Dr. Norman Jonas Profile picture
Medical Doctor | Internal Medicine - Kilimanjaro Christian Medical University College | Always a Beautiful Day to Save Lives | norman.jonas@kcmuco.ac.tz
high fructose corn syrup Profile picture 1 subscribed
Oct 2, 2022 17 tweets 6 min read
#AfyaSwahili | OCTOBA - MWEZI WA UELEWA JUU YA SARATANI YA MATITI

➡️Uzi maalumu wenye jumbepicha ili kusaidia wanawake wapate kufahamu dalili za kansa

➡️Tafadhali sambaza isaidie wengi

Credit: Know Your Lemons

#BreastCancerAwarenessMonth ➡️Saratani ya titi ni kati ya saratani zinazowaathiri zaidi wanawake. (Namba 2 chini ya saratani ya shingo ya kizazi)

➡️Mwaka 2020 Tanzania kulikuwa na wagonjwa wapya 3992 wa saratani ya matiti (hawa ni wale waliofika kwenye vituo vya Afya) wengi huchelewa tiba

Uelewa ni muhimu
Oct 1, 2022 9 tweets 3 min read
#AfyaSwahili | MAMBO MUHIMU KUFAHAMU KUHUSU UGONJWA WA EBOLA.

--> Uzi huu ni muhimu kutokana na kuwepo kwa mlipuko wa Ebola katika nchi jirani na elimu ya msingi ni muhimu sana. ➡️Ebola ni ugonjwa unaotokana na maambukizi vya virusi.

➡️Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa ya mlipuko yajulikanayo kama homa za virusi ambazo huambatana kutokwa damu sehemu mbalimbali za mwili (Viral haemorrhagic fevers).
Nov 14, 2021 17 tweets 5 min read
#DondooZaDaktari | Leo ni siku ya ugonjwa wa KISUKARI duniani #WorldDiabetesDay

➡️Siku maalumu ambayo wanajamii tunaelimishana kuhusu tatizo hili la kiafya.

➡️Tatizo hili linaongezeka na moja ya kisababishi kikuu cha magonjwa ya figo,moyo, upofu na ulemavu wa kupoteza viungo. #KISUKARI NI NINI?

➡️Kisukari ni ugonjwa wa kudumu ambao hutokea pale kiwango cha sukari (glukosi) katika damu
kipo juu zaidi kutokana na kukosekana au mwili kushindwa kutumia homoni ya insulini

➡️Kiwango cha glukosi kikiwa juu kwa muda mrefu, husababisha madhara katika mwili
Oct 29, 2021 12 tweets 5 min read
#DondooZaDaktari | Leo ni siku ya #KIHARUSI #WorldStrokeDay

➡️Tatizo la dharura la kiafya ambalo ni moja ya magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo.

➡️Mitindo ya maisha na Lishe ni vitu vinavyochangia wagonjwa wanaopata stroke kuongezeka

➡️Kiharusi huacha ulemavu au kifo ➡️KIHARUSI hutokea pale seli za ubongo 🧠 zinapokufa kutokana kuziba au kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo hivyo kukosa hewa ya oksijeni na virutubisho.

➡️Kiharusi kikihusisha mshipa wa mkubwa wa damu kwa wastani mgonjwa hupoteza seli za ubongo (neuroni 1.9) kila dakika.
Oct 28, 2021 4 tweets 3 min read
#DondooZaDaktari | #USUGU WA #DAWA

➡️ #Antibiotiki ni dawa zinazotumika kutibu maambukizi ya bakteria.

➡️Usugu wa antibiotiki hutokea pale bakteria wanapotengeneza usugu dhidi ya aina flani ya dawa.

➡️USUGU hufanya dawa kushindwa kufanya kazi

#AntimicrobialResistance Matumizi holela ya dawa aina ya antibiotiki huchangia usugu wa dawa kutokea.

Bakteria wanapopata usugu husababisha
➡️Kutokupona ugonjwa hata baada ya kutumia antibiotiki ambazo zimekuwa zikitibu ugonjwa huo
➡️Kuongezeka kwa gharama za matibabu
➡️Kifo
Oct 27, 2021 4 tweets 2 min read
#DondooZaDaktari | Ugonjwa wa kisukari unaongezeka kwa kasi hata katika nchi zetu maskini.

✍️Kisukari hutokana na mwili kushindwa kutumia glukosi (sukari)

➡️Kisukari ndio sababu kuu ya:
- Kiharusi
- Upofu
- Ugonjwa wa kudumu wa figo
- Shambulio la moyo
- Watu kukatwa miguu Image ➡️Kwa mwaka 2019, takribani vifo millioni 1.5 Duniani vilichangiwa moja kwa moja na tatizo hili la kisukari.

➡️ Kuanzia mwaka 2000 hadi 2016, kuna ongezeko la 5% la vifo katika umri mdogo (premature death) kutokana na kisukari. Image
Jul 7, 2021 18 tweets 4 min read
#CORONA --- #UVIKO19 UZI 👉 Je dalili kwa sasa ni zipi? Zimebadirika ? Picha ya ugonjwa ukiambukizwa ni ipi kwa sasa? DALILI HUTOFAUTIANA KULINGANA UKALI WA UGONJWA?
✍️Tafiti kuhusu makali ya ugonjwa wa Korona-19 (UVIKO-19) yameonyesha makundi 3 ya wagonjwa

1. Ugonjwa usio mkali (81 kati ya 100)

2. Ugonjwa mkali maana mtu anahitaji oksijeni au 50% limeshambuliwa na ugonjwa (14 kati ya 100)
Feb 25, 2020 9 tweets 2 min read
Inaweza tokea katikati ya usingizi mtu hasa mtoto akawa na tabia ya kutembea,kuongea au kufanya vitendo vingin akiwa usingizini

Hii ni SLEEPWALKING

Hutokea zaid kwa watoto hasa wavulana,inahisiwa hutokea kwa sababu mfumo wa ubongo kudhibiti msawaziko wa kulala/kuamka haujakomaa Tabia ya kutembea au kuongea usingizini ikianza kwa mtu mzima inahusishwa na msongo mkubwa wa mawazo muda mwingine aina ya kifafa

🔵Tatizo la kutembea usingizini hutembea katika familia; 45% ya watoto wanaotembea usingizini pia na wazazi wao walitembea usingizini
Jan 28, 2020 14 tweets 4 min read
THREAD | MAMBO MUHIMU KUFAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO

KWANZA : Vidonda vya tumbo hutokea pale mfumo unaolinda kuta za tumbo unaposhindwa kazi hivyo asidi ya tumbo kuchoma kuta na kuleta kidonda/mchubuko.

🔵 Sababu kuu huwa ni maambukizi ya H. Pyroli na Dawa kundi la aspirin Mtu mwenye vidonda vya tumbo hupata shida kama:
1️⃣Maumivu makali ya tumbo yanayochoma mara nyingi eneo la chini ya chemba ya moyo
2️⃣Tumbo kujaa gesi
3️⃣Kiungulia
4️⃣Uchovu huweza kutokea kama kuna upungufu wa damu kutokana na vidonda
5️⃣Kinyesi cheusi humaanisha vidonda vinatoa damu