unaona kwa mwezi imeweza kuokoa 17% ya bando

#ElimikaWikiendi

Kufanya hivo bonyeza doti tatu za kulia juu ya chrome then settings >data server na baada ya hapo utaona kabisa matumizi yako ya bando yamepungua

#ElimikaWikiendi

4.Zuia background activity za apps

Kuna apps zingine hua zinatumia data hata kama simu huitumii au wakati una multitask,kikawaida background activity ni kawaida kwenye simu kwa mazingira mazuri ya app ila kama unataka kuokoa bando unaweza kuzuia

#ElimikaWikiendi

Kwa kwenda Settings >>Restrict data usage kwenye app ambayo unataka kuzuia ulaji wake wa bando

Sasa twende upande wa watumiaji wa iphone

#ElimikaWikiendi

1.Disable background app refresh

Hii inasaidia kuzuia activity zote ambazo hua zinafanyika hata wakati hutumii simu mfano feeds zote za kwenye social networks au WhatsApp,kupata feeds inakua ni mpaka uifungue app husika

#ElimikaWikiendi

2.Ruhusu low power mode

Ukiruhusu low power mode inasaidia kuzuia task zote ambazo hua zinafanyika background mfano syncing ya picha na videos kwenye icloud ambayo hutumia MB nyingi sana

#ElimikaWikiendi

3.3G/4G

Unaweza amua ku switch kwenda 3G kutoka 4G LTE ambayo hua inasaidia kupunguza matumizi ya bando

3G -hutumia mpaka 7mb kwa sekunde na wakati huo 4G hutumia mpaka 20-40mb kwa sekunde kama mtandao umetumika

#ElimikaWikiendi ✌️

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling