Dr. Norman Jonas Profile picture
Medical Doctor | Internal Medicine - Kilimanjaro Christian Medical University College | Always a Beautiful Day to Save Lives | norman.jonas@kcmuco.ac.tz

Oct 2, 2022, 17 tweets

#AfyaSwahili | OCTOBA - MWEZI WA UELEWA JUU YA SARATANI YA MATITI

➡️Uzi maalumu wenye jumbepicha ili kusaidia wanawake wapate kufahamu dalili za kansa

➡️Tafadhali sambaza isaidie wengi

Credit: Know Your Lemons

#BreastCancerAwarenessMonth

➡️Saratani ya titi ni kati ya saratani zinazowaathiri zaidi wanawake. (Namba 2 chini ya saratani ya shingo ya kizazi)

➡️Mwaka 2020 Tanzania kulikuwa na wagonjwa wapya 3992 wa saratani ya matiti (hawa ni wale waliofika kwenye vituo vya Afya) wengi huchelewa tiba

Uelewa ni muhimu

➡️Kuwa na uelewa kuhusu mwili wako na kuweza kugundua mabadiriko ni moja ya njia bora ya kulinda afya yako.

➡️Hii ina umuhimu mkubwa hasa linapokuja suala la matiti kwa wanawake.

Kwa wastani mwanamke 1 kati ya 8 huwa na uwezekano wa kupata saratani ya matiti kwa maisha.

KUCHUNGUZA SARATANI YA MATITI
1⃣Kujichunguza mwenyewe mara kwa mara kwa mara.
2⃣Uchunguzi wa kitabibu wa matiti kila mwaka.
3⃣Wanawake wote wenye umri kuanzia miaka 21 wajichunguze matiti yao siku ya 5-7 baada ya kumaliza hedhi mbele ya kioo.

DALILI 1 - UGUMU KWENYE TITI
➡️Saratani huweza kuja kama eneo gumu kwenye ngozi ya titi.

➡️Lakini sio kila ngozi ngumu kwenye titi ni saratani, huweza kutokea hata wakati wa hedhi au kunyonyesha.

➡️Ni muhimu hali hii kwenye titi kuangaliwa na daktari ili kujihakikishia.

DALILI 2 - KISHIMO KWENYE TITI (Dimple)

➡️Uvimbe wa saratani huweza kuvuta ngozi na tishu za titi ndani na kusababisha kishimo.

➡️Kishimo ambacho hakiondoki huweza kuwa dalili ya uvimbe ndani za titi hivyo huitaji uchunguzi.

DALILI 3 - UKOKO KWENYE CHUCHU (Crusty)
➡️Hali ya ukoko kwenye chuchu mara nyingi huwa sio tatizo kubwa, vilevile huweza kuwa dalili ya ugonjwa wa Paget.

➡️Seli za saratani ya ziwa huweza kuishi katika chuchu na kusababisha hali ya ukoko hasa wekundu ambao hautoki.

DALILI 4 - WEKUNDU KATIKA ZIWA
➡️Wekundu na ziwa kupata joto mara nyingi ni dalili ya maambukizi kwenye ziwa (mastitis) hasa wanaonyonyesha.

➡️Lakini kama matibabu hayasaidii; wekundu kwenye maeneo ya ziwa huweza kuwa dalili ya aina ya saratani (inflammatory breast cancer).

DALILI 5 - CHUCHU KUTOA MAJIMAJI
➡️Chuchu zinapoanza kutoa majimaji yanayotoka katika kipindi usipotarajia mfano: Huna maambukizi, huna ujauzito wala hunyonyeshi ni muhimu hiyo hali ikaangaliwa na daktari.

DALILI 6 - KIDONDA/VIDONDA KWENYE TITI

➡️Saratani ya matiti huweza kusababisha kidonda kwenye titi.

➡️Mara nyingi kidonda hiki huambatana na uvimbe mgumu ndani ya titi.

➡️Kadri muda unavyokwenda kidonda hiki huweza kuanza kutoa harufu.

DALILI 7 - UVIMBE/KIVIMBE KWENYE TITI

➡️Uvimbe mlaini kwenye ziwa huweza sababishwa na changamoto mbalimbali ambazo sio saratani.

➡️Lakini uvimbe ambao ni mgumu, pia haujongei ndani ya ziwa huweza kuwa saratani.

Ni muhimu kila uvimbe kuangaliwa na daktari.

DALILI 8 - CHUCHU KUINGIA NDANI

➡️Mabadiriko kwenye umbo la chuchu kama chuchu kuingia dani huweza kuwa dalili ya saratani.

➡️Uvimbe wa saratani ukiwa unakua ndani ya titi huvuta chuchu kuelekea kwake.

DALILI 9 - MSHIPA MPYA UNAOKUA KWENYE TITI

➡️Mara nyingi mtu anaponenepa au kunyonyesha matiti hupata mishipa ya damu inayoonekana kwenye ngozi.

➡️Lakini katika hali ambayo ni nadra sana; mshipa mpya kwenye ngozi ya titi huweza kuwa dalili ya saratani ya titi.

DALILI 10 - TITI KUBADILIKA UMBO AU UKUBWA
➡️Kwa kawaida ujauzito, unyonyeshaji au hedhi huja na mabadiriko ya umbo/ukubwa wa maziwa.

➡️Lakini iwapo titi moja bila kutarajia linapovimba, kubadiri umbo au kuanguka ni dalili inayohitaji uchunguzi.

DALILI 11 - NGOZI YA TITI KUWA KAMA GANDA LA CHUNGWA

➡️Ngozi ya titi mara nyingi ni laini.

➡️Inapotokea ngozi ya titi kuanza kupata mwonekano kama ganda ya chungwa huweza kuwa dalili ya saratani hasa aina inayoitwa "inflammatory breast cancer".

MUHIMU

⚠️Iwapo utagundua au utaona badiriko lolote kwenye matiti/titi ni muhimu kutopuuzia.

✍️Nenda Hospitali

✅Daktari atachukua historia yako na kukupima pia kuna vipimo muhimu kwenye uchunguzi kama mammogram utafanyiwa.

Saratani ya matiti inatibika, chukua hatua mapema, itambue na wahi kupata ushauri wa kitaalamu.

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling