SAKATA LA MAUAJI YA RAIS WA CONGO.
🧵🔥
#PichaLinaanza Hili ni picha kuhusu tukio la kuuawa kwa rais wa Congo Laurent-Désiré Kabila,ni kama movie la kutisha lakini BASED ON TRU EVENT. Mwamba ambaye ni Stelingi wetu anaitwa RASHIDI MIZELE,baadaye mastelingi watabadilika.
hii ndio story,ambayo tulikugusia episode zilizopita za rais aliyeingia mkataba maarufu wa kuigawa Congo MKABA WA LEMERA.HADI leo Congo juzi kati imekubaliwa kuwa sehemu ya africa mashariki,ni nchi yenye historia nyeusi.Licha ya kwamba imebarikiwa madini...
ANZIA HAPA......agiza popcorn kabisa
Acha turewind mkanda ,Lets go back hadi siku ya TUKIO lenyewe la mwamba aliyempiga risasi kadhaa Rais wa nchini na akatoka zake mbio akitarajia kutoroka.Huyu ndo mwenye siri hii nzito ya KWANINI alimuua rais wa Congo Laurent-Désiré Kabila
ambaye alimuondoa madarakani Dikteta MOBUTU SESEKO.Hii ni kama RISE and FALL ya Lauraa Kabila rais wa 3 wa DRC.Stelingi wetu wajina wake Chid Benz ndugu RASHID MIZELE ambaye kabla alienda kama Rashidi Kasereka, mwamba ambaye alikua kati ya walinzi wa rais siku hiyo mwaka 2001
akala kitu chake cha Chuga,akasema “Bangi nibangue nigeuke rambo PAH PAH PAH!” kweli bwana mwamba akaamua kufanya tukio ambalo lilizaa kizazaa na fumbo kubwa hadi leo.Ehe,ilikuwaje?
Kwanza ujue huyu RASHIDI MISELE au tumuite CHID km ChidBenz,ni kijana wa miaka 18 tu wakati huu,
na tayari alikua ni mlinzi wa rais kwasabab alikua kati ya askari watoto waliotumika kuung'oa utawala wa dikteta MOBUTU. So licha ya kuwa hajauacha utoto sana kiumri, alishapitia mengi na alishakuwa na uwezo wa kufanya mengi.
Lkn jinsi alivyokua amepanga kutoroka ndo utaona utoto wake.
Emile Mota ndiye shuhuda wa 1 aliyekua karibu na eneo la tukio,huyu alikua mshauri wa uchumi wa rais Laurent Kabila ,siku hiyo Ilikua mwanzo wa mwaka January tar 16 mwaka 2001 ndani ya WHITE HAUS akiwa amekaa akipanga
..mipango flani.
Kulikuwa na mkutano ambao ilibidi ahudhurie unaitwa FRANCE AFRICA SUMMIT,so rais akamuita ndugu mshauri wake EMILE MOTA akamwambia ndugu MOTA amundalie list ya watu anaopaswa kwenda nao kwenye mkutano kama huo uliofanyika Cameroon .
Ghafla mlangoni akatokea mtu amefungua mlango,kucheki vizuri wakagundua ni kijana ambaye MOTA hakuwa anamfahamu kwa jina lakini alikuwa anamjua ni kati ya walinzi wa rais, bila shaka rais Kabila yey3 alimjua kwa jina kijana aliyesimama mlangon “OH Kumbe ni wewe” so akaonekana
kama anahitaji kuongea na boss. akakaribishwa rais akamwambia “Kuna nini mzee Chid ?karibu" Chid alipiga Salute kama kawaida kwa rais,wakati huo MSHAURI WA RAIS ankali MOTA akiwa anachukua notes za mazungumzo waliyokua wanaongea punde,akasikia risasi ya kwanza.
Hajakaa sawa akasikia nyingine.Chid akatulia kidogo akamuangalia akamuwasha nyingine.Jumla zikawa risasi 3 kisha akachomoka zake mlangoni mbio bunduki mkononi.
Hakuna aliyeamini kilichotokea.Ndugu Mota akili zikamcheza ghafla na akili zinamrudia ndo anaanza kutoka speed kusema
jamani huyu muhuni amempiga rais risasi,Wakati huo chid anatafuta njia ya kutokea kwa ile speed ya Harmorapa baada ya kuona ile bastola.
Hakupiga hatua mingi sana kuelekea alipokua anakimbilia,akatokea mwamba anaitwa Chiribagula mlinzi mwingine ikulu akiwa na mashine yake mkononi
akamuona CHID akiwa na ‘mguu wa kuku' yaani kile kitu alichokimbiaga harmorapa,alafu nyuma yake anasikia kelele za bwana Mota kwamba huyo bwana Chid amempiga rais risasi.Fasta ile ki-shoz niga CHIRIBAGULA akafyatua risasi ikampata CHID mguuni na akaanguka Palepale.
Muda uleule ndo anaibuka STELINGI WETU mwingine ambaye ndiye boss wa walinzi wote ikulu KANALI EDDY KAPEND akiwa na mashine yake mkononi,bila kuuliza chochote akamuwasha RASHID shaba za kushato na palepale ROHO ya ANKALI wetu CHID ikauacha mwili,
akageuka MWENDA ZAKE lakini mwendazake huyu akaiachia dunia maswali mengi ambayo waliyojua majibu hawakuwa tyr kuyatoa.
SAKATA la nani kapanga mauaji ya rais likaanza rasmi kwasabab jibu la NANI kaua lilijulikana tayari.CONGO ikazizima mipaka ikafungwa,mtaan kukawa kimya na hofu,
watu wakiwa hawajui WHAT NEXT.Rais kauawa. Alipofika mahakamani Chiribagula alisema lengo lilikua asimuue Chid na alimwambia Kapend amuache sababu atahitajika kusema aliyemtuma lakini ndugu KAPEND kwa hasira alimuwahisha Chid Akhera akiwa na siri zake.
Waliokuwa eneo la tukio wanasema rais alifariki palepale,ingawa serikali ilificha ikisema alikua njiani kupelekwa nje ya nchi.Lakini Trustory ndani ya muda mfupi tukawa tumepata WENDA ZAKE wawili ambao ni Rais wa nchi Laura Desire Kabila na muuaji wa rais wa nchi ankali CHID
Kitu moja muhimu kujua ni kwamba kiongozi OnTop wa nchi akiuawa popote,moja ya vitu MUHIMU ni LAZIMA awepo mtu au watu ambao wameshakamatwa kuhusu msala husika hashtag WabebaLawama,tena ndani ya muda mfupi.Tulikupa story ya kuuawa kwa rais wa HAITI nadhani tuko pmj
kamatakamata ya watu kibao, kwasababu hii ni ishara kwamba nchi ipo IMARA au active kiasi gani. Ni aibu kiongozi level kubwa auawe then siku zipite nchi haina majibu.
So waliobaki kutegua kitendawili cha NANI ANAHUSIKA ANANI AHUSISHWE HATA KAMA HAUSIKI ni wale waliobaki hai.
Hapa ndipo picha lilinoga.Nani muhusika?Nini kiliendelea? Itaendelea lakini pia unaweza Fuatilia full story iko YouTube
Tulikuahidi #TaarifaNaMaalifa
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.