#AfyaSwahili | MAMBO MUHIMU KUFAHAMU KUHUSU UGONJWA WA EBOLA.
--> Uzi huu ni muhimu kutokana na kuwepo kwa mlipuko wa Ebola katika nchi jirani na elimu ya msingi ni muhimu sana.
➡️Ebola ni ugonjwa unaotokana na maambukizi vya virusi.
➡️Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa ya mlipuko yajulikanayo kama homa za virusi ambazo huambatana kutokwa damu sehemu mbalimbali za mwili (Viral haemorrhagic fevers).
➡️Ebola ni ugonjwa hatari sana.
➡️Kwa wastani husababisha vifo kwa wastani wa nusu wa watu wote waliougua.
➡️Uwezo wa kusababisha vifo hutofautiana kati ya mlipuko na mlipuko kwa wastani vifo huwa 20% hadi 90% ya wagonjwa.
➡️Mlipuko wa kwanza wa ugonjwa wa Ebola ulitokea
karibu na mto Ebola huko Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.
➡️Hii ilikuwa mwaka 1976
NAMNA UNAVYOWEZA KUAMBUKIZWA EBOLA 1/2
Kutoka kwa Wanyama kwenda kwa binadamu
➡️Hii hupitia kugusa au kula nyama ya wanyama pori wenye maambukizi
NAMNA UNAVYOWEZA KUAMBUKIZWA EBOLA 2/2
Kutoka kwa mtu mwingine. Kwa
- Kugusa majimaji ya mwili (damu, jasho, matapishi,
mkojo, kinyesi, machozi nk.)
- Kugusa au kuosha maiti ya aliyekufa kwa Ebola
- Kuchangia vitu vyenye ncha kali
- Kufanya ngono na mtu aliyeambukizwa
HATUA MBALIMBALI ZA UGONJWA WA EBOLA
1⃣Kuumwa kichwa, misuli kuuma, homa
2⃣Homa kali, kutapika, kuzubaa
3⃣Kutoka damu kwenye mdomo, pua, macho,
damu kwenye haja kubwa, ini kushindwa kufanya kazi vizuri
4⃣Kupoteza fahamu, degedege
HATUA MUHIMU KUCHUKUA KUJIKINGA
➡️Osha mikono yako kwa maji tiririka na sabuni au tumia vitakasa
➡️Pika chakula chako ipasavyo
➡️Nenda hospitali ukiwa na dalili za homa, kuumwa viungo na misuli, kutapika, kuchoka nk.
➡️Elimisha wengine kuhusu Ebola
➡️Usiguse mtu mwenye dalili za Ebola
➡️Usiguse nguo, kitanda na vitu vya watu waliokufa kwa Ebola
➡️Usiguse damu, majimaji, mkojo, haja kubwa nk. kutokwa kwa mtu mwenye dalili za Ebola
➡️Usicheze na nyani, sokwe, nk.
➡️Usile nyama ya wanyama pori kama kuna mlipuko wa Ebola
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.