👨🏿🎓 Comp Engineer |Laboratory scientist UDSM | Tech Reviewer | Found by Jesus Christ,
Sep 26, 2023 • 9 tweets • 4 min read
🦅HATUA ZA AWALI ZA KU TRACK SIMU ILIYOPOTEA
PART 1
🧵🧵🧵!
hizi hatua za awali za namna ya ku track simu ni muhimu kwa kila mtu kuzipitia maana unaweza poteza simu au unaweza kutana na mtu amepoteza simu ukamsaidia,hizi mara nyingi hufanya kazi kama simu imeibiwa muda mfupi uliopita
1.Find my device(Google)
hii app i download kutoka playstore na kama hauja register simu yako fanya ku register credentials zako au pia nenda settings>security>turn on ile option ya remotely locate this device kama inavyoonekana hapa chini
sasa ikitokea umepoteza simu yako fanya
Aug 25, 2023 • 5 tweets • 2 min read
🦅CODE ZA KU BLOCK SMS &SIMU ZINAZOINGIA AMA KUTOKA BILA YA MTUMAJI KUJUA.
⚡️⚡️⚡️⚡️
Unaweza ukazuia simu ama sms zinazoingia kwenye simu yako ama zinazotoka kutokea kwenye simu yako
1. *35*0000*11 #
Hii code inazuia simu zote zinazoingia ama zinazopigwa kutokea mtandao wowote
Namna ya kuitoa hio code baada ya ku set ni kubonyeza tena code hii # 35*0000*11 #
2. *33*0000*11 #
Hii ni code kwaajili ya kuzuia simu kutoka au kupiga,hii nzuri unamsetia mtoto au mdada wa kazi kama anapenda kuongea ongea na simu usiku 😀
Hii unaitoa kwa # 33*0000*11 #
Aug 23, 2023 • 4 tweets • 1 min read
🦅KABLA HUJANUNUA SIMU USED
TUMIA HIZI CODE KUIHAKIKI !
🧵🧵🧵
Hizi simu used kabla hujainunua hakikisha unainunua kwa mtu unaye mwamini na hakikisha anakupa na original box halafu tumia hizi code hapa chini kuikagua
1.anza kwa kuivhunguza simu yenyewe battery 🪫 yake hali ya simu kwa ujumla na takwimu za kutumika kwake kwa kutumia code hii *#*#4636#*#*
2.Baada ya kumaliza kuicheki simu kama simu hakikisha unaifanyia factory reset ili kujua kama imekua bypassed ama imekua rooted *#*#7780#*#*
May 24, 2023 • 6 tweets • 2 min read
🦅KUJUA KAMA iphone YAKO NI ORIGINAL IPIME KWENYE HIVI VITU VITANO (5)
🧵🧵🧵!
Leo nataka nikupe tips muhimu tano tu ,kujua kama simu unayotumia ni genuine na imekua designed kutoka pale Cupertino ,California steve job’s theater 🎭 au ndo imekua assembled China uswahilini 😀😀
1.Check battery health yako kama inaendana cycle counts 😎 simu original sensor zake zimewekewa limit kiwango flani cha ku miss behave ukipiga hesabu ukapata 80% na battery yako ni 79% hio sio mbaya maana haiko mbali sana,soma uzi wake zaidi kwenye pinned tweet yangu
Aug 27, 2022 • 11 tweets • 5 min read
🦅KINACHOTOKEA WAKATI WA KU BOFYA NA KUSAMBAZA LINK ILI KUPATA ZAWADI📚
Kuna links nyingi sana ambazo hua watu wanaambiwa ku share na watu labda 10 au kwenye baadhi ya ma group ya WhatsApp ili kujishindia zawadi au kupata udhamini wa kusoma nje ya nchi
#Elimikawikiendi
Links hua zipo nyingi sana kuna zingine ni kujishindia simu flani mpya iliyotoka wakati huo,gari ya thamani,kwenda kutizama mechi ulaya live,au kampeni zingine ni kuataka kutabiri namna mtoto wako atakavyokua ama zingine kutabiri utakua tajiri kiasi gani moja kati ya kitu ambacho
Jul 30, 2022 • 12 tweets • 6 min read
🦅VITU VYA KUFANYA ILI KUOKOA MATUMIZI YA BANDO KWENYE SIMU!
📚📚📚
Kuisha haraka kwa internet Bundles imekuwa ni malalamiko ya wengi, lakini pia unaweza kufanya settings kadhaa kwenye simu yako kuokoa bundle kuisha haraka
Twende pamoja hapa chini 👇
#ElimikaWikiendi
Tuanze na simu za android then nitamalizia na iphone
ANDROID
1.Zima accounts syncing
Baadhi ya apps kama Facebook, Google Fit data, Google Play Movies, na Google Play Music ambazo mara nyingi wengi wetu hua hatuzitumii
🦅UMEWAHI KUJIULIZA NAMNA AMBAVYO FAST CHARGERS HUFANYA KAZI ?
📚📚📚
Hivi umewahi kujiuliza kwanini ukiwa unatumi fast charger ina charge simu kutoka 0%-80% kwa speed sana 🥺 then baada ya hapo inakua tu na speed ya kinyonga ?
Sio kila charger ni fast charger ,na sio kila smartphone ina support fast charging pia kuna simu zingine inaweza ikawa ina support fast charging lakini kufanya kazi ni mpaka option ya fast charging ui turn on
Apr 11, 2022 • 8 tweets • 2 min read
🦅ZIJUE SECRET CODES ZINAZO SAIDIA KUTAMBUA KAMA SIMU NI FAKE AU LAA!
USSD codes-uninstructured supplementary service data(ussd) ni code za siri ambazo unaweza kuzitumia kugundua baadhi ya features ambazo zimefichwa kwenye simu,na mara nyingi simu ambazo sio genuine hua
zinakataa baadhi ya codes,codes hizi ni kwaajili ya watumiaji wa vifaa vyenye operating system ya android tu
1.*#*#7780#*#*
Hii ni kwaajili ya kufanya factory reset ,kufuta apps zote na accounts zote kwenye simu na kuirudisha simu kama mpya ulipokua unaitoa kwenye box
Apr 9, 2022 • 8 tweets • 2 min read
🦅VITU 6 VYA KUZINGATIA KABLA HUJANUNUA SIMU USED
⚡️⚡️⚡️⚡️⚡️⚡️
Simu used huwavutia watu wengi sana,kutokana na bei zake kua cheap na kuwa na uwezo ule ule kama simu tu mpya!
Kabla hujafanya maamuzi ya kununua simu yeyote used zingatia haya 👇👇
1.Epuka simu za wizi
Polisi kuna kesi nyingi sana za wizi wa simu,na asilimia kubwa ya watu wanaokamatwa sio walio iba ila wameuziwa simu za wizi, kuepuka hili hakikisha anaye kuuzia anakupatia risiti aliyonunulia au boksi la simu lenye IMEI namba za hio simu
Apr 8, 2022 • 4 tweets • 2 min read
🦅UMEIBIWA SIMU NA HUKUMBUKI IMEI NUMBER UFANYE NINI:
⚡⚡⚡⚡⚡⚡⚡
inaweza kutokea ukapoteza simu yako na ukawa hukumbuki IMEI number yako ,either risiti au boksi navyo umepoteza,ukiwa na IMEI number itawasaidia polisi kuweza kujua ni laini ipi imewekwa kwenye simu yako uliyo
Ibiwa ,namna ya kufanya ili uipate imei namba yako
1.hakikisha unakumbuka gmail yako na password yake ,download apllication inaitwa find device kutoka play store,baada ya ku install kwenye simu nyingine inatakiwa u sign in kama guest kwenye hio simu nyingine
Mar 28, 2022 • 4 tweets • 2 min read
🦅DALILI ZA CAMERA AMBAYO NI NON GENUINE(sio original)
⚡️⚡️
Kabla hujafanya maamuzi yeyote yanayohusiana na simu ,fanya kupitia page yetu hapa itakusanua na mambo mengi sana ambayo ulikua hujui
Namna ya kucheki camera ya iphone yako kama ni original au laa
Au mfano ulikua umevunja camera yako kwa bahati mbaya na ukaenda kwa fundi kubadilisha camera 📷
Dalili muhimu za camera ambayo sio original
-camera hai focus vizuri picha haziko sharp
-unapokua unatumia portrait mode subject inakua haipo in focus au inakua focused nusunusu
Mar 27, 2022 • 5 tweets • 2 min read
🦅UKIBADILISHA SCREEN YA iphone YAKO HAKIKISHA FUNDI ANAIRUDISHA NA True Tone
⚡️⚡️
True Tone hii ni sensor muhimu sana inapatikana kuanzia iphone 8+ na kuendelea inafanya kazi ya kubadilisha mwanga wa simu kutokana na mazingira uliyopo ili kulinda afya ya macho yako 🙄
🧵
Mara nyingi true tone hua haipo kwenye vioo vinavyouzwa madukani hua ipo kwenye kioo original kilichokuja na simu yenyewe,na ndio maana ikitokea umebadilishiwa kioo na fundi ambaye sio mwelewa true tone hua inatoka na hairudishi
Ukimaliza kubadilishiwa kioo chako nenda
Jan 29, 2022 • 5 tweets • 3 min read
MATATIZO YA MARA KWA MARA KWENYE ANDROID TVS(Televisions)NA NAMNA YA KUYATATUA.
Kama tulivyo elezea kwenye nyuzi nyingi zilizopita ni android tv kua na uwezo wa ku support play-store na wakati huo smart haina uwezo huo ,
Matatizo ya android tv ni kama
1.KUJIZIMA MARA KWA MARA
Kama Tv yako hua ina tabia ya kujizima na kujiwasha kila mara hii yaweza kua ni settings kwenye day dream na screen saver unacho takiwa ni ku turn off hizo settings kama likiendelea basi fanya factory reset ya Tv yako
Jan 26, 2022 • 9 tweets • 4 min read
VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA KABLA YA KUFANYA MAAMUZI YA KUNUNUA TV(Television )📺 !
Kutokana na uzi nilio andika jana kua na maswali mengi sana juu ya vitu kama smart tv,Android tv,UHD,FHD,4k,8k leo nitajubu maswali mengi sana kwenye huu uzi shuka nami 🧵 1.SMART TV AU ANDROID TV
Hapa nitakupa utofauti kati ya smart tv na android tv then wewe ndio utafanya uamuzi uchukue ipi.
Smart Tv -ama kwa jina jingine wanaita internet TV ni Tv yenye uwezo wa kuunganishwa na internet na hufanya kazi kuikaribia sana smartphone
Dec 30, 2021 • 11 tweets • 3 min read
👨🏿🎓TEKNOLOJIA 5(tano) ZILIZOLETWA NA UJIO WA COVID-19 DUNIANI .
Ujio wa Covid-19 duniani unalazimisha idadi kubwa ya nchi kuanza kutumia teknolojia tano(5) muhimu ambazo zina athiri utendaji kazi wa watu moja kwa moja huku idadi kubwa ya ajira tulizo zizoea zikipotea ifikapo2025
Jitahidi kuzisoma hizi nyuzi maana zimebeba mambo muhimu sana yatakayo kusaidia kufanya maamuzi mazuri juu ya skills gani unatakiwa kuwa nazo na ni fani gani umshauri mdogo wako au mtoto wako ama ndugu yako ambazo zitakua na soko miaka ijayo
Zifuatazo ni Teknolojia 5 muhimu
Dec 29, 2021 • 4 tweets • 2 min read
LIST YA SIMU MPAKA SASA (29 DEC 2021)
ZINAZO SUPPORT eSIM Technology
👨🏿🎓
Kwa ambao watapenda kutumia teknolojia hii mpya 1.Apple
-iPhone XR (model A2105 kuanzia 2018)
-iPhone XS (model A2097 kuanzia 2018)
-iPhone XS Max (model A2101 kuanzia 2018)
-iPhone 11
A2221 kuanzia 2019)
-iPhone 11 Pro (model A2215 kuanzia 2019)
-iPhone SE (model 2020)
-iphone 12 mpaka iphone 13promax
2.Samsung
-samsung galaxy S20 mpaka S22 ambayo itakua released mapema January 2022
-samsung note 20
-samsung note 20ultra 5G
Dec 29, 2021 • 5 tweets • 2 min read
UJIO WA Teknolojia YA kutotumia tena laini za simu 💡eSIM 👨🏿🎓
Moja kati ya safari fupi sana zilizobaki ni utumiaji wa laini za simu kwa maana ya micro SIM na Nano SIM,
Leo nitakupa uzii kwa lugha nyepesi kabisa upate kuwa na ufahamu juu ya eSIM na faida zake pia
Utofauti wake na SIM cards ,
Kwanza kabisa kirefu cha SIM ni subscriber identity module card ambayo ina uwezo wa kujifadhi namba za simu,IMSA na keys 🔑 zake ambazo kwa ujumla husaidia kuwatambua wateja wa mtandao husika !
Sasa tukija upande wa eSIM yenye kirefu cha
Dec 28, 2021 • 5 tweets • 2 min read
UKWELI KUHUSU TWS EarBuds
Hivi karibuni kumekua na brand nyingi sana duniani zimeweza kutengeneza TWS earbuds kwa majina tofauti tofauti pia mfano ,
-inpods
-airdots
-macaron
-Airpods
-TWS i..
Brand zote hizo pamoja na utofauti wa majina lakini zote zimela
zimika kutumia Teknolojia ya bluetooth sasa kuna kampuni nyingi duniani ambazo zinatengeneza Bluetooth chipsets models na ni vigumu kuzijua kwa kuziangalia muundo wake wa nje mpaka pale ambapo umezipasua kwa ndani ukiangalia vizuri kwenye PCBA kunakuaga na herufi
Nov 14, 2021 • 7 tweets • 2 min read
ZIJUE AINA ZA SCREEN PROTECTORS ZA SIMU NA UBORA WAKE.👨🏿🎓
Kuna ka uoga flani hua kanakujia baada ya kuiangusha smartphone yako,hii sio tu inaleta uoga lakini inapunguza thamani ya simu pia lakini haya yote unaweza kuepukana nayo kwa kuchagua screen protector yenye ubora wa kulind
a simu yako
Zifuatazo ni Aina za Protectors nimezipanga kutokana na ubora wake.
1.Tempered glass screen protector
Maana ya glass kua tempered ni glass yenyewe kupitishwa kwenye joto kali na kuchanganywa na kemikali muhimu ambazo zinaongeza uimara wa glass kuhimili mgandamizo