Madinidotcom Profile picture
Show ya radio kwa #TAARIFANaMAARIFA kila wiki.Tunajadili ya dunia kwa lugha rafiki na nyepesi. kila Jumamosi 9alasiri - 10jioni Eastafrica Radio..Subscribe👇

Aug 23, 2022, 37 tweets

SAKATA LA BILIONEA JEFF BEZOS NA KING SALMAN WA SAUDIA.

Did you know unaweza kuhack an Iphones? Unafahamu ndicho chanzo cha tajiri namb 1 duniani Jeff Bezos kuachwa na mkewe?unafahamu aliyefanya hilo tukio ni King Salman kiongozi wa Saudi Arabia? #PICHALINAANZA

Kuna imani kwamba iphones zina strong security ni ngumu kuichezea,yes inawezekena bhanaa lakini kudakwa ni njenje.Sasa hacking inahitaji vitu flani ambavyo sometimes ni teknolojia ghali au lazima uwe na connections kali .
Juzi kati ikatangazwa BREKING NYIUZ

WhatsApp imeishtaki kampuni flani inayodevelp computer programs kutoka Israel. Sababu inashtumiwa kumpa Paul Kagame wa Rwanda program ya computer iliyowezesha kudukua "WhatsApp conversation” za wapinzani wa serikali ya Rwanda wanaoishi uhamishoni wanaojiita 'wanaharakati'

na hii kusababisha msala wa kupotea kwa wahusika kwenye Party ya kimyakimya.
Hii taarifa iliripotiwa na BBC na haikujadiliwa sana,lakini kuna mwanangu wa IT aliniambia its really hard kudukua maongezi whatsapp sababu database ziko strongly encrypted na location wise ziko mbali.

Trustory kuna program Rwanda inadaiwa wanayo inayowezesha kudukua mawasiliano ya wapinzani wa serikali tena walioko nje ya Rwanda ili kujua mikakati inayoendelea na nini wanapanga!
Baada ya almost 5 yrs za kudukuliwa na wapinzani kuanza kufa nje ya Rwanda na walikuwapo ndani,

WhatsApp wakasema "ngashtuka machale kundesa" something is wrong somewhere, kupeleleza ndo wakagundua its security walls are not strong kiiivo.Ukuta wao wa ulinzi kidigitali waliohisi ni mzito kupenya risasi ,kumbe wahuni wanajua jinsi ya kuutekenya na kutoboa kwa bisibisi.

Ukiskia INKRIPTED au SEKIYURITI WALL unaweza jiuliza ndo nini?Well,utaelewa soon acha ninukuu sehemu ya taarifa hii kutoka #BBCSWAHILI ya Tar 9november 2019 .
"WhatsApp imeishutumu Kampuni ya NSO Group kwa kuweka programu kwenye simu karibu 1,400 kwa nia ya kufanya upelelezi...

"Programu yake ya Pegasus inaweza kufanya kazi hiyo hata ikiwa mbali.
Idadi kubwa ya watu wanaofuatiliwa wanadaiwa kuwa raia wa Rwanda.
Kampuni ya NSO Group imekana madai dhidi yao, ikisema kuwa programu ya Pegasus imekuwa ikiuzwa kwa wateja waliohakikiwa na si wenye nia mbaya"

Yes,Hiyo program PEGASUS na utajiuliza kwani inafanyaje kazi?na INKRIPTED MESEJI ndo nini?Well,ukifungua whats app kwenye simu yako,kwenye kila mtu uliyechati naye,utaona pale juu kuna maandishi fulani yanasomeka messages and calls in this chart are end to end encrypted.

Kuna vimaneno vingi kwa lugha ya yai,lengo likiwa kukuhakikishia kwamba UPO SALAMA na kwamba hata wao Whats app wenyewe,hawana uwezo wa kusoma Meseji zako.Hii inafanyaje kazi?Well,Hii ni teknolojia ambayo iligunduliwa juzi kati.Kuielewa zaidi fuatilia hapa audiomack.com/madinidotcom/s…

Ndio maana whats app wamekuwekea kwa kujiamini hiyo meseji kwenye kila convo kwamba UPO SALAMA.CHA KUSHANGAZA ni baadaye Whats hao hao wanaibuka na kulalamika kwa Izrael nchi ya ahadi acheni umang’aa, kuna wahuni wametupiga na kitu chenye ncha kali.

Means kuna wahuni wameweza kuzisoma hizo code na kuelewa zimebeba nini.
Wahuni wenyewe wanapatikana kipande cha NCHI YA AHADI Israel,kampuni mtuhumiwa ni NSO GROUP na tayari washafanya biashara na wameuza hiyo UARABUNI na AFRICA na mnunuzi ni jirani yetu.

Tho rais paul kagame alikanusha lakini akasema anatamani angekua nazo awaonyeshe.Kagame alinukuliwa na bbc akijibu mchongo huu.
Virusi wa aina hii walianza kutumwa kwa simu za wahusika na Ndo Whats app kufuatilia zaidi hiyo virus aligorthim (ni kama fingure prin ya computer),

ikaonesha imetengenezwa Israel na jina la kampuni NSO grup ,hence whatsapp imefungilia kampuni hiyo mashtaka.Kama ulivyosikia wanasema wao kweli wana hiyo teknolojia lakini wanawauzia watu salama tu,so swali ni watu salama ndo kina nani?

Kwasabab kwa mujibu wa sheria nyingi duniani ni kitu kisichoruhusiwa kuhack mawasiliano ya mtu yeyote.Yaani kumfuatilia bila yeye kujua.
Wakati story ikiendelea kumbuka inapatikana youtube hapa

#PICHALINAENDELEA

Hata mahakamani huwezi kutumia ushahidi uliopatikana kwa njia ya udukuzi,ndio maana njia za kisheria hufanyika kwa makampuni husika kuombwa data za mtuhumiwa. So wengi wenye hofu kudukuliwa, hutumia whatsApp kuwasiliana mambo yao kwasabab ya hiyo teknolojia END TO END ENCRYPTION.

Uwepo wa program kama PEGASUS it means sio njia salama kiivyo.Hata hivyo program za kufanya kazi kama hizi sio hela ndogo.
Mpaka sasa TELEGRAM ndo unaotajwa kama mtandao salama zaidi wa kijamii kwasabab system yao haihifadhi data ya watumiaji popote pale.

So kinachosemwa kikifika kwa mhusika hakiachi ushahidi au copy popote kwenye internet labda wakutegee wakati mnawasiliana au kuchat .Hawa virusi ni codes maalum ambazo zinaweza kufikishwa kwenye simu au kifaa chako kwa njia mbalimbali.

Njia maarufu ni ya meseji(Social enginering hacking) na kuna ile ya kutumia vifaa kama Chaja ya simu,mtu anakubadilishia chaja ya simu,unapewa waya maalum ambao unafanana na chaja yako lakini una kazi zaidi ya hyo.utaelewa zaidi ukifuatilia series yetu👇 audiomack.com/madinidotcom/s…

Wakati rais Kagame anajibu shutuma hizi alisema hizi teknolojia ni bei mbaya sana,vinginevyo angeshakuwa nayo awafuatilie vizuri maadui wa rwanda.Kwenye taarifa ya BBC waliripoti.nanukuu angalia screenShot 👇

Mwisho wa kunukuu unagundua alikanusha kuwa nayo lakini maelezo yake yanaonesha anafahamu uwepo wa teknolojia ya aina hii na anaitamani.TUNAFIKA kwenye sakata lenyewe.Najua nimekuzungusha sana lakini lengo ni upate context nzima ya mada husika.

Sakata lenyewe ni hili..
BILIONEA on top 3 ya watu wenye mkwanja duniani, recently baada ya kupata hasara ya 0.7% drop kwenye shares za Amazon ndugu Jeff Bezos,hajakaa vizuri mawasiliano yake yakadukuliwa mpaka ikapelekea kuvunjika kwa ndoa yake na talaka juu.. #PICHALINAENDELEA.

Kutoka kwa mke wake wa zaidi ya miaka 20 MacKenzie Bezos iliyomcost matrillion ya hela hii ni sababu nyingine kwanini ameshuka pia.
Ikasemekana hela aliyopata huyu dada kwenye talaka hiyo imemfanya kuwa mwanamke tajiri wa nne duniani according to forbes.

Kwenye episode iliyopita tulizungumzia jinsi kampuni ya AMAZON inavyohusishwa na kuuza teknolojia hatari kwa idara za ulinzi za marekani na Israel,sasa boss mwenye kampuni alidukuliwa na kuvujishwa kwa information sensitive ikiwa ni pamoja na picha zake za koneksheni..

na message zake na mchepuko wake, na ndoa ikaishia hapo .by the way Bi.Mackenzie amepewa pia 4% ya shares za amazon ( natamani nikueleze thamani yake ila go google)Tusije kumuonea gere mama wa watu bure, alishiriki kuzitengeneza na wanasema marekani Talaka ni ghali kuliko harusi.

So kama ulisikia kuachwa kwa huyu bwana,shida ilikuwa hii hapa na picha halijaishia hapo.mpya zikaja baada ya uchunguzi mzitoo wa wapelelezi binafsi walioajiriwa na Bezos wamegundua kwamba aliyehack Iphone ya Bezos ni Muhammed Bin Salman The current CROWN PRINCE wa Saudi Arabia.

PICHA LINANOGA ,MBS alituma Message yeye mwenyewe kwa Bezos ikiwa na link ya viruses hao walifanikisha udukuwaji huo and the rest is history.Hizi ni zile link ambazo wala hawahitaji uzifungue ndo zikuathiri, ila ikishafika tu kwa simu yako,imeshakufungisha ndoa na wadukuzi.

Bin salman ni mtoto wa kifalme ambaye amekulia kwenye hela na mzee wa MATUKIO kwasababu ameponea chupuchupu kwenye ule msala wa mwandishi wa habari aliyeuwawa ndani ya ubalozi wa Saudi arabia uturuki Jamal Kashoggi.
Kulikuwa kuna mpaka ushahidi wa picha via CCTV.

Kashoggi akiingia kwenye ubalozi huo na hakuonekana akitoka, baadae ikasemekana aliuwawa mule ndani kwa orders toka kwa crown prince MBS.Lilikuwa sakata la kukata na shoka duniani but ikazimwa na mtoto wa Kashoggi alionekana ikulu na kupiga picha akipeana mikono na Salman.

Huyu Kashoggi ndo sababu ya kwanini MBS alifanya alichokifanya ,kuhack simu ya BILIONEA ambaye walikua washkaji wanaotembeleana.
Jamal Kashoggi ameingiaje hapa?

Kama nilivyokwambia walikuwa washkaji na kuna wakati walitembeleana na KING SALMAN alimwalika Bezos kwa mazungumzo,

ni kipindi ambacho gazeti la WASHINGTON POST ambalo linamilikiwa na Bezos lilikuwa linaandika makala za kuponda uongozi wake na impact yake ni kubwa duniani.Mwandishi alikuwa ndugu JAMAL KASHOGGI. So MBS alijua Bezos ana uwezo wa kumtuliza mwajiriwa wake anajifanya hausiki.

Akaona dawa ya mnafiki ni kumalizana naye kinafiki.
Ni kama Kondeboy alivyomshukutumu CHIBUDEE kuwaruhusu BABA LEVO na wenzake wanamtukana kila siku na wameajiriwa kwenye media ya CHIBUDEE ,so angeweza kumwambia aache .Nadhani mlimsikia ndugu jeshi akitoa ya moyoni.

baada ya mazungumzo yao,Bezos na King Salman walibadilishana namba na ndipo akamtumia file hilo la video ambalo lilipoingia tu kwenye simu ya Bezos mchezo ukawa umeisha.Baada ya siku kadhaa marafiki wa karibu wa Jamal Kashoggi walitumiwa kirusi kama hicho kwenye whats app zao

na siku kadhaa mbele Jamal Kashoggi akauawa ndani ya ubalozi wa Saudia.Baadaye iligundulika kudukuliwa kwa Marafiki wa karibu wa Kasshoggi kulisaidia sana kujua movement za kashoggi na hatari yake kwa utawala wa UFALME WA SAUDIA. So wakamuwahi

Before taarifa za kudukuliwa kujulikana na yeyote,Mr.MBS mwenyewe alimtumia JEFF picha ya mwanamke yenye maneno ya kuchekesha (meme) Ikisomeka.
“arguing with a woman is like reading the software license agreements,in the end you have to ignore everything and click “I agree”

Kwa kiswahili "kubishana na mwanamke ni kama kusoma vigezo na masharti kwenye software ,mwishoni itabidi uachane na yote na kubonyeza "nakubali"

Picha ya mwanamke iliyokuwa kwenye maneno hayo alikuwa ni mchepuko wa Jeff wa wakati huo na hakuna aliyekuwa anamjua.🧐🤠

UNGEKUWA JEFF ungefanyaje?🤠Umeona pia BIDEN juzi kasahau mauaji ya Kashoggi na kakutana na MBS sebuleni kwake.Sakata halijaishia hapo.Ifuatilie full story hii youtube .

Tulikuahidi #TaarifaNaamaarifa

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling